Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Utafiti wasema virusi hivyo vimebainika kuishi kwa siku 28
Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19 vinaweza kubaki kwenye vitu kama fedha za karatasi, vioo vya simu na kwenye chuma kisichoshika kutu kwa siku 28, watafiti wameeleza.
Matokeo hayo ya shirika la kisayansi la taifa nchini Australia yanasema kuwa virusi vya SARS-Cov-2 vinaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyofikiriwa.
Hatahivyo, jaribio hilo lilifanyika katika mazingira ya giza kwani mwanga wa UV tayari ulishaonesha kuua virusi.
Baadhi ya wataalamu wameonesha mashaka kuhusu tishio la maambukizi kupitia vitu hivyo katika maisha ya kawaida.
Virusi vya corona huambukiza watu wanapokohoa , kupiga chafya au kuzungumza.
Lakini pia kuna ushahidi kuwa virusi vinaweza kusambazwa kwa chembechembe zilizo kwenye hewa. Pia inawezekana kuwa mtu anaweza kupata maambukizi kwa kugusa vitu au maeneo yenye virusi kama chuma au plastiki kwa mujibu wa vituo vya kudhibiti magonjwa vya nchini Marekani.
Utafiti unasema nini?
Majaribio ya maabara awali yalibaini kuwa SARS-Cov-2 vinaweza kuishi kwa siku mbili mpaka tatu kwenye fedha za karatasi na kioo, na mpaka siku sita kwenye plastiki na chuma kisichoshika kutu, ingawa matokeo yanatofautiana.
Hatahivyo, utafiti wa shirika la Australia CSIRO ulibaini kuwa virusi ni ''imara sana'' vinaishi kwa siku 28 kwenye maeneo yasiyo magumu kama kioo cha simu, fedha za karatasi na plastiki , pale vinapowekwa kwenye mazingira ya nyuzi joto 20C na kwenye giza.
Kwa ulinganisho, virusi vinavyosababisha mafua vinaweza kuishi kwenye mazingira kama hayo kwa siku 17.
Utafiti huo, uliochapishwa katika Jarida la linaloeleza masuala ya stadi za virusi, pia uligundua SARS-Cov-2 viliishi kwa muda mfupi kwenye mazingira ya joto kuliko kwenye mazingira ya baridi viliacha kuambukiza ndani ya saa 24 kwa 40C vilipokuwa kwenye vitu vilevile.
Pia vilikaa kwa muda mrefu kwenye nyuso laini, zisizo za ngozi kuliko kwenye vifaa kama kitambaa, ambapo iligundulika kuwa hakibebi virusi vyovyote vya maambukizi siku 14 zilizopita.
Utafiti huu haukubaliani kwenye masuala gani?
Profesa Ron Eccles, Mkurugenzi wa zamani wa kituo kinachotafiti maradhi ya mafua katika Chuo kikuu cha Cardiff , amekosoa utafiti na kusema kuwa kusema kuwa virusi vinaweza kuishi hai kwa siku 28 ''ni kusababisha hofu isiyo ya lazima kwa Umma''.
"Virusi huenea kwenye nyuso kutoka kwenye kamasi kwenye kikohozi na kupiga chafya na vidole vichafu na utafiti huu haukutumia kamasi mpya ya binadamu kama chanzo cha kueneza virusi," alisema.
''Kwa maoni yangu virusi vinaishi kwa saa kadhaa kwenye kamasi kwenye vitu kuliko siku kadhaa.''
Katika jarida lililochapishwa na Lancet mwezi Julai, Emanuel Goldman, Profesa wa stadi za vijidudu katika chuo cha Rutgers alisema '' nafasi ya maambukizi kupitia vitu mbalimbali ni ndogo mno''.
Alisema tafiti ambazo zilisema kuna hatari kubwa zilikuwa zimeundwa kwa ''kutokuwepo mazingira halisi ya maisha''. "kufanana kidogo na hali halisi za maisha".
Juma lililopita Profesa wa masuala ya dawa katika Chuo Kikuu cha Carlifonia Monica Gandhi alisema kuwa virusi vya corona havisambai kupitia vitu kama noti na maeneo mengine.