Kwanini mkataba wa makubaliano ya amani ya UAE na Bahrain ni muhimu

Iliyochapishwa

Rais wa Marekani Donald Trump, amepongeza "mwanzo mpya" wa Mashariki ya kati, wakati mkataba ya kihistoria wa Israel ukisainiwa na Umoja wa Falme za kiarabu(UAE) na Bahrain.

Bwana Trump amezungumza wakati mataifa mawili ya Ghuba yakisaini mkataba wa kuwa na uhusiano mzuri na Israel.

Mataifa hayo matatu yalisaini mkataba wa kihistoria ,wakati utawala wa bwana Trump ukiwa umesaidia kuwaunganisha.

Mataifa ya Ghuba yaliyosaidi ni ya tatu na ya nne kuitambua Israel tangu mwaka 1948.

Bwana Trump ana matumaini kuwa mataifa mengine yatafuata mfano huo, lakini Palestina imewasihi wasifanye hivyo kwa kuwa matatizo bado hayajatatuliwa.

Kwa miongo kadhaa, mataifa mengi ya Uarabuni yamekuwa yakiipinga kuwa na uhusiano na Israel, kwa kusisitiza kuwa watahusiana na taifa hilo iwapo tu litamaliza migogoro yake na Palestina.

"Baada ya miongo ya mgawanyiko na migogoro tumeanza mwanzo mpya na Mashariki ya Kati," Bwana Trump aliwaambia mamia ya wananchi waliokusanyika White House siku ya Jumanne.

"Tuko hapa mchana huu kufanya mabadiliko ya kihistoria," aliongeza.

Waziri mkuu wa Israeli bwana Benjamin Netanyahu amepokea makubaliano hayo na kusema , "Siku hii ni kitovu cha historia; imetuma ujumbe wa mwanzo wa amani."

Lakini kiongozi wa Palestina bwana Mahmoud Abbas alisema Israeli inaweza kuleta Amani kama tu ikiachia maeneo waliyoyachukua.

.

"Amani, ulinzi na usalama havitaweza kupatikana mpaka kazi wanayoifanya Israeli katika maeneo yao isitishwe, AFP imeripoti.

Jeshi la Israeli limesema roketi mbili zilitunguliwa katika ukanda wa Gaza wakati wa sherehe za kusainiwa kwa mkataba wa Israel zikiwa zinaendelea.

Kwanini makubaliano haya yanatambulika kuwa ya kihistoria?

Kabla ya UAE na Bahrain, mataifa mengine ya kiarabu pekee kutoka Mashariki ya Kati kuitambua rasmi Israel ni Misri na Jordan, Mataifa hayo yalisaini mkataba wa amani na taifa hilo mwaka 1978 na 1994.

Mauritania, ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kiarabu kaskazini magharibi mwa Afrika, ilianzisha mahusiano ya kiplomasia na Israel mwaka 1999 lakini walisitisha mahusiano hayo mwaka 2010

Macho yote sasa yapo kuangalia kama mataifa mengine yatafuata mkondo huo ingawa mpaka sasa Saudi Arabia inaonekana kuwa bado haipo tayari kusaini mkataba huo.

Makubaliano hayo yanaonekana kama yanaweza kuleta uhusiano mpya wa usalama na mataifa mengi ya Ghuba ya Uarabuni ambao hawana uhusiano mzuri na Iran.

Mafanikio yaliyopatikana

Uchambuzi

Makubaliano haya yanawakilisha mafanikio makubwa ya kidiplomasia katika utawala wa Trump.

Kufanikiwa kuzishawishi nchi hizo mbili kusaini mkataba na Israel - bila kujali suluhu ya swali la Palestinan - inaonyesha kuwa hatua nzuri ya kuleta umoja na mataifa ya kiarabu.

Maelezo ya mkataba huo bado hayajawekwa wazi kwa umma, lakini but kutakuwa na balozi, mikataba ya kibiashara na kufungua kwa uhusiano wa kusafiri kati ya mataifa hayo.

Bwana Trump alipendekeza mataifa matano mengine ya Uarabuni kukamilisha kusaini mkataba wa aina hiyohiyo.

Lakini makubaliano hayo yamepingwa na uongozi wa Palestina kutajwa kuwa 'siku nyeusi' kwa ukanda wao.

Maendeleo katika eneo la ukingo wa Magharibi na Gaza bado hayakubaliki katika mahusino haya ma,pya.

Kwanini Palestina haikubaliano na makubaliano hayo?

Palestina imesema kuwa makubaliano hayo ni usaliti wa hatari kubwa.

Wanaamini kuwa mataifa ya Ghuba wamekiuka makubaliano ya mataifa ya kiarabu ya kutohusiana na Israel mpaka taifa la Palestina likiwa limemaliza migogoro na taifa hilo.

Umoja wa falme za kiarabu, UAE imesema kuwa makubaliano yake na Israel yamejumuisha ahadi kutoka kwa Israel kusitisha mpango tata wa kumiliki eneo la ukingo wa magharibi, rais Trump aliainisha kuwa mpango wa Amani kufikia Januari utakuwa umejulikana.

Palestina ilikataa pendekezo la bwana Trump na kudai kuwa linaupendeleo kwa Israel na kutoa angalizo kuwa mpango huo utaondoa matumaini ya uhuru waliyokuwa nayo kwa siku zijazo .

Waziri wa mambo ya nje wa UAE ameileza BBC kuwa aliona fursa wakati bwana Netanyahu inaonyesha ishara kuwa ataachana na mpango wake huo mwanzoni mwa mwaka ujao.

"Kila mtu ana hofu kuhusu kuachiwa kwa ardhi ya Palestina, ambayo ni tishio la kufikia muafaka kwa mataifa hayo mawili," Anwar Gargash alisema.

"Na nadhani huu ni mpango ambao umeleta mpango wetu sababu kufikia maamuzi hayo sasa na sio mwaka 2021 au 2022.

Bwana Gargash alisema hakumwamini bwana Netanyahu au kiongozi mwingine wa Israeli kuwa wanaweza kuhaidi kuachana na mpango wake ukingo wa maghabi.

UAE imeutaka uongozi wa Palestina kutumia wakati huu kujipanga kushirikiana na Israel ili waweze kufanya mambo ya muhimu.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair anasema mkataba huo ni mkubwa na unakaribisha fursa za uhusiano wa kisiasa katika ukanda huo.

Alisema kuhusu suala la Palestina kupinga "itafikia wakati ambao Palestina wataelewa kuwa ni vyema kubadili mikakati yao ili eneo hilo la Palestina liweze kuachiwa ".

Historia?

Kuna uhasama wa kidiplomasia katika ukanda huo kati ya Saudi Arabia na Iran.

Migogoro iliyopo kati yao kwa miongo kadhaa ilianzia kwenye tofauti za kidini.

Wote ni waislamu lakini kuna pande kuu mbili za uislamu-Iran ina waislamu wa Shia wakati Saudi Arabia inaonekana kuwa inatawaliwa na utawala wa kiislamu wa Sunni.

UAE ni Bahrain, ni washirika wa Saudia.

Hatua itakayochukuliwa na Saudi Arabia inaangaliwa kwa ukaribu.Ingawa hakuna dalili za kuonyesha kuwa Saudia iko tayari kuifuata Bahrain na UAE.

Kabla ya kutangazwa kwa makubaliano ya UAE na Israel, mwezi Agosti-ambayo yanajumuisha kusitishwa kwa mpango ulio na utata kwa kulichukua eneo la ukingo wa magharibi-Israel haikuwa na uhusiano na mataifa ya Ghuba ya Uarabuni.

Mwezi uliopita, ndege ya kwanza ya Israel ilionekana ikiwa inatoka Israel kuelekea UAE, jambo ambalo lilonekana kwa hatua kubwa ya kuweka uhusiano mzuri.

Mkwe wa rais Trump Jared Kushner ambaye ndiye mshauri wake, alikuwa katika ndege hiyo , alielezea mkataba wa UAE kuwa na fursa ya kuleta mabadiliko ka Mashariki ya kati yote.