Uchunguzi wafanyika kubaini chanzo cha moto uliowaka katika Chuo Kikuu Makerere

Moto uliwaka kuanzia majira ya saa sita usiku mpaka asubuhi

Chanzo cha picha, Makerere university/Twitter

Maelezo ya picha, Moto uliwaka kuanzia majira ya saa sita usiku mpaka asubuhi
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Polisi nchini Uganda wanachunguza chanzo cha moto uliokiteketeza chuo kikuu maarufu, kikubwa na cha zamani zaidi nchini humo cha Makerere, kilichopo katikati mwa mji mkuu Kampala.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda moto huo ulianzia kwenye paa, na baadae kusambaa kwenye sakafu za majengo ya vitengo vya fedha na rekodi za chuo.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa maafisa walikabiliana na moto mkubwa kuanzia takriban saa sita usiku hadi asubuhi Jumapili.

Jengo kuu lilikuwa na chumba cha kuhifadhia nyaraka za rekodi na kumbukumbu za Chuo kikuu cha Makerere

Chanzo cha picha, @UNSEEN_ARCHIVE

Maelezo ya picha, Jengo kuu lilikuwa na chumba cha kuhifadhia nyaraka za rekodi na kumbukumbu za Chuo kikuu cha Makerere

Jengo hilo maarufu lililoungua mbalo linafahamika kama Ivory Tower, lenye kuta nyeupe na madirisha ya bluu, ni moja ya majengo yanayotambulisha Chuo hicho maarufu barani Afrika.

Picha katika baadhi ya mitandao ya kijamii ya Chuo hicho zinaonesha sehemu ya nje ya kuta nyeupe za chuo hizo zilizoungua na kugeuka kuwa rangi nyeusi, na baadhi ya madirisha yaliyoungua:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ivory Tower pia lina Ofisi ya Naibu Kansela wa chuo hicho pamoja na ukumbi mkuu wa chuo.

Naibu kansela Profesa Barnabas Nawangwe, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter , ameelezea tukio hilo kama asubuhi nyeusi sana na akaongeza kuwa uharibifu uliotokea ni wa kiwango cha kutoaminika:

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Unaweza pia kusoma:

Makerere ni mojawapo ya vyuo vikuu vya hali ya juu zaidi barani Afrika, na ndicho Chuo Kikuu cha zamani zaidi katika Afrika Masharariki, ambapo kilianzishwa mwaka 1922 mara ya kwanza kama shule ya ufundi.

Viongozi mbali mbali wa Afrika wamepata elimu ya juu katika Chuo cha Makerere akiwemo muasisi wa Taifa la Tanzania hayati mwalimu Julius kambarage Nyerere, Mwandishi maarufu wa vitabu wa Kenya Ngugi wa Thiong'o, wasomi na viongozi wa kidini kama vile Askofu Mkuu wa mstaafu Kiangilikana wa New York John Sentamu,