Shinzo Abe: Waziri mkuu wa Japan ajiuzulu kutokana na sababu za kiafya

Iliyochapishwa

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametangaza kwamba amejiuzulu kutokana na sababu za kiafya.

Amesema kwamba hataki maradhi alionayo kuingilia kazi yake , na kuomba msamaha kwa raia wa Japan kwa kushindwa kukamilisha muda wake.

Ameugua kwa miaka mingi kutokana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini hali yake imekuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni.

Mwaka uliopita , alikuwa waziri mkuu wa Japan aliyehudumu kwa kipindi kirefu nchini Japan.

Kipindi chake cha kuhudumu kilianza miaka 2012.

Mwaka 2007 , alijiuzulu ghafla alipokuwa waziri mkuu kutokana na mapambano yake ya ugonjwa huo wa tumbo , ugonjwa hatari ambao ameishi nao tangu alipokuwa kijana.

Ameimarisha sekta ya ulinzi nchini Japan na kuongeza matumizi ya kijeshi , lakini ameshindwa kubadilisha kifungu cha sheria kinachoruuhusu jeshi kulinda taifa hilo pekee.

Je Abe alisema nini?

Waziri huyo alisema kwamba afya yake ilianza kuzorota baada ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo anaougua kumrudia tena katikati ya mwezi Julai.

''Alikuwa akipokea matibabu ya ugonjwa huo ambayo ilikuwa lazima kufanyiwa mara kwa mara na hivyobasi hangepata muda wa kutosha kufanya majukumu yake ya uwaziri mkuu'', aliongezea.

Alisema kwamba hangependa kufanya makosa hususan kuhusu maamuzi muhimu na hivyobasi akaamua kujiuzulu.

''Nilifanya uamuzi kwamba sitaendelea na kazi yangu kama waziri mkuu'', alisema.

''Ningependa kuomba msamaha kwa raia wa Japan kwa kuuwacha wadhfa wangu huku ikiwa nimesalia na mwaka mmoja afisini wakati ambapo kuna mlipuko wa virusi vya corona huku baadhi ya sera zikiwa katika harakati za kuidhinishwa''

Kwa nini kuna wasiwasi?

Ziara za mara mbili katika kipindi cha wiki moja hospitalini zilizua masuali kuhusu iwapo afya ya bwana Abe ilikuwa inazorota.

Alitarajiwa kuhudumu hadi Septemba 2021.

Maafisa wa LDP walikuwa wamefutilia mbali uvumi kwamba hatojiuzulu, akisema kwamba afya ya waziri mkuu ilikuwa sawa.

Siku ya Jumanne mmoja ya washauri wake waliambia Reuters kwamba alidhania kwamba bwana Abe atakamilisha kipindi chake .

Udhabiti na kashfa

Waziri mkuu Abe ameugua kwa muda mrefu ugonjwa wa vidonda vya utumbo.

Ugonjwa huo ulimlazimu kujiuzulu 2007 -mara ya kwanza alipoongoza serikali.

Sasa baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu yeye kukosekana kazini mbali na katika maeneo ya umma licha ya tataizo la vurusi vya corona nchini Japan inaonekana anajiuzulu kwa mara nynegine kutokana na ugonjwa huohuo.

Huku akiwa waziri mkuu aliehudumu kwa kipindi kirefu zaidi, anawacha umaarufu wa kulifanya taifa la Japan kuwa thabiti na serikali yenye uwezo mkubwa ambayo iliruhusu sera ya kuimarisha uchumi.

Pia aliimarisha uhusiano na Marekani kwa kufanya urafiki na rais Trump mara kwa mara katika uwanja wa gofu.

Ijapokuwa serikali ilikumbwa na kashfa, ikiwemo suala la upendeleo mbali na kuharibu makusudi rekodi za umma.

Wakati mlipuko wa corona ulipokumba taifa hilo , jibu lake alilaumiwa mara kwa mara kwa kuchelewa kuchukua hatua madhubuti na mtu ambaye hakuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Ni nini kitafanyika?

Bwana Abe alisema kwamba ataendelea kuhudumu hadi mrithi wake atakapopatikana.

Tangazo lake litasababisha kupigwa kwa kura ndani ya chama cha LDP ili kutafuta mrithi wake.

Chama kitaamua Jumanne ijayo jinsi ya kufanya uchaguzi , kulingana na ripoti za chombo cha habari cha Kyodo.

Uchgauzi huo utafuatiwa na ule wa ubunge ili kumchagua waziri mkuu.

Mshindi atahudumu katika wadhfa huo hadi mwisho wa muhula wa bwana Abe.