Mali: Kwa nini mapinduzi yanashangiliwa nyumbani, majirani wakilalamika

People on motorbikes in Bamako celebrating the military takeover in Mali - 19 August 2020

Chanzo cha picha, EPA

Iliyochapishwa

Makundi ya watu yaliwashangilia makanali walipindua serikali ya Mali, nchi ambayo inapakana na jangwa la Sahara, ambako vikosi vya usalama - ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa Ufaransa na walinda usalama wa Umoja wa Mataifa - wanapigana na makundi ya kijihadi, lakini sio kila mtu amefufurahia hatua hiyo, anasema Mchambuzi wa Afrika Magharibi Paul Melly.

Mashauriano yanadaiwa kuendelea ya kutafuta jinsi ya kumpeleka mafichoni Ibrahim Boubacar Keïta, rais wa Mali aliyetolewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi siku ya Jumanne na ambaye anazuiliwa pamoja mwanawe wa kiume na Waziri Mkuu wake Boubou Cissé lakini pia na viongozi wengine wakuu serikali.

Lakini sasa Ecowas, muungano wa kiuchumi wa mataifa ya Afrika Magharibi ambayo Mali ni mwanachama, umeelezea kughadhabiishwa kwake na hatua hiyo huku marais wa muungano huo wakitoa witoBw. Keita kurudishwa madarakani.

Ibrahim Boubacar Keïta alishinda muhula wa pili mwaka 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ibrahim Boubacar Keïta alishinda muhula wa pili mwaka 2018

Sauti iliyojaa hofu ya Bw. Keita aliye na miaka 75 akitangaza kujiuzulu kwake katika televisheni karibu saa sita usiku suku ya Jumanne, katika chumba kinachodhaniwa kuwa kambi ya kijeshi ya Kati, iliyopo kilo mita 15 swa na (maili tisa) kutoka mjini Bamako, ambako yeye na Bw. Cissé walipelekwa na maafisa hao nyakati za mchana.

Hutua hiyoilijiri baada ya miezi miwili ya maandamano ya ya kupinga kati ya serikali yake yaliyoitishwa na wanasiasa wa upinzani wakishirikiana na wanaharakati wa kijamii, ambayo yalivutia umati mkubwa wa watu waliotiwa hamasa na imamu maarufu Mahmoud Dicko.

Imam Mahmoud Dicko akiwahutubia watu mjini Bamako, Mali - Juni 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Imam Mahmoud Dicko amesema hana haja na uongozi wa kisiasa

Waandamanaji walikuwa wanataka kitu kimoja tu - Kujiuzulu kwa Bw. Keïta, japo Imam Dicko hakujitokeza wazi kushinikiza hilo.

Katiika mashauriano yaliyosimamiwa na Ecowas, Bw. Keïta alitoa ahadi moja baada ya nyingine, lakini hakuitikia wito wa kumtaka ajiuzulu bali aliendelea kufanya marekebisho tata ya kisheria abayo hatimaye yalimfanya apoteze uungwaji mkono na hata wandani wake jeshini.

2px presentational grey line

Pia unaweza kusoma:

2px presentational grey line

Hiyo haikutosha hadi pale kundi la viongozi wa kuu jeshini - kuchukuwa hatua ya kumuondoa madarakani

Lakini Ecowas haiko tayari kuendelea mbele na mageuzi ya madaraka yanayokiuka sheria na wajumbe wake, huku rais wazamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, akitarakiwa kurejea Bamako kwa mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa nchini humo.

Mashauriano makali yanatarajiwa kufanyika na hakuna anayejua jinsi yatakavyokuwa

Kupoteza nafasi

Milio ya risasi iliposikika katika kambi ya jeshi ya Kati siku ya Jumanne haikuwa wazi moja kwa moja tataizo nini kando na dhana kwamba pengine ni vurugu za wanajeshi wa kawaida waliokuwa wakilalamikia kiwango cha juu cha ufisadi wakati wanahataridha maisha yao kupigana na makundi ya kijihadi kaskazini mwa nchi.

Magari yakiwasafrisha wanajeshi wa Ufaransa na Mali kaskazini mwa eneo la Timbuktu - 2015

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, MB. Keïta alishindwa kutumia nafasi ya mapema kushughulikia ghasia kaskazini mwa Mali ambako wanajeshi kadhaa wameuawa

Ipi hatima ya baadaye ya Mali?

Katika kipindi cha muda mfupi walinda usalama wa Umoja wa Mataifa, vikosi vya Ufaransa vya kupambana na ugaidi na majeshi ya mali yaliyopelekwa kaskazini mwa nchi yanatakiwa kudumisha usalama wa nchi.

Lakini hali kwa sasa ni tete na suala la kukabiliana na makundi ya kijihadi huenda likachangia mashauriano ya muda mrefu kabla ya kubuniwa kwa serikali ya mpito, itakayokubaliwa kimataifa kabla ya uchaguzi mpya.

Mtu pekee ambaye amesema wazi hatachukua mstari wa mbele katika siasa za nchi hiyo ni Bw. Dicko.

Imamu huyo maarufu ametangaza kwamba anajiondoa katika siasa kwa sasa, japo atasalia kuwa kiungo muhimu, endapo ataamua kutumia ushawishi wake kama kiongozi wa kidini .

Kwasasa, hatima ya Mali inategemea mazungumzo yanayotarajiwa kati ya majeshi, vingozi wa vyama vya upinzani vya M5-RFP na Ecowas.