Je inachukua idadi gani ya watu katika maandamano kumuondoa kiongozi wa kisiasa madarakani?

Waandamanaji wa hivi karibu nchini Mali
Iliyochapishwa

Je! Ni maandamano gani yenye ufanisi zaidi, vurugu au yasiyo ya vurugu? Na maandamano yanastahili kuwa makubwa kiasi gani kumuondoa madarakani kiongozi wa kisiasa? Matafiti mmoja ambaye amechunguza kwa makini maswali haya, anafikiria asilimia 3.5 ya watu huenda wakafaulu.

Harakati za pamoja huko Poland miaka ya 1980, ikiongozwa na vyama vya wafanyakazi; harakati ya muda mrefu ya kupambana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini; kung'olewa madarakani kwa rais wa Serbian Slobodan Milosevic; maandamano dhidi ya rais wa Tunisia, Zine al-Abidine Ben Ali, ambayo yalichangia msururu wa maandamano ya kuleta mageuzi katika ulimwengu wa kiarabu…

Hii yote ni mifano iliotumiwa na wanaharakati wa kupigania mageuzi ambayo yalileta mabadiliko ya kisiasa.

Maandamano ya hivi karibuni yale yanayoendelea Belarus - ambako maelfu ya watu wamemiminika barabarani kufuatia mzozo wa uchaguzi, ambao Rais Alexander Lukashenko anadai ushindi.

Mamlaka imetumia nguvu kuvunja maandamano hayo; baadhi ya waandamanaji wamekamatwa na visa kadhaa vya mateso vimeripotiwa katika vituo vinavyowazuilia.

Licha ya haya, maandamano hayo yamesalia kuwa ya amani katika maeneo mengi nchini humo.

Je huenda yakafaulu?

Njia moja ya kubaini hilo, ni kuangalia historia. Jambo ambalo mtaalamu wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Harvard Erica Chenoweth, amefanya.

Prof Chenoweth amejikita zaidi katika maandamano yanayofanyika katika nchi zilizo na tawala za kidikteta na wala sio demokrasia.

Chanzo cha picha, KRIS SNIBBE / HARVARD GAZETTE

Maelezo ya picha, Prof Chenoweth amejikita zaidi katika maandamano yanayofanyika katika nchi zilizo na tawala za kidikteta na wala sio demokrasia.

Prof Chenoweth amejikita zaidi katika maandamano yanayofanyika katika nchi zilizo na tawala za kidikteta na wala sio demokrasia.

Tofauti na viongozi wa kidemokrasia, madikteta hawawezi kuondolewa madarakani.

Katika tawala za kidemokrasia, ikiwa sera ya uongozi inapingwa na wengi, wanasiasa wanaweza kuchaguliwa wakiahidi kuifutilia mbali. Hakuna utaratibu kama huo katika uongozi wa kiimla.

Suala la ufafanuzi linajitokeza hapa. Ufafanuzi kuhusu maana ya demokrasia na udikteta unapingwa. Kuna wale wanasema mfumo wa kisiasa una wigo mpana - unaweza kuwa wa demokrasia au la.

Kuna pia suala la jinsi mtu anavyoainisha vurugu au bila vurugu.

Je shambulio dhidi ya mali linaweza kuitwa "vurugu"? Vipi na watu wanaolalamikia kushambuliwa kibaguzi bila kuwa na ushahidi wa kudhuriwa kimwili? Je visa vya kujitoa muhanga - kama kususia chakula? Pia ni vurugu?

Licha ya changamoto hizi za uainishaji, kuna aina zingine za maandamano ambazo ni wazi kuwa hazina vurugu na zingine ambazo zina vurugu. Mauaji bila shaka ni vurugu.

Maandamano ya amani, kuwasilisha maombi, kuinua mabango, mgomo na kususia huduma, kukaa ndani na matembezi, sio vurugu.. Kulingana na uainishaji mmoja unaojulikana, kuna aina 198 za maandamano yasiyo ya vurugu.

Na kulingana na uchambuzi wa maandamano yote ambayo data yake ilikusanywa kutoka 1900 hadi 2006, Erica Chenoweth na mtafiti mwenzake Maria Stephan walifikia hitimisho kwamba harakati hizo zilikuwa na uwezekano mara mbili wa kufanikiwa ikiwa maandamano hayakuwa ya vurugu.

Swali linalofuata ni - kwa nini?

Jibu linaonekana kuwa vurugu hupunguza msingi wa msaada wa harakati. Watu wengi zaidi watajiunga kikamilifu na maandamano yasiyo ya vurugu.

Hii ni kwa sababu inachukuwa muda mfupi kupanga maandamano kama hayo. Kutokana na sababu hizi, harakati zisizo na vurugu zina viwango vya juu vya ushiriki kutoka kwa wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu.

Maafisa wafyatua vitoza machozi katika makabiliano na polisi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maafisa wafyatua vitoza machozi katika makabiliano na polisi

Na kwanini jambo hili ni muhimu? Jibu lipo katika, mfano wa harakati za mapinduzi dhidi ya Slobodan Milosevic.

Askari walipohojiwa kwanini hawakuwapiga risasi waandamanaji, walisema ni kwa sababu wanawajua baadhi yao.

Walisita kupiga risasi kwenye umati uliokuwa na binamu zao, au marafiki, au majirani zao. Na bila shaka, kadiri maandamano yalivyokuwa makubwa ndivyo polisi na vikosi vya usalama watakavyo wajua washiriki

Erica Chenoweth amekuja na takwimu sahihi ya jinsi ukubwa wa maandamano unastahili kuwa ili harakati za mageuzi zifanikiwe.

Anasema washiriki wanatakiwa kuwa asilimia 3.5 ya idadi ya watu katika nchi husika.

Idadi hiyo huenda ikaonekana ndogo lakini ina ushawishi mkubwa. Kwa mfano, idadi ya watu nchini Belarus ni zaidi ya millioni tisa - Hii ina maanisha asilmia 3.5 ni zaidi ya watu 300,000.

Kanuni ya asilimia 3.5 haijatiliwa kikomo. Maandamano mengi yamefanikiwa japo viwango vya washiriki vilikuwa chini ya asilimia 3.5, japo moja au mbili ambayo yamefikia viwango hivyo pia hayakufaulu kwa kukosa uungwaji mkono - katika maandamano ya mwaka 2011 ya Bahrain, mfano kama huo ulijitokeza anasema Chenoweth.

Takwimu za utafiti wa awali wa Chenoweth zilikuwa za hadi 2006, lakini sasa amekamilisha utafiti mpya ambao unachunguza harakati za hivi karibuni za maandamano.

Na wakati matokeo yake ya hivi karibuni kwa ujumla yanaimarisha utafiti wa awali - yanaonyesha kwamba kutokuwa na vurugu ni bora zaidi kuliko vurugu - Pia amegundua mielekeo miwili.

Wa kwanza ni kwamba maandamano yasiyo ya vurugu yamekuwa njia maarurfu ya kutafuta mageuzi ikilinganishwa na harakati za watt kujihami au kusababisha vurugu.

Kati ya mwaka 2010 na 2019 kulishuhudiwa maandamano mengi ambayo hayakuwa ya vurugu duniani ikilinganishwa na muongo mwingine wowote katika historia.

Mwelekeo wa pili ni wa kushuka kwa viwango vya maandamano.

Ukiangalia kwa makini maandamano ya vurugu yapepungua kabisa - karibu tisa kati ya maandamano 10 saga zinafeli, Chenoweth anasema.

Lakini maandamano yasiyo ya vurugu pia yanafanikiwa mara chache kuliko ilivyokuwa. Kabla ya hapo, karibu kampeni moja kati ya mbili zisizo na vurugu zilifanikiwa - sasa ni karibu moja kati ya tatu

Kwanini? Kunaweza kuwa na maelezo mengi, lakini huenda ni kutokana na mabadiliko katika ulimwengu wa kidijitali ulioleta mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa miaka michache, inaonekana uwepo wa intaneti na kuibuka kwa mitandao ya kijamii kumewapatia waandaji wa maandamano zana mpya yenye nguvu zaidi na ambayo imewawezesha kuwasilisha ujumbe kwa urahisi- kwa mfano, ni lini na wapi watu watakutana kwa maandamano yajayo.

Lakini tawala za kimabavu sasa zimepata njia za kugeuza silaha hiyo na kuitumia dhidi ya wapinzani wao. ''Mipango ya kidijitali'' inaweza kuingiliwa na kuvurugwa, anasema Erica Chenoweth.

Serikali pia inaweza kutumia mitandao ya kijamii kueneza propaganda na taarifa ghushi.

Hali hii inashuhudiwa Belarus ambapo simu za waandamanaji waliowekwa kizuizini zinachunguzwa mara kwa mara, kubaini ikiwa zinafuatilia harakati za upinzani kupitia programu ya Telegram

Wakati watu wanaoendesha progamu hizi wakikamatwa, Telegram huzifunga akaunti zao ikiwa na matumaini kwamba polisi hawatatumia hiyo kama kugezo cha kuwachukulia hatua.

Je! Rais Alexander Lukashenko anaweza kusalia madarakanicling? Ataweza kweli kufanya hivyo wakati ambapo upinzani dhidi ya utawala wake umejitokeza wazi ? Pengine huenda isiwe hivyo. Lakini ikiwa historia ni mwongozo utakaozingatiwa - Ni magma sana kumwondoa