Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanaume auza zawadi ya pombe alizopewa kusherehekea siku yake kuzaliwa kununua nyumba
Mwanaume mmoja ambaye baba yake alimpa zawadi ya pombe kwa miaka 18 kila ilipotimia siku ya yake ya kuzaliwa anaziuza ili kununu nyumba.
Matthew Robson, kutoka Taunton, alizaliwa mwaka 1992 na katika maisha ya baba yake Pete ametumia takriban pauni 5,000 kununua chupa 28 za pombe moja aina ya Macallan
Hadi sasa chupa hizo zina thamani ya pauni 40,000 na sasa zinauzwa.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 "huenda haikuwa " zawadi nzuri kwa mvulana mdogo lakini kwa "maagizo ya kwamba asizifungue kamwe chupa hizo " zimekua sawa na mayai katika kiota cha ndege.
"Kila mwaka nilipokea chupa moja kama zawadi ya kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa ," Matthew alisema. "Nilidhani ni zawadi ndogo ya ajabu kwasababu nilikuwa mdogo sana kuanza kunywa.
"Lakini nilipewa masharti makali, nisiwahi hata siku moja kufungua na nilijaribu sana kujitahidi na nikafanikiwa na chupa zote bado zimefungwa.
Baba yake Pete, ambaye ni mkazi wa Milnathort in Scotland, alisema chupa ya kwanza ya whisky ya mwaka 1974 ilinunuliwa kwa ajili ya "kulewesha kichwa cha mtoto mchanga".
"Nilifikiri litakua ni jambo la kufurahisha kama ningenunua chupa moja kila mwaka ili awe na machupa 18 atakapotimiza umri wa miaka 18 whisky ," alisema.
"Haikuwa zawadi pekee aliotuletea. Ilikuwa tu ni zawadi ya kipekee, lakini ilikuwa ni bahati kidogo kwamba iliendelea ."
Tangu wakati huo, wataalamu wanasema pombe hizo aina ya Macallan zimekusanywa na Matthew anatumaini kuziuza kwa pauni 40,000 na kutumia pesa hizo kununulia nyumba.
Inauzwa na mlanguzi wa whisky Mark Littler, ambaye alizielezea kama described it "pombe zinazofaa".
"Thamani ya pombe ya Macallan imepanda sana katika kipindi cha miaka 5 hadi 10 ." Kuwa na kiwango cha aina hiyo cha chupa zake zitauzwa sana ."
Alisema kuwa "idadi kubwa ya watu ambao wameelezea utashi " wa kuzinunua, hasa kutoka kwa wanunuzi mjini New York na bara la Asia.