Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Robert Trump: Kaka mdogo wa Rais Donald Trump afariki dunia hospitalini
Rais Donald Trump ametoa rambirambi kwa "rafiki yake mkuu" na kaka yake mdojgo kufuatika kifo chake akiwa na umri wa miaka 71
" Ni kwa moyo mzito ninawashirikisha taarifa kwamba kaka yangu mwema Robert , amefariki kwa amani leo usiku," alisema katika taarifa yake Jumamosi.
Rais alikuwa amemtembelea kaka yake hospitalini mjini New York siku moja kabla ya kifo chake, akawaambia waandishi wa habari kuwa : " Anawakati mgumu."
Haijajulikana wazi ni nini kilichosababisha kifo cha Robert Trump.
Taarifa za vyombo kadhaa vya habari zinasema kuwa amekuwa akiugua sana.
"Hakuwa kaka yangu tu , alikua rafiki yangu mkuu ," Donald Trump alisema katika taarifa yake ya Jumamosi kuhusu kifo hicho "Kumbukumbu yake itaishi moyoni mwangu daima ."
Mtoto wa kiume wa Rais Trump Ericalimuelezea baba yake mdogo kama "mwanaume mwema-thabiti na aliyekuwa na maadili ".
" Familia yetu mzima itamkosa sana ," aliandika kwenye Twitter.
Robert alikuwa ndiye mtoto mdogo wa Fredna Mary Anne Trump kati ya watoto wa tano, na alizaliwa miaka miwili baada ya kaka yake Donald Trump.
Kaka yao mkubwa , Fred Jr, alifariki dunia mwaka 1981.
Robert Trump alitumia muda wake wa kazi katika kampuni ya nyumba ya familia, akawa Mkurugenzi mkuu .
Katika kitabu chake cha mwaka 1987 The Art of the Deal, ( au Sanaa ya mkataba) Donald Trump aliandika kwamba "Robert anaelewana na karibu kila mmoja, jambo ambalo ni zuri kwangu kwasababu wakati mwingine inanibidi niwe mtu mbaya ".
Katika mahojiano ya mwaka 2016 na gazeti la New York Post a kabla ya uchaguzi wa urais, kaka mdogo wa Trump alisema "Ninamuunga mkono Donald asilimia mia moja".
Hivi karibuni alikwenda mahakamani kwa azma iliyofeli ya kutaka kusitishwa uchapishaji wa kitabu cha mpwa wake Mary Trump ambacho kinaelezea yote kumuhusu Rais kinachoitwa - How My Family Created the World's Most Dangerous Man
Alimtaliki mke wake wa kwanza Blaine zaidi ya muongo mmoja uliopita na kumuoa Ann Marie Pallan mwezi Machi mwaka huu.
Kwamujibu wa gazeti la the Post, Robert alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Mount Sinai Hospital iliyopo Manhattan kwa zaidi ya wiki moja mwezi Juni.
Likimnukuu rafiki wa familia gazeti la New York Times lilisema kuwa alikuwa alipata tatizo la kuvuja damu kutoka kwenye ubongo ambalo lilianza baada ya kuanguka hivi karibuni.