Ni akinanani ambao wamekua viongozi bora katika historia ya dunia?

Ni ipi kati ya orodha ndefu ya viongozi wa dunian inaweza kutangazwa kuwa ni viongozi bora kuliko wengine? Ni vigezo gani vinaweza kuwa muhimu katika kuwachagua?
Kuna nyakati ambapo viongozi huonekana kuwa wanafanya vyema kwasababu ambazo wengine hawaziona kama ni za maana. Elizabeth Bowes-Lyon, mama yake Malkia Elizabeth wa Uingereza wa sasa , kwa mfano aliwapa matumaini na kulitia moyo sana taifa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia kiasi kwamba Adolf Hitler alimuelezea kama ''mwanamke hatari sana barani Ulaya . "
Tabia kama vile kukataa kwake kutoroka na watoto wake wa kike , kama watu wengine wa familia za kifalme za Ulaya walivyofanya licha ya ukweli kwamba mabomu ya Ujerumani yalikua yakianguka kama mvua jijini London ni jambo lililomfanya awavutie na kuwa mfano kwa wake.

Kwa hiyo kama tunaangalia aliyekua kiongozi botra zaidi tunapashwa kuangalia nini ? Aliye mfano wa kuigwa au jasiri? Mwenye ufanisi au mvumilivu? Tuangalie yote vigezo vyote tulivyotaja na zaidi ya hivyo ?
Kiongozi bora ni nani?
Ukweli ni kwamba ni swali ambalo ni vigumu kulijibu , kwani huenda kila mtu akawa na jibu lake…labda uulizwe kama ''mtu anayetoa maoni yake binafsi ".
Lakini kujiuliza kama swali na kujaribu kulijibu ni jambo gumu.
Hicho ndicho jarida la BBC la masuala ya Historia- BBC HistoryExtra lilichokifanya mwaka jana.
Kwanza , waliuliza wanahistoria 20 maariufu kuwateua wale wanaowaona kama watu waliokuwa viongozi bora zaidi , mtu aliyepata mamalaka na kuleta mafanikio kwa binadamu, na ambaye alihfanikiwa katika majukumu yake na ambaye anaweza kuwa mfano wa kuigwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Orodha hiyo haikumjumuisha Mama yake Malkia Elizabeth wa England ambaye alimuudhi sana Hitler, lakini iliwajumuisha wanawake wengine saba .
Je wewe ungemjumuisha nani?
Unaweza kutuambia katika mitandao yetu ya kijamii .
Hata hivyo katika orodha hiyo alikuwemo Kiongozi wa ufalme wa Wu Zetian (690-705) -kwasababu "alikuwa ni mwanamke mwenye mamlaka zaidi katika historia ya China" - Hadi karne ya 16 pamoja na mtawala Oda Nobunaga -kwasababu aliweza " kuiunganisha Japan " -, pia walimtaja Amenophis III (c 1390-1352 BC) - kwasababu "alikuwa ni faraha mkubwa wa Misri wakati Misri ilipoitawala dunia ya kale " - wale waliochaguliwa na wanahistoria walikuwa wengi wao ni waliokua viongozi barani Ulaya.
Na baada ya kuangalia vigezo vya uteuzi wao, wasomaji wa jarida la BBC HistoryExtra waliwapigia kura wanaowapenda.
Na mshindi alikuwa ni...
Katika nafasi ya 5 akiwa na 4% ya kura alikuwa ni : Malkia Elizabeth wa 1 wa England , ambaye aliteuliwa kwasababu katika karne ya 16 "alirejesha amani na kujenga taifa baada ya ghasia."
Katika nafasi ya 4, Aliteuliwa rais wa zamani wa Marekani Abraham Lincoln , kwasababu " aliwatete wafanyakazi na kuanzisha mchakato wa kusitisha utumwa ."
Katika nafasi ya 3 aliyepata 7% ya kura alikuwa ni Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill ,kwasababu "alikataa kukujbali kukubali madai ya Hitler ".
Katika nafasi ya pili akiwa na 25% ya kura alikuwa ni , Amílcar Cabral , ambaye aliwaunganisha raia zaidi ya milioni wa Guinea kupata uhuru baada ya uvamizi wa ukoloni wa Mreno , na matokeo yake nchi nyingine za Afrika zilizokuwa makoloni zikawa na mwako wa kudai uhuru wao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Maharaja Ranjit Singh , kiongozi aliyeiongoza Ufalme wa Sikh katika miaka ya mwanzoni ya karne ya 19, ndiye aliyeongoza akiwa na 38% ya kura na hivyo kuwa ndiye kiongozi bora aliyewahi kuwepo katika historia ya dunia.
Maharaja Ranjit Singhni nani ?
Maharaja Ranjit Singh alikuwa ameteuliwa awali na Matthew Lockwood , mwanhistoria katika Chuo Kikuu cha Alabama, ambaye kwa kifupi alikuwa amempendekeza kwasababu , " alibuni Ufalme wa uvumilivu ."

Chanzo cha picha, Getty Images
"Katika kipindi kikubwa cha karne ya 18 , India ilikua imegawanyika na lilikua ni taihfa lililoharibiwa na vita. Ufalme ambayo wakati mmoja ulikua umetawala kwa mamlaka makubwa ulifika wakati ukasambaratika na kuanguka, India ikawa na ombwe la utawala.
Punjab ilikua na matatizo makubwa pia. Wakati Ranjit Singh alipozaliwa mwaka 1780, Afghanstan iliivamia Punjab na kufanya mashambulio ya mara kwa mara katika majimbo ya Punjab, na kupanuka kwa himaya ya Uingereza ndani yake kuliliacha jimbo hilo katika matatizo zaidi ya kisiasa, uchumi dhaifu na mgawanyiko mkubwa kidini .
Yote haya yalibadilika kutokana na kupanda kwa Singh, 'Simba wa Punjab' .
Katika muongo wa kwanza wa karne ya 19, iufalme wake ulikua tayari umefanya jeshi la Sikh Khalsa army kuwa la kisasa, akijumuisha uvumbuzi wa kimagharibi bila kuacha miundo ya nyumbani na taasisi, akawaunganisha waasi, akaimarisha usalama katika mpaka na Afghanstan na kufikia mapatano ya maelewano na kampuni ya Uingereza iliyojulikana kama East Indies.
Singh, hata hivyo alikua zaidi ya mshindi
Ingawa India ilikua imegawanywa na watawala , dini na vita, Singh alikuwa muunganishi, nguvu ya uthabiti, mafanikio na uvumilivu.
Ufalme wake ulileta kipindi cha mabadiliko ambayo yanakumbukwa hadi leo katika jimbo la Punjab na Kaskazini -magharibi mwa India.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa alikuwa ni Sikh aliyejitolea ambaye alianzisha kampeni za kurejesha minara mikubwa ya dini yake, ikiwa ni pamoja na mnara wa Harmandir Sahib au Hekalu la Dhahabu lililopo katika Amritsar, pia alifanya kila aliwezalo kuhahakikisha kunakuwepo na uhuru wa kuabudu katika ardhi yote ya utawala wake.
Aliyapa misaada mahekalu ya Hindu na Sufi , na kushiriki ibada na sherehe za Wahindu na Waislamu, akawauoa wanawake wa Kihindu na wa Kiislamu na hata akazuwia kuchoma ng'ombe ili kulinda imani ya Wahindu.
Waislamu, Wahindu, Wasikhs, na Watu kutoka Ulaya waliajiriwa katika jeshi lake na katika kazi za utawala katika ufalme wake.
Chini ya utawala wake, miundo mbinu iliboreka, biashara zikafunguliwa na kupanuka na usanii ukashamiri.
Uongozi wake mzuri haukuendelea
Baada ya kifo chake mwaka 1839, ufalme wa Ranjit Singh wa kuvumiliana ulisambaratika. Waingereza walivamia, utawala wa Sikh ukaporomoka na hali mbaya ya usalama ikarejea tena katika kanda hiyo.
Ingawa alikuwa alikuwa ni beberu , Ranjit Singh alikuwa ni mtu aliyekuwa na utawala wa kujumuisha watu wa tabaka mbali mbali kwa minajili ya kujenga taifa, na alikua alifungua njia iliyohitajika sana wakati huo ya kuleta umoja na kuvumiliana miongoni mwa wahindi na wageni.
Bado tunaweza kunufaika na mifano yao leo . "












