Kwanini uchaguzi wa Merikani unaweza kuamua vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Iliyochapishwa

Rais atakayeingia White House katika miaka minne ijayo huenda atakuwa kiungo muhimu katika vita dhidi ya mabadiliko hatari ya hali ya hewa, wataalamu wanasema. Matt McGrath anatathimini uchaguzi wa Marekani na jinsi unavyohusiana na juhudi za uhifadhi wa mazingira.

Wanasayansi wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa wanasema kuchaguliwa tena kwa Donald Trump huenda "kukalemaza" jitihada za kupunguza ongezeko la joto duniani.

Wana hofu miaka mingine ya Trump huenda "kukaendeleza" matumizi ya mafuta yanayochangia hewa chafu kwa miongo kadhaa ijayo - hali itakayoimarisha miundo mbinu ya ukuzaji wa mafuta na gesi badala ya kuachana nayo kama wanavyotaka wanamazingira.

Wanasayansi wanasema mpango wa Joe Biden kuhusu masuala ya hali ya hewa utapatia ulimwengu nafasi ya kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Kando na kuiondoa Marekani katika makubaliano ya Paris - mkataba wa kimataifa uliobuniwa kuzuia ongezeko la joto duniani- Timu ya Rais Trump imekuwa ikifanya kila iwezekanalo kuondoa vikwazo ambavyo wanaonelea vitadhibiti ukuzaji wa kawi.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, watafiti katika Chuo Kikuu cha Colombia mjini New York wamekumbana na mabadiliko 160 ya kanuni za mazingira. Kanuni hizo zinajumuisha viwango vya mafuta ya gari, hadi uzalishaji wa methane, hadi balbu za taa.

Masuala haya yanaibuka wakati ambapo Marekani bado inajikokota kutoka kwa athari za miaka kadhaa zilizosababishwa na mioto ya nyikani katika majimbo ya magharibu. Baadhi ya wanasayansi wanahusisha mioto hiyo na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa hivyo tuko wapi katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi baada ya miaka minne ya Donald Trump - na mambo yatakuaje baada ya uchaguzi wa Novemba tarehe tatu?

Msimamo wa Trump kuhusu mabadiliko ya tabianchi ni upi?

"Trump anaamini kuwa kanuni zote ni gharama na hakuna faida," anasema Prof Michael Gerrard kutoka Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York.

"Anapinga uwepo wa mabadiliko ya tabianchi na kama ipo basi sio mbay hivyo. Anaamini kuna haja ya kuweka masharit ya kila aina na wala sio tu ya mazingira."

Wakosoaji wanasema hatua ya kuondoa baadhi ya masharti yanayolenga kuhifadhi mazingira ni sehemu ya ajenda ya serikali kuondoa hatua zilizopigwa katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa .

"Utawala wa Trump umefanya kila juhudi kutofautiana na masuala ya kisayansi na kuwadhalilisha wanasayansi," anasema Gina McCarthy, Mkuu wa zamani wa Shirika la kuhifadhi Mazingira (EPA) ambaye kwa sasa ni rais wa mfuko wa NRDC.

"Wamefanya kili jitihada kujaribu kuwashawishi watu kwamba kile wanachokiona na kuhisi na kuonja hakijitokezi mbele yao ."

Hatua ya Trump ilikuwa na athari gani?

Wafuasi wa Rais Trump watasema uungaji mkono wake wa ukuzaji wa mafuta umepata ufanisi .

Kutokana na mbinu ya ukuzaji wa mafuta kutokana na miamba ya mawe Marekani ilikuwa muuzaji mkubwa wa mafuta nje ya nchi duniani mwishoni mwa mwaka jana. Mbinu hiyo inayofahamika kama (Fracking) inajumuisha utumizi wa mbinu maalumu ya kutoa mafuta na gesi kutoka kwa mwamba wa mawe.

Lakini inapokuja suala la mkaa wa mawe, hali ni tofauti. Licha ya juhudi za utawala wa Trump kufanyia mabadiliko kanuni zilizowekwa, ufukuaji wa mkaa wa mawe umeendelea kushuka huku karibu ajira 5,000 zinazohusiana na ufukuaji wa mkaa wa mawe zikishuhuhudiwa sasa kuliko wakati Donald Trump aliposhaguliwa.

Kwa baadhi ya wale wanaomuunga mkono Trump, na vitendo vyake katika climate are consistent with boosting energy production and keeping the economy growing.

Wengine wanadai kuwa vita vya Trump dhidi ya kanuni za mazingira haihusiani kabisa na uchumi

"Trump anaamini mabadiliko ya tabia nchi ni suala la mabadiliko ya kiutamaduni ambayo inachochewa chuki kutoka kwa wapinzani wake ," anasema Paul Bledsoe, aliyehudumu kama mshauri katika utawala wa Clinton sasa ni mshauri wa Democrat, kutoka Taasisi Ya Sera ya Progressive.

"Kwa hivyo anaona hilo kama jitihada za kuzua uhasama miongoni mwa wafuasi wake. Haina manufaa yoyote kwake. Na hajali chochote kitakachotokea."

Kuondoka katika mkataba wa Paris kutakuwa na atharigani?

Hatua ya Rais Trump kuitoa Marekani katika makubaliano ya Paris ilikuwa ujumbe mkubwa kwa ulimwengu kwamba nchi hiyo haikubaliani na suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Akitangaza kujiondo kwenye makubaliano hayo, Bw. Trump alizungumzia haja ya kujadiliana umpya yaliyomo kwenye mkataba huo, lakini pendekezo hilo halikuangaziwa.

Baadhi ya waangalizi wanaamini hatua ya Marekani imefanya nchi zingine kama Brazil na Saudi Arabia, kukata pole pole uzalishaji wa kaboni.

"Kwa sasa, tuna sua sua na ni aibu sana kutafakari kuwa Marekani inaweza kujipata katika hali kama hiyo," anasema Gina McCarthy.

"Na hiyo yote ni kwa sababu tuna rais ambaye hajali maslahi ya watu wote. Anachotilia maanani ni wale tu wanaomuunga mkono."

Ikiwa Joe Biden atashinda, itabatilisha uamuzi wa kuiondoa Marekani katika mkataba wa Paris hark iwezekanavyo. Kujiunga tena na mkataba huo kunahitaji notisi ya mwezi mmoja tu.

Nini kitafanyika ikiwa Trump itachaguliwa tena?

Ushindi wa Trump utakuwa ishara ya kuunga mkono hatua yake ya kujiondoa Marekani katika mkataba wa Paris, hali ambayo itachangia ukuzaji zaidi wa mafuto kutoka kwenye miamba. Hatua hiyo bila shaka itakuwa na athari kubwa katika juhudi zakudhibiti viwango vya joto duniani.

"Ni vigumu kufikia lengo la kupunguza viwango vya joto chini ya nyuzi joto 1.5 kwa sasa, japo kuna uwezekanao wa kufikia lengo hilo kinadharia," anasema Michael Gerrard.

Alikuwa anaangazia moja ya malengo katika makubaliano ya Paris- ogezeko la joto duniani kupita nyuzi joto 1.5 kunachukuliwa kama moja ya chanzo cha ongezeko hatari la viwango vya joto.

Miaka miwili iliyopita, uchanganuzi wa kisayansi wa kutathimini kufikiwa kwa lengo la kudhibiti ongezeko la viwango vya joto ulibaini kuwa hatua hiyo italeta mabadiliko chanya kwa watu na mazingira.

"Ikiwa Trump atachaguliwa tena, nadhani itakuwa vigumu kuishawishi Marekani kuunga mkono mkataba huo," anasema Prof Gerrard.

"Itabidi tusubiri kwa miaka mingine minne kufanyika kwa uchaguzi mwingine kujaribu kurekebisha hitilafu hiyo, na kufikia muda huo miundo mbinu ya ukuzaji mafuta kutoka kwa miamba itakuwa imeimarishwa. Hii inamaanisha gesi chafu nyingi itakuwa imeathiri mazingira. Kwa hivyo, itakuwa habari mbaya sana kwa wanaharakati wa mazingira."

Biden anatofautiana vipi na Trump?

Joe Biden anasema mango wake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi utaiwezesha sekta ya kawi ya Marekani kutozalisha hewa ya kabuki kufikia mwaka 2035. Hatua hiyo itaiwezesha nchi hiyo kufikia malengo kutozalisha kabisa hewa chafu kufikia mwaka 2050.

Mr Biden has ambitious ideas to revolutionise transport in the US using electric vehicles and trains. Pia anataka kujenga makazi milioni 1.5.

Mpango wake hautawafaidi wafuasi wake tu bali pia utawanufaisha Wamarekani wote, wafuasi wake wanasema, utasaidia kuleta chini viwango vya joto.

"Huu ni uchaguzi wa kwanza amber huenda ukaamua mustakabali wa mabadiliko ya tabia nchi," anasema Paul Bledsoe.

"Joe Biden anapendekeza Marekani izilipishe ushuru wa mabadiliko ya hali ya hewa nchi ambazo hazitapunguza uzalishaji wa kaboni. Mpango wa kimataifa wa Biden kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa vumepatia kipaumbele kuliko mipango ya ndani.Kwa hivyo hakuna mjadala kati ya wawili hao kuhusu suala hilo"

Rais Trump ametuhumu mpinzani wake kwamba anataka kupiga marufuku mbinu ya uzalishaji mafuta kutoka kwa miamba. Lakini Biden anasema mbinu hiyo itaendelea wakati ambapo Marekani inajiandaa kwa uchumi wa kijani.

Msimamo wa makundi ya kidini ni upi kuhusu suala la mazingira?

Wakristo wa dhehebu la Kianglikana ni miongoni mwa makundi ya kidini yanayomuunga mkoni Rais Trump. Kura za maoni zinaashiria huenda yakajitokeza tena kumpigia kura kwa wingi.

Lakini waumini vijana wa kanisa la kianglikana wamejitenga na Trump, hususan kuhusiana na suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Emily Robertson ni mwnafunzi mwenye umri wa miaka 21- katika taasisi ya Covenant mjini Lookout Mountain, Georgia, na anapiga kura mara ya kwanza katika uchaguzi huu.

Anasema kama angelipiga kura katika uchaguzi mkuu uliyopita huenda angelimpigia Trump, kama walivyofanya wazazi wake.

Lakini katakana na Helena wake kuhusu masuala ya mabadiko ya tabia nchi ameshawishika kumpigia kura Joe Biden mara hii.

Licha ya kuwa ongezeko la uelewa wa suala hilo muhimu, anaamini baadhi ya vijana Wakristo wenzake bado watamuunga mkono rais Trump.

"Katika mitandao ya kijamii, nimeona vijana wengi wakiwashawishi wenzao kumpigia kura Biden, lakini katika maeneo machache," anasema.

"Kwa baadhi ya watu,pengine huenda wakafanya hivyo lakini hata wale nimejaribu kusema nao, japo wanaelewa athari za mabadiliko ya tabia nchi, sidhani watashawishika kumpigia kura Biden badala ya Trump."