Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
August Browne: Mzaliwa wa Nigeria aliyepigania uhuru kwa kuungana na kikosi cha Poland
- Author, Na Nicholas Boston
- Nafasi, Chuo kikuu cha mji wa New York
- Iliyochapishwa
Miongoni mwa mamia ya maelfu ya wazalendo wanaosherehekewa huko Poland kama wapiganiaji uhuru katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ni raia mmoja mweusi mzaliwa wa Nigeria.
Mwanamuziki wa mtindo aina ya Jazz, August Agboola Browne alikuwa katika umri wa miaka ya 40, na alikuwa ameishi Poland kwa miaka 17, alipojiungana na wapiganiaji uhuru dhidi ya utawala wa Wanazi mwaka 1939 - na inasemekana kwamba ndio mtu mweusi pekee nchini humo kufanya hivyo.
Jina la siri alilopewa "Ali", alipigania nchi yake ya kuasili wakati wa 'Vuguvugu la Warsaw', pale Ujerumani ilipoivamia, ambavyo vilimalizika miaka 76 iliyopita.
Ambalo bado ni fumbo ni kwamba alinusurika vita hiyo licha ya wakaazi asilimia 94 wa Poland ama waliuawa au kutoroka makazi yao na kuendelea kuishi katika mji ulioharibika hadi mwaka 1956 alipohamia Uingereza na mke wake wa pili.
Mnara mdogo huko Warsaw sasa hivi una kumbukumbu ya maisha ya Browne. Lakini taarifa chache kumuhusu huenda hangejulikana ikiwa sio kwa ombi alilotuma la kutaka kujiunga na chama cha wapiganiaji uhuru mwaka 1949.
Fomu hiyo ilihifadhiwa kwa miongo 6 hadi 2009, pale Zbigniew Osinski kutoka Makumbusho ya Warsaw alipoipata.
Fomu hiyo iliyojazwa kwa maandishi ya kupendeza na yenye picha mfano wa ile ya pasipoti iliyoambatanishwa kwenye kona, na katika jiwe lake la Rosetta - nyaraka hiyo iliyoongoza watafiti kufasiri mambo ya kweli kuhusu maisha yake na kujua pale kizazi chake kinapoishi.
Kwenye picha, Browne, akiwa amevalia jaketi na lililomkaa vizuri, anaonekana mcheshi na kijana na tabasamu kidogo usoni mwake.
Wote waliokutana na Browne wanamuelezea kama kijana mtanashati na ambaye mavazi yake yalikuwa yakuvutia.
Hadi kufikia wakati huo alikuwa kwenye miaka ya 50 kulingana na fomu hizo zinazoonesha kwamba alizaliwa Julai 22, 1895 hadi Wallace na Jozefina huko Lagos - wakati huo ikiwa sehemu ya Milki ya Uingereza.
Aliwasili England akiwa kwenye meli ya Uingereza akiwa ameandamana na baba yake baharia mzoefu. Kutokea hapo, alijiunga na kundi la wasanii lililokuwa linazuru Ulaya na kuishia kufika Poland kupitia Ujerumani.
'Aliwapa hifadhi wakimbizi wa ghetto'
Lakini kinachooumisha kichwa zaidi, fomu hiyo haioneshi ni kitu gani kilichompa hamasa ya kuondoka Nigeria au kufika Poland na kuchagua nchi hiyo kama makazi yake, hiyo basi pengine ilikuwa ni hamu ya kutaka kujua maeneo.
Kufikia miaka ya 1930, alikuwa mwanamuziki maarufu aliyecheza muziki katika migahawani mbalimbali nchini humo.
Alichoandika Browne ni kwamba wakati wa mapigano alisambaza magazeti kwa njia ya chini ya ardhi, alifanya biashara ya elektroniki na "kuwapa hifadhi wakimbizi kutoka ghetto".
Hili lilikuwa eneo lililotengwa la mji ambapo Wayahudi walilazimishwa na Wanazi kuishi na ambapo 91,000 kati yao walikufa kwa njaa, magonjwa na kuuawa.
Baadhi ya Wayahudi 300,000 walisafirishwa na kupata mauti yao katika kambi za Wanazi zilizokuwa zimesongamana.
Vuguvugu la Warsaw
Agosti -October 1944
- Jeshi Poland lilivamia maeneo yaliyokuwa yamekaliwa na vikosi vya Ujerumani Agosti 1
- Kwa haraka wakachukua udhibiti wa maeneo mengi ya mji huo
- Ujerumani ilituma vikosi vyake na jeshi jirani la Usovieti halikusaidia
- Wapoland wakajisalimisha Oktoba 2 baada ya siku 63
- Raia 200,000 na wapiganaji 16,000 wa Poland walifariki dunia
Chanzo: Encyclopaedia Britannica na kumbukumbu ya Warsaw
Inaonekana kwamba Browne kusalia Poland baada ya vita kulikuwa kupenda kwake - kwasababu kama raia wa Milki ya Uingereza alikuwa na fursa ya kuondoka.
Alipowasili Poland, kwanza aliishi Krakow ambapo alioa mke wake wa kwanza, Zofia Pykowna, na kujaaliwa naye watoto wawili, Ryszard na Aleksander.
Kwa bahati mbaya ndoa yake haikudumu lakini vita vilipotokea, Browne alifanya mipango watoto wake na mama yao wakapata hifadhi Uingereza.
Lakini - pengine kwasababu alikuwa amejitolea kupigania uhuru wa Poland, Browne hakuandamana nao.
Taarifa ambazo hazijakamilika zinazua maswali mengi kuhusu maisha yake.
'Mwanaume mkimya aliyependa maisha yake kuwa faragha'
Tatiana, binti yake wa mke wa pili Olga Miechowicz, ndoa iliyodumu kwa muda mrefu, alizaliwa na kukuzwa mji wa London na ndio mtoto pekee aliyehai hivi sasa nchini Uingereza.
Anasema baba yake hakuwahi kuzungumzia kilichotokea.
Sasa hivi ana umri wa kiama 61 - baba yake alikufa waka 1976 alipokuwa na umri wa miaka 17.
Anamkumbuka kama mtu mkinya, ambaye hakupenda kuzungumzia maisha yake na kwamba hakuwahi kusimulia yaliyotokea akiwa Poland au miaka yake ya awali huko Lagos.
Tatiana hajui kwanini wazazi wake wote hawakumuelezea mengi yaliyotokea siku za nyuma.
Anashuku kwamba hilo lilitokana na haja ya kutaka kusahau machungu waliopitia na madhila walioshuhudia.
Anakumbuka akitazama makala ya vita hivyo akiwa na wazazi wake na kama yake akasema: "Nakumbuka kuona watu waliotundikwa barabarani; Najua huo ni ukweli kwasababu nilshuhdudia hilo kwa macho yangu mawili."
Lakini hakukuwa na mazungumzo zaidi ya hapo na sasa hivi anatamani kama angalau wangemuelezea zaidi.
Ingawa Browne, hakuwa kupuuza utamaduni wa Poland ambako alikuwa ameishi kwa miaka 35, na Tatiana anasema kwamba Poland ndio lugha pekee iliyokuwa inazungumzwa katika makazi yao ya Uingereza.
Alikumbukwa na waliomfahamu huko Poland kwa kuzungumza "lugha asili ya Poland, yenye lahaja ya Warsaw".
Pia alikuwa anazungumza lugha kadhaa kwa ufasaha.
"Baba alinifunza namna ya kuandika na kusoma lugha ya Poland," Tatiana anasema.
'Mwepesi wa mambo na mcheshi'
Namna mwanamuziki, ambaye kama mtu mweusi alikuwa rahisi kutambulika alivyoweza kunusurika wakati wa utawala wa Wanazi huko Poland bado ni fumbo.
Wanaume wengine wawili weusi, Jozef Diak kutoka Sudan, na Sam Sandi, ambaye asili yake bado haitambuliki, walivyonusurika katika jeshi la Poland wakati wa Vita vya Poland-Bolshevik (1919-1921) na baadae wakasalia Warsaw lakini wote wakafariki dunia kabla ya kuanza kwa vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Wao pamoja na Bwana Browne, wataalamu wanasema huenda kulikuwa na watu wengine wawili weusi wakaazi wa Warsaw miaka ya vita, wataalamu wa burudani ambao hawakupatikana tena wakati wa vita.
Lakini kumbukumbu ya Tatiana kuhusu ucheshi wa baba yake huenda kukamdokezea vile baba alivyoweza kuvumilia.
"Baba yangu alikuwa mwepesi wa mambo na mcheshi," Tatiana anasema.
"Tulipokuwa tunaenda kanisani Jumapili, Nilikuwa nikimuona akizungumza sana na watu wengine. Kiuhalisia alikuwa muungwana na moja kwa moja kungekuvutia kumpenda.
"Alipokuwa kwenye kazini na watu wengine,alikuwa mcheshi na mwenye nguvu ya kipekee. Watu walimpenda sana."
Simulizi ya Brown ilijitokeza mwaka 2009 kulipokuwa na gumzo lililotanda kote nchini humo kuhusu wazalendo na ubaguzi dhidi ya wageni huko Poland.
Gumzo hilo lilianza kujadiliwa katika majukwaa yote ya kisiasa na kukawa na wito wa kumkumbuka kama shujaa wa taifa.
Wakati huo, aliyekuwa rais Lech Kaczynski, mwanzilishi mwenza wa chama cha Haki conservative Law and Justice alitaka kumtunuku katika maadhimisho ya miaka 65 ya 'Vuguvugu la Warsaw', alisema Krzysztof Karpinski, wanahistoria wa muziki wa jazz aliyehudumu kama makamu rais wa Chama cha Muziki wa Jazz Poland, kilichopigiwa simu na ofisi ya Kaczynski kwa maelezo zaidi kumhusu Browne.
Kaczynski alifariki katika ajali ya ndege mwaka 2010 na kwa bahati mbaya akawa ameenda na mpango huo.
Lakini mwaka jana mnara dogo wa raia wa Poland wenye asili ya Nigeria August Browne aliyepigania uhuru hatimae ukazinduliwa
Mnara huo ulizunduliwa na shirika lisilo la kifaida.
Waliopigania uhuru wanaenziwa na wenye msimamo mkali na wanaotaka mabadiliko kama ishara ya Poland ya sasa.
Browne aliishi maisha ya unyenyekevu Uingereza kwa miongo miwili. Aliendelea kuishi kama mwanamuziki na alipokuwa mzee, alikuwa akitoa mafunzo ya kucheza piano nyumbani kwake, kulingana na binti yake Tatiana.
Walikuwa wakiishi kama familia yenye upendo, amesema daktari Michael Modell aliyemtibu Browne ugonjwa wa saratani.
Alikufa akiwa na umri wa miaka 81 mwaka 1976 na kuzikwa kaskazini mwa London.