Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je Amy Coney Barrett ataidhinishwa kuwa Jaji wa mahama kuu?
Rais wa Marekani Donald Trump ameripotiwa kumchagua Amy Coney Barrett kuwa jaji mkuu, ambaye anapendwa na jamii ya conservative.
Maamuzi ya rais - yatatangazwa rasmi Jumamosi katika Ikulu ya White House.
Amy atachukua nafasi ya jaji Ruth Bader Ginsburg, ambaye alifariki Ijumaa ya wiki iliyopita.
Ingawa uteuzi huo unaweza kuzua upinzani mkali kutoka katika baraza la Seneti ili kumuidhinisha kuwa jaji mkuu kwa kuwa uchaguzi wa urais unakaribia kufanyika mwezi Novemba.
Chombo cha habari cha CBS - kimepata taarifa kutoka sehemu mbalimbali ambazo zina uelewa wa mchakato wa uchaguzi wa Jaji mkuu -ambapo imeripotiwa kuwa rais amemchagua Jaji Barrett.
Lakini rais alipoulizwa juu ya uchaguzi wake, Ijumaa jioni, bwana Trump alikataa kutoa maelezo yoyote: "Mtafahamu kesho. Angalia wote ni wana vigezo. Anaweza kuwa yeyote kati yao.
Kama Jaji Barrett ataidhinishwa, kura za conservative-zitakuwa 6-3 ambao watakuwa wengi katika siku za usoni.
Amy mwenye umri wa miaka 48-atakuwa jaji wa tatu kuchaguliwa na rais huyu wa Republican, Neil Gorsuch alichaguliwa mwaka 2017 na Brett Kavanaugh ilikuwa mwaka 2018.
Majaji tisa wa mahakama kuu uchaguliwa kutumikia mahakama katika maisha yao yote, na maamuzi yao yanaweza kutunga sera za kila kitu kuanzia kwenye umiliki wa bunduki mpaka kwenye haki ya kupiga kura kuridhia utoaji mimba na ufadhili wa kampeni baada ya rais aliyewateua kuondoka nadarakani.
Miaka ya hivi karibuni, mahakama iliruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwa majimbo yote 50, walimruhusu bwana Trump kuweka marufuku ya usafiri kwa mataifa ya kiislamu na kuchelewesha mpango wa kupunguza uzalishaji wa kaboni..
Ni nafasi Democrats
Uchambuzi
Amy Coney Barrett amekuwa katika orodha ya Donald Trump, ya watu ambao wanaweza kuajiriwa katika mahakama kuu kwa muda sasa.
Lakini suala ni je Amy anaweza kuwa mbadala sahihi wa Ruth Bader Ginsburg?
Wiki iliyopita, suala hilo lilikuwa halifikiriwi kwa namna hiyo.
Hata kabla ya Trump kuripotiwa kumchagua Jaji Barrett , conservatives walikuwa wakiwakusanya karibu wagombea wote , yeyote ambaye atakayepata alionekana kuwa sawa.
Na kama wangekuwa pamoja, kama walivyoonekana basi kulikuwa hakuna wasiwasi kuhusu uteuzi wake.
Uchaguzi wa Jaji Barrett unawaweka Democrats kuwa katika nafasi ngumu.
Wanahitaji kupata nafasi ya kumdhoofisha aliyeteuliwa bila kuonekana kuwa wanamshambulia kutokana na imani yake ya kikatoliki au historia yake binafsi-ili kuondoa hatari ya kupoteza wapiga kura mwezi Novemba.
Watachelewa kufanya harakati hizo kwa namna nzuri , ili kuendelea kulenga kwenye masuala ya afya na utoaji mimba, ili kuwepo katika mapambano ya kisheria ya Jaji Justice Barrett kwa upande wa conservative katika mahakama.
Wana matumaini kuwa Jaji Barrett, au Republicans, wanafanya makosa fulani yanayokithiri.
Vilevile ni mlolongo mrefu ambao wanapaswa kuufuata.
Amy Coney Barrett ni nani?
Amy anatambulika kuwa ni mkatoliki ambaye alisema maisha yanaanza katika mimba, kwa mujibu wa makala iliyoandikwa kwenye jarida la mwaka 2013.
Suala ambalo limemfanya apate ushabiki mkubwa kutoka kwa conservatives ambao wanafuatilia dini sana, na anawania kuondoa maamuzi ya mahakama kuu ya mwaka 1973 ya kuruhusu utoaji mimba katika nchi yote.
Amehusishwa haswa na makundi ya imani ya kikristo ,ambao wamekuwa wakimsifu katika vyombo vya habari.
Huku kundi moja la kutetea haki za binadamu linapinga uteuzi wa Jaji Barrett' kwa kuwa anaweza kuwa tishio kwa haki za wapenzi wa jinsia moja.
Licha ya Amy kuwa anasisitiza kila wakati kuwa kazi yake haihusiani na kazi yake.