Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uhifadhi: Daraja la matumaini kwa nyani adimu duniani
Kwa nyani aina ya gibbon kuruka kutoka mti mmoja hadi mwingine ni jambo la kawaida.
Lakini hilo haliwezekani kukitokea maporomoko ya udongo ambayo husababisha mianya mikubwa katika misitu, na kuwafanya washindwe kuzunguka na kufika mbali kutafuta chakula na ''wapenzi'' wao.
Kwa nyani hao adimu duniani, suluhisho la muda sasa limepatikana: daraja la kamba inayounganisha miti.
Na wanasayansi wamewanasa kwenye kanda ya video nyani aina ya gibbon, wakipanada na kubembea kutoka sehemu moja ya msitu hadi nyingine kwa sekunde kadhaa.
Baadhi yao walitumia kamba kama kiunganishi, wengine wakitumia mikono yao kubembea ama kutembea juu ya kamba iliyofungwa kati ya msitu mmoja hadi mwingine.
Nyani hao wanapatikana katika misitu ya China katika Hainan.
Wote tisa katika kundi hilo wamejifunza kutumia kamba isipokuwa mmoja wa kiume ambaye huruka kutoka mti mmoja hadi mwingine, wakati mwingine akiandamana nyani wadogo wanaofurahia kufanya hivyo.
Wanasayansi wa uhifadhi wa mazingira wanasema ujenzi wa daraa la urefu wa mita 18 huenda ukaokoa maisha ya wanyama tofauti huku misitu ikipata nafasi ya kunawiri na kurejelea hali yake ya asilia.
Idadi ndogo ya nyani hao, wakiwamo orangutan, wameonekana kutumia madaraja bandi aya kamba. Lakini hii ni mara ya kwanza Hainan Gibbon wamejifunza kutumia kamba.
Mpango wa uhifadhi unaoendenshwa na shamba la Kadoorie bustabi ya Botanic huko Hong Kong unajaribu kuokoa spishi hiyo adimu ya nyani wasiangamie.
Dk Bosco Chan anasema daraja la kamba litasaidia kuongeza idadi ya nyani hao na jitihada za uhifadhi.
"Nilipoanza kufanya kazi katika hifadhi hii, 2003, tulikuwa na makundi mawili yaliyokuwa na nyani 13 ambao wamesalia kote ulimwenguni," aliambia BBC.
"Idadi ya gibbon imeendelea kuimarika, huku thuluthi moja na makundi ya familia nne zikibuniwa mwaka 2011 na 2015, mtawalio.
"Mwanzoni mwa mwaka 2020, tulibaini kubuniwa kwa kundi la tano, idadi ya nyani hao ikiongezeka hadi 30. Inaonesha spishi hiyo imeanza kukua hali inayotupatia matumaini."
Kukuza upya misitu inatakiwa kupewa kipaumbele ili kuzuia spishi kuangamia, aliongeza.
"Tunahitaji kuhakikisha tunadhibiti uwindaji haramu, kupanua misitu ambayo ndio makazi asilia ya makundi ya gibbon yanayotarajiwa kubuniwa siku za usoni ili kuepusha hatari ya kuangamia kwao. "
Wanyama hao ambao walikuwa wakipatikana kwa urahisi katika maeneo tofauti nchini China, sasa wamehifadhiwa katika msiti mmoja wa kisiwa cha bahari ya kusini mwa China.
Ndani ya makazi yao asilia, wanatembea juu ya miti kutoka eneo moja hadi lingine. Misitu aili na ile iliyopandwa na binadamu, inaweza kuwazuilia mahali pamoja, hali ambayo inaathiri kuzaana kwao na kuwaweka katik ahatari ya kuvamiwa.
Karibu spishi 20 za gibbon wanaishi kote ulimwenguni, kutoka kaskazini mashariki mwa India hadi Borneo. Baadhi yao wanakabiliwa na hatari ya kuangamia kutokana na uharibifu wa misitu, uwindaji na biashara haramu.
Spishi mbili za gibbon hivi karibuni zilitoweka China na spishi za China zilizosalia wakiwamo Hainan Gibbon (Nomascus hainanus), wameorodheshwa kuwa katika hatari ya kuangamia na Muungano wa Kimataifa wa uhifadi wa wanama na mazingira asilia.
Utafiti huo umechapishwa katika jarida la kisayansi.