Australia: Nyoka waingia ndani ya nyumba ya mwanaume kupitia kwenye dari

A snake crawls outside the house

Chanzo cha picha, North Brisbane Snake Catchers and Relocation

Maelezo ya picha, Nyoka walipatikana ndani ya nyumba
Iliyochapishwa

Mwanaume mmoja nchini Australia alipatwa na mshituko wakati aliporudi nyumbani na kuwapata nyoka wawili walikua wamepita kwenye dari lake la nyumba na kuingia ndani ya nyumba yake katika mji wa Queensland .

David Tate alimpata nyoka mmoja katika chumba chake cha kulala na wa pili sebuleni siku ya Jumatatu. Nyoka hao walikua na uzito wa kilo 22.

Mkamataji wa nyoka Steven Brown alisema kuwa walikua na "ukubwa wa kipekee".

Inadhaniwa kuwa nyoka hao wawili dume huenda walikuwa wakimpigania nyoka wa jike ambaye bado hajapatikana.

Upana wa chatu hao ulikua ni wa mita 2.8 (futi 9.1 ) na walikuwa na urefu wa mita 2.5

A chunk of ceiling that has fallen onto the kitchen

Chanzo cha picha, North Brisbane Snake Catchers and Relocation

Maelezo ya picha, Wanyama hao walikua wameanguka kutoka darini

Bwana Tait alisema kuwa awali aliwaona nyoka wakiota jua juu kwenye paa la nyumba yake.

"Niliporudi nyumbani ...niliona kipande kikubwa cha dari kilichoangushwa kwenye meza ya jikoni ,"aliliambia gazeti la The Courier-Mail.

Baada ya kuona hali ya dari, alitazama huku na kule na hatimae akawapata wanyama hao.

Aliamua kumuita mkamataji wa nyoka na mambo yakaishia hapo "haraka sana".

"Sikutaka kabisa kuwashika mwenyewe," alisema.

A snake under a cupboard

Chanzo cha picha, North Brisbane Snake Catchers and relocation

Maelezo ya picha, Mmoja wa nyoka alikuwa sebuleni na mwingine alipatikana katika chumba cha kulala

Bwana Brown kutoka taasisi inayowakamata nyoka na kuwarudisha kwenye makao yake ya Brisbane, North Brisbane Snake Catchers and Relocation aliiambia BBC: "Hawa ni nyoka wenye ukubwa usio wa kawaida ukiwalinganisha na ukubwa wa nyoka wengine ambao tunawapata kwa kawaida ."

Ni mpaka alipofika nyumbani ndipo alipobaini kuwa wanyama hao walikua wamevunja dari na kuinga ndani ya nyumba, alisema kwenye ujumbe wake wa Facebook.

"Tunaingia katika msimu wetu wa nyoka kwani leo ni mwanzo wa msimu wa kuzaliana na nyoka watakuwa na joto la uzazi kadri joto litakavyokua linaongezeka katika msimu wetu wa majira ya joto ," aliiambia BBC.

Bwana Brown alisema kuwa watu wanaokutana na nyoka, ni muhimu kusimama wima na kuiacha nyoka ipite kwani hawatakuona wewe kama tisho kwao.

"Kile nyoka wote wanachokuwa wanakitaka ni kukwepa tisho lolote la hatari ," aliongeza.