Mwanamume aambukizwa corona mara ya pili - Kwanini maambukizi ya pili ni hatari zaidi?

Iliyochapishwa

Mwanaume mmoja nchini Marekani amepata maambukizi mara ya pili, huku kuugua kwake mara ya pili ku kiwa kwa hatari zaidi kuliko alipopata maambukizi mara ya kwanza, madaktari wameripoti.

Mtu huyo mwenye miaka 25 alihitaji tiba ya hospitalini baada ya mapafu yake kushindwa kupata hewa ya oksijeni ya kutosha ndani ya mwili wake.

Maambukizi ya mara ya pili yameendelea kuwa nadra kutokea na sasa mwanaume huyo amepona.

Lakini utafiti katika idara ya magonjwa ya kuambukiza ya Lancet, unatoa maswali kwamba ni kwa kiasi gani kinga inaweza kujengwa kutokana na virusi hivyo.

Mwanaume huyo mkazi wa mji wa Nevada hakuwa na maradhi yoyote ya kiafya yaliyokuwa yakifahamika au changamoto za kinga ambazo zingemfanya mwili wake kushindwa kupambana na ugonjwa wa Covid-19.

Nini kilichotokea na lini

• 25 Machi - Wimbi la kwanza la dalili ikiwemo maumivu ya koo, kukohoa, maumivu ya kichwa, kuharisha na kichefuchefu.

• 18 Aprili - Alipimwa na kukutwa na maambukizi kwa mara ya kwanza.

• 27 Aprili - Dalili za awali ziliondoka

• 9 na 26 mwezi Mei- Alipimwa na kukutwa hana ugonjwa wa Covid-19 kwa nyakati mbili tofauti.

• 28 Mei - Alianza kupata tena dalili za maambukizi, awamu hii ikiwemo homa, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kikohozi, kichefuchefu na kuharisha.

• 5 Juni - Alipimwa na kukutwa na maambukizi kwa mara ya pili , na kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni kwenye damu huku akiwa na shida ya kupumua.

Wanasayansi wanasema mgonjwa huyo alikutwa na virusi vya corona mara mbili na si kuwa kwamba awali hakupona kisha ugonjwa ukajionesha tena.

Tofauti ya kipimo cha kijenetiki kilichochukuliwa wakati wa dalili za kwanza na za mara ya pili kinaonesha kuthibitisha kuwa sababu za maambukizi ni tofauti.

''Tulichogundua kinaashiria kuwa maambukizi ya awali si lazima yakukinge dhidi ya maambukizi mengine siku za usoni,'' allisema Dkt Mark Pandori wa Chuo Kikuu cha Nevanda.

''Uwezekano wa kuambukizwa tena kunaweza kuwa na athari kwa kuelewa kuhusu kinga itokanayo na kuugua Covid-19''.

Amesema watu wanaopona wanapaswa kuendelea kufuata masharti kama ya kutotangamana, kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara na maji tiririka.

Uchambuzi wa James Gallagher

Mwandishi wa habari wa masuala ya afya

Wanasayansi bado wanatafiti kujua suala la virusi vya corona na kinga.

Kuna mtu yeyote huwa na kinga? Hata kwa wale wasio na dalili kali? Ni kwa muda gani kinga hiyo itadumu?

Haya ni maswali muhimu ili kuelewa namna gani virusi vitatuathiri kwa muda mrefu na vinaweza kuwa chachu ya mchakato wa kupata chanjo .

Mpaka sasa maambukizi ya mara ya pili yanaonekana kuwa nadra -kumekuwa na mifano michache kati ya maambukizi ya watu milioni 37 yaliyothibitishwa.

Ripoti huko Hong Kong, Ubelgiji na Uholanzi zinasema kuwa hakukuwa na maambukizi mengine kuliko ya kwanza, nchini Ecuador kulikuwa na maambukizi ya mara ya pili yaliyokuwa mabaya zaidi kuliko awali lakini hayakuhitaji tiba ya hospitali, sambamba na Marekani hali ilikuwa hivyohivyo.

Hata hivyo, ni mapema kwa janga hili, na historia ya aina nyingine ya magonjwa yanayosababishwa na virusi vya corona kusema kuwa janga limepungua.

Wakati nchi kadhaa zikikabiliwa na wimbi la pili la virusi hivyo, tunaweza kupata majibu sahihi.Eneo hatari zaidi kwa wanawake