Raia wa Iraq wauawa katika shambulio la roketi karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad

Iliyochapishwa

Raia watano wa Iraqi wameuawa baada ya roketi kurushwa kwenye nyumba iliyokuwa karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, jeshi la Iraqi limesema.

Waathirika walikuwa wanawake wawili na watoto watatu kutoka kwa familia moja. Watoto wengine wawili walipata majeraa.

Hakuna kundi ambalo limedai kurusha roketi hiyo lakini uwanja wa ndege ikiwemo kambi ya jeshi ya Marekani, mara nyingi nyingi ndio inayolengwa na kulaumiwa wanamgambo wanaounga mkono Iran wanaopigwa na Marekani.

Hii ilikuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa raia wa kawaida kujeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Iraqi Mustafa al-Kadhimi aliagiza kusimamishwa kazi kwa vikosi vya usalama katika uwanja wa ndege kufuatia ajali hiyo iliyotokea Jumatatu.

Maafisa watachukuliwa hatua kwa kushindwa kuchukua hatua na kuruhusu vitendo vya ukosefu wa usalama kama hivyo, taarifa hiyo imesema.

Bwana Kadhimi ametoa wito wa juhudi za pamoja"kumaliza uhalifu wa aina hiyo dhidi ya raia" na kuahidi kutoruhusu "magenge hayo kuwa huru wakati yanatatiza usalama bila ya kuadhibiwa".

Kushindwa kwa Serikali ya Iraqi kusitisha mashambulizi ya roketi yanayorushwa kuelekezwa uwanja wa ndege na uwanja wa ubalozi wa Marekani huko Baghdad kumesababisha wasiwasi mkubwa.

Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo inasemekana kwamba alimuonya rais Barham Salih kwa njia ya simu kwamba ubalozi huo utafungwa ikiwa mashambulizi hayo yataendelea.

Wizara ya mambo ya nje ya ilisema Jumapili kwamba haitajibu mazungumzo ya siri ya Bwana Pompeo na viongozi wa nchi za nje.

Lakini ikasisitiza: "Makundi yanayoungwa mkono na Iran yanayorusha roketi kulenga ubalozi wetu ni hatari sio tu kwetu bali pia kwa serikali ya Iraq."

Kumetokea mashambulizi karibu 39 ya roketi na mabomu yanayolenga marekani nchini Iraq kati ya Oktoba na mwisho wa Julai, kulingana na shirika la habari la AFP.

Tangu mwezi Agosti, kumeshuhudiwa idadi ya mashambulizi sawa na hayo.

Mapema mwezi huu, Marekani ilitangaza kuwa itaondoa zaidi ya robo tatu ya jeshi lake nchini Iraq ndani ya wiki kadhaa.

Gen Kenneth McKenzie aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi litapunguzwa kutoka wanajeshi wapatao 5,200 mpaka 3,000 ndani ya mwezi huu wa Septemba.

Hao watakaosalia wataendelea kuwashauri na kusaidia vikosi vya usalama vya Iraq kukabiliana na kundi la wapiganaji wa kiislamu la 'Islamic State (IS)'.

Uwepo wa jeshi la Marekani limekuwa tatizo kubwa Iraq tangu Marekani ilipohusika kumuua kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran Qasem Soleimani katika mapigano ya anga mjini Baghdad mwezi Januari.

Bunge la Iraqi lilipitisha mswada wa kuondoa vikosi vya jeshi vya kigeni suala ambalo lilipelekea Rais Trump kutishia kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Iraq.