Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Je nini kinachowasubiri wanafunzi shuleni Kenya?
Shule huenda zikafunguliwa wakati wowote nchini Kenya baada ya kufungwa mapema mwezi Machi kutokana na kuzuka kwa mlipuko wa virusi vya corona.
Hii ni baada ya mpango wa kuzifungua hii leo Jumtatu tarehe 12 mwezi wa kumi, kusitishwa kwa muda kufuatia majadiliano kuhusu hatua zilizochukuliwa na wazazi pamoja na serikali ili kuhakikishia usalama wao wanafunzi.
Hatahivyo ni wanafunzi wa madarasa ya nne, wale wa darasa la nane na wenzao wa kidato cha nne waliotakiwa kuripoti shuleni.
Baadhi ya wanafunzi katika shule za kibinafsi hatahivyo watalazimilka kusalia majumbani baada ya wamiliki wa shule hizo kuzibadilisha na kuzifanya maeneo ya biashara.
Hali hiyo inawalazimu wanafunzi waliokuwa katika shule zilizofungwa kutafuta maeneo mbadala.
Cha kusikitisha ni kwamba wazazai wengi wana wasiwasi kuhusu hali ya usalama wa wanao huku wengi wakishindwa kutafuta karo na kununua vifaa vya kusomea.
Wengi wa wazazi hawa hawakutarajia kufunguliwa kwa shule na kwamba walidhani hali iliopo hivi sasa itaendelea hadi mwaka ujao.
Wengine wanalalamika kwamba kufungwa kwa sehemu nyingi za kufanyia kazi mbali na masharti makali ya kukabiliana na virusi vya corona yaliotolewa na serikali kumesababisha hali ngumu ya kiuchumi.
"Unawezaje kumpa mzazi wiki moja kufungua shule ambazo zilikuwa zimefungwa kwa miezi kadhaa wakitarajiwa kununua sare mpya za shule na kulipa karo?, aliuliza mzazi mmoja
Je ni nini ambacho wanafunzi hawa watakumbana nacho shuleni?
- Shule zitalazimika kutoa maji safi katika lango lake kuu , huku wanafunzi wakitakiwa kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia , kuvalia barakoa mbali na kufanyiwa vipimo vya kiwango cha joto mwilini.
- Wanafunzi watakaopatikana na dalili zinazohusishwa na virusi vya corona watatengwa na kupelekwa katika eneo tofauti la shule wakisubiri kurudishwa nyumbani.
- Mbali na kwamba wanafunzi hao wanapaswa kuvalia barakoa ili kujikinga na corona pia watalazimika kukaa mbalimbali ndani na hata nje ya darasa, huku wakilizimika kutocheza pamoja .