Virusi vya corona: Utaratibu unaotumiwa na mbwa kugundua virusi siku tano kabla ya mtu kuonesha dalali ya maambukizi

Iliyochapishwa

Je covid-19 ina harufu?

Hilo ni jibu ambalo mbwa tu anaweza kutupa kwa usahihi.

Uwezo wa mnyama huyo umbaye anafugwa nyumbani na baadhi ya watu umegeuka kuwa kifaa cha kudhibiti janga la covid-19, ambalo tayari umesababisha maambukizo zaidi ya milioni 20 na vifo vya watu zaidi ya milioni moja duniani.

Mamlaka katika nchi kama vile Finland, Lebanon, Argentina, Chile, Ujerumani, Marekani, Colombia na Mexico, zimekuwa zikiwapa mbwa mafunzo ya kuwawezesha kugundua ikiwa watu wameambukizwa virusi vya corona.

Wiki chache zilizopita mbwa waliopewa mafunzo maalum ya kunusa harufu ya COVID-19 walianza majaribio ya kuwakagua abiria waliojitolea katika uwanja wa ndege wa Vantaa nchini Finland kama sehemu ya mpango wa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Mtafiti anayeongoza utafiti huo anasema majaribio hayo yameonesha matokeo ya kufana lakini usahihi wa mbwa hao bado haujathibitishwa.

Kwa mujibu wa Profesa Anna Hielm-Bjorkman kutoka Chuo Kikuu cha Helsinki, mbwa wanaweza kugundua virusi kwa wanadamu siku tano kabla ya dalili kujitokeza.

"Ni wazuri sana [kugundua virusi vya corona]. kwa karibu asilimia 100% ,"anasema.

Kwa upande wake, Felipe Valencia, daktari wa mifugo na mtaalamu wa kutoa mafunzo maalum kwa mbwa na ambaye anaendesha mpango sawia na huo katika Chuo Kikuu cha Antioquianchini humo, anabainisha kuwa uwezo wa mbwa unaweza kuwafanya waaminike sana katika visa hivi.

" Mbwa hutumia asilimia 40 ya ubongo wao kung'amua harufu kwa kunusa, kwa hivyo wanaweza kutumiwa kudhibiti ugonjwa," alisema.

"Covid-19 sio janga": wanasayansi wanaoamini kuwa virusi vya corona ni mchanganyiko wa magonjwa (na hii inamaanisha nini kwa matibabu yake)

Madhumini ya baadhi ya mipango hiyo ni kutumia mbwa katika maeneo ambayo yanatumiwa na wageni kuingia nchini, kama vile viwanja vya ndege au vituo vya treni, ili kuwawezesha watu kutangamana bila haja ya kuweka vikwazo au kuwazuilia watu mahali pamoja.

Lakini mbwa wanaweza vipi kugundua covid-19?

Jasho na machozi

Kulingana na tafiti tofauti, ni vigumu kubaini kile mbwa wanachonusa.

Kama alivyoangazia katika makala yake Dk. Susan Hazel, daktari wa mifugo katika Chuo Kikuu cha Adelaide nchini Australia "Mbwa hao wamefunzwa kunusa harufu ya virusi vya corona", kile wanachonusa ni sampuli ya jasho kutoka kwa watu ili kubaini ikiwa wameambukizwa au la.

Dk. Susan Hazel pia anasema kuwa mbwa wana karibu vipokezi harufu milioni 220 kwenye pua zao ambayo inawawezesha kung'amua mabadiliko ya harufu katika vitu.

Wataalamu kutoka Chile wanatumia mafunzo aina moja ya mbwa kubaini harufu ya covid-19 huku wale kutoka nchi zingine wakiwfunza mbwa kubaini covid-19 kwa watu ambao huenda wameambukizwa corona lakini hawajaonesha dalili.

"Haimanishi kuwa virusi vina aina fulani ya harufu, lakini ukweli ni kwamba athari inayojionesha kwa mtu aliye na maambukizo ndio hugunduliwa ," daktari wa wanyama Fernando Madrones, kutoka Chuo Kikuu cha Katoliki nchini Chile, aliambia mtandao wa Diario.es portal.

Katika tafiti kadhaa duniani mikojo mate na jasho hutumiwa kubaini Covid-19.

Pia unaweza kutazama: