Virusi vya corona: Yafahamu mataifa 10 ambayo hayajathibitisha mgonjwa yeyote wa corona

Iliyochapishwa

Covid-19 imeathiri karibia kila taifa duniani isipokuwa mataifa 10 .

Hivyobasi tunauliza yanafanya nini mataifa hayo?

Hoteli ya Palau ni maarufu kwasababu ilipofunguliwa 1982 ilikuwa hoteli ya pekee kwani hakukuwepo na hoteli nyengine.

Tangu wakati huo taifa hilo dogo , linalozungukwa na bahari ya pacific limejipatia watalii wengi. Mwaka 2019 , watalii 90,000 walitembelea Palau , ikiwa ni idadi mara tano ya jumla ya idadi iliopo.

Mwaka 2017, takwimu za IMF zilionesha kwamba utalii ulichangia asilimia 40 ya kipato cha nchi hiyo cha kila mwaka. Lakini hilo ni kabla ya mlipuko wa virusi vya corona kuanza.

Mipaka ya Palau ilifungwa tangu mwisho wa mwezi Machi.

Ni miongoni mwa mataifa 10 duniani ambayo hayakuthibitsha mgonjwa yeyote wa Covid 19 bila kuorodhesha Korea kaskazini na Turkmenistan lakini bila kuambukiza mtu yeyote virusi hivyo vimeliathiri pakubwa taifa hilo.

Hoteli hiyo ya Palau imefungwa tangu mwezi Machi na haipo pekee.

Mikahawa haina watu, maduka yamefungwa na wageni wa pekee ni raia waliojiweka katika karantini.

Mataifa ambayo hayajathibitisha hata mgonjwa mmoja wa corona.

  • Palau
  • Micronesia
  • Marshall Islands
  • Nauru
  • Kiribati
  • Solomon Islands
  • Tuvalu
  • Samoa
  • Vanuatu
  • Tonga

Bahari hapa ni nzuri na yenye mandhari ya kuvutia zaidi ya eneo lolote lile jingine duniani, kulingana na Brian Lee, meneja na mmiliki mwenza wa hoteli ya Palau.

Ni bahari ya rangi ya buluu ambayo ilimfanya Brian kuwa na kazi ya kufanya.

Kabla ya Covid 19 vyumba vyake 54 vilikuwa na kati ya asilimi 70 na 80 ya wageni , lakini mipaka ilipofungwa , hakukuwa na chengine cha kufanya.

''Ni taifa dogo , hivyobasi wakaazi hawawezi kuishi Palau'', anasema Brian.

Ana takriban wafanyakazi 20 na amefanikiwa kutowafuta kazi huku wakifanya kazi kwa saa chache .

''Najaribu kuwatafutia kazi ,kupitia kufanya ukarabati na kadhalika'', anasema. Lakini hoteli zisizo na wateja haziwezi kukarabatiwa kila siku .

Nitaendelea kutoa huduma kwa nusu mwaka mwengine halafu nifunge , anasema Brian.

Briana hailaumu serikali , ambayo imetoa usaidizi wa kifedha kwa raia wake mbali na kufanikiwa kuzuia kuingia kwa virusi hivyo.

''Nadhani walifanya kazi nzuri'', anasema, ''iwapo hoteli ya kwanza ya Palau itaendelea kuhudumu kitu kinafaa kubadilika.

Rais hivi majuzi alitangaza kwamba safari za ndege muhimu huenda zikarudi kufikia tarehe mosi Septemba

Lakini huku wakifunga mipaka , hatua hiyo imeyafanya mataifa yasio na maambukizi ya Covid kuwa masikini zaidi na sio kila mtu anataka yafunguliwe.

Dkt. Len Tarivonda ni mkurugenzi wa afya katika eneo la Vanuatu , ambapo idadi yake ya watu ni 300,000.

Ijapokuwa hufanya kazi katika mji mkuu wa bandari ya Vila, anatoka maeneo ya Ambae , kisiwa chenye takriban watu 10,000 yapata maili 170 kaskazini.

''Unapozungumza nao , wengi wao wansema wanataka mipakaiendelee kufungwa kwa muda mrefu zaidi'', anasema. Wanasema hawataki ugonjwa la sivyo tutaangamia kabisa.

Asilimia 80 ya watu wa Vanuatu wanaishi nje ya miji na uchumi rasmi, alisema Dkt Tarivonda. Na maoni yangu ni kwamba bado hawajaanza kuathiriwa.

Ni wakulima wanaopanda chakula chao wenyewe - wanategemea uchumi wa mashambani.

Hatahivyo, taifa hilo litaathirika .

Benki ya bara Asia inatarajia kipato cha taifa kitashuka kwa asilimia 10 ikiwa ndio kiwango kikubwa tangu taifa hilo lijipatia uhuru 1980.

Kuanguka kwa uchumi hakusababishwi na kufungwa kwa mipaka kwasababu ya corona.

Mwezi Aprili, kimbunga kwa jina Harold kilipiga eneo kubwa la taifa hilo, na kuwaua watu watatu na kuwaathiri zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini humo