Virusi vya corona: Mwanamke wa kwanza kufanyiwa upandikazaji wa mapafu mara mbili kwa corona

Iliyochapishwa

Mayra Ramírez aliamka kutoka kwa usingizi mzito katikati ya Juni baada ya kudungwa sindano ya kulala akiwa kwenye mashine ya kupumua kwa zaidi ya siku 40, lakini wakati huo hakuelewa kilichokuwa kimetokea.

Alikuwa amelala katika hospitali moja ya Chicago nchini Marekani, akiwa ameunganishwa kwa nyaya kumi na kitu - vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vile vya kufuatilia hali yake, tukio sawa na lile ambalo analikumbuka vyema alipokuwa amelazwa baada ya kubainika na dalili za ugonjwa wa corona mwisho wa Aprili.

Lakini makovu aliyoyaona mwilini mwake yalionesha kwamba kuna kitu kimetokea.

Baada ya kudungwa sindano ya kulala, muda si muda alipoteza fahamu na kuanza kuota ndoto za kumsumbua.

"Hadi nilipoamka ndipo nilipobaini kwamba nilifanyiwa upandikizaji wa mapafu Juni 5 na kwamba hayo yalikuwa matibabu ya kwanza kufaanyika nchini Marekani kwa mgonjwa wa virusi vya corona," amesema katika mahojiano na BBC.

Daktari wa Ramírez's anasema mwanamke huyo, 28, ambaye hakuwa na ugonjwa wowote unaojulikana hali yake ya afya iliendelea kuzorota hata zaidi, na afya yake kuendelea kuwa mbaya tangu alipolazwa hospitali.

Mwanamke huyo kijana, alikuwa amewasili hospitalini akiwa na matatizo ya kupumua lakini wiki kadhaa baadae mapafu yake yalikuwa kama jibini.

Mwanzoni mwa Juni, hospitali ilizungumza na familia ya mgonjwa huyo ili wamuage mpendwa wao kwa madai kwamba hana siku zaidi ya mbili za kuendelea kuwa hai duniani.

Lakini dakika za mwisho, madaktari waliamua kujaribu matibabu ambayo bado hayawahi kufanya kabla nchini Marekani kwa mgonjwa wa virusi vya corona.

"Mayra, kabla ya kuugua, alikuwa kijana mwenye afya, kwahiyo kama tulifanikiwa kutatuwa tatizo lake la mapafu awali, kila kitu kinastahili kuwa sawa," Daktari wa upasuaji Ankit Bharat, mmoja wa waliomfanyia upandikizaji amezungumza na BBC.

Siku mbili baadae wakaanza kumfanyia matibabu bila kuwa na matumaini yoyote - au uhakikika - wa matokeo yake.

Kipindi kigumu sana maishani

Marya amekuwa akihakikisha anakuwa na afya njema kwa kuendeleza mazoezi kama kukimbia, kusafiri na wakati wake wa ziada aliutumia kutembelea marafiki au familia ama kucheza na mbwa wake.

Janga la virusi vya corona lilipoanza kukumba jimbo la Illinois, hofu ya kupata maambukizi kulimfanya kuchukua tahadhari zaidi: Alianza kufanyakazi akiwa nyumbani na ikawa nadra sana kwake kutoka nje.

Lakini Aprili alipoanza kuhisi vibaya, dalili zikaanza kujitokeza.

"Ni kipindi kigumu sana kuwahi kukipitia maishani mwangu. Nilikuwa nafanya kazi nyumbani na nilipoanza kupoteza hamu ya kula na kukosa harufu, mimi nilikuwa ninafanya kazi nikiwa nyumbani. Nilikuwa nahisi uchovu wa ajabu, nikawa na matatizo ya kupumua na sikuweza kutembea mwendo mrefu," anakumbuka.

Aliwasiliana na maafisa wa kukabiliana na virusi vya corona kulingana na ushauri uliokuwa umetolewa. Walimsihi kujitenga nyumbani na kufuatilia dalili alizokuwa nazo.

Lakini kila siku hali ilizidi kuwa mbaya.

"Aprili 26 hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi na nikapelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Walinipima na kugundua kwamba kiwango changu cha oksijeni kilikuwa chini sana. Na ndani ya dadkika 10 tu walikuwa wananitaka niwape jina la mtu ambaye wangezungumza nae ili waweze kufanya maamuzi yao ya kitabibabu", Marya anakumbuka.

Hiyo ndio kumbukumbu yake ya mwisho.

Mwanamke huyo mara moja alidungwa sindano ya usingizi na kuunganishwa na mashine kadha wa kadha papo hapo, mashine inayosaidia moyo kufanyakazi na matatizo ya kupumua.

"Nilikuwa kwenye mashine za kusaidia kupumua kwa wiki sita," anasema.

Kipindi chote hicho, anakumbuka tu kuota ndoto mbaya ambazo bado zinamuandama mpaka leo.

"Wakati huo nilikuwa na ndoto ambazo bado zinaniathiri mpaka leo, na nikaanza kurejesha uwezo wangu wa kubaini vitu pamoja na kuimarika kwa afya yangu ya akili," anasema.

Kumuaga binti yao kwasababu anakaribia kufa

Lakini baada ya mwezi mmoja na nusu ya kuwa kwenye mashine ya kusaidia kupumua, Mayra hakuonesha dalili zozote za afya yake kuimarika na tayari mapafu yake yalikuwa yameanza kuathirika kiasi cha kutoweza kutibiwa tena.

"Hapo ndipo waliwaambia wazazi wangu kuwa mapafu yangu yameharibika vibaya na kuwaomba kufika hospitalini kumuaga mtoto wao kwasababu hawangempata akiwa hai usiku uliofuata."

Hata hivyo timu ya madaktari iliamua kufanya uamuzi hatari: walifanya tathmini yao ya haraka, wakawasiliana na familia na hatua ya mwisho waliamua kumfanyia tena upandikizaji wa mapafu.

Ni matibabu ambayo awali yalijaribiwa katika nchi za Austria na China kwa wagonjwa wa virusi vya corona lakini hadi wakati huo hakukuwa na matibabu ya awali ambayo yangetumika kama mfano nchini Marekani.

"Punde tu baada ya kufanyiwa upandikizaji, moyo wake ulianza tena kupeleka damu kwa njia stahiki katika viungo vingine vyote," amesema Dkt. Bharat.

Wiki nne baadae, alikuwa ametoka hospitali. Na sasa hivi yuko nyumbani, anazungumza vizuri na mwenye oksijeni ya kutosha," ameongeza.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na hospitali, kisa cha Marya na mwanamume mwingine aliyefanyiwa upasuaji wa aina hiyo muda mfupi baada ya kujitokeza kwa dalili kama hizo, baadae ilijitokeza wazi kwamba upandikizaji wa mapafu mara mbili pia kunaweza kuwa chaguo kwa wagonjwa aliyeathirika vibaya na virusi vya corona.

Kwa Marya, baada ya kufanyiwa oparesheni, sio tu alianza safari ndefu ya kupata afueni lakini pia alilazimika kuanza kujifunza tena namna ya kupumua na vile mtu anavyoweza kutembea.

Pia, anasema anakabiliana na hisia kali na makovu ya kisaikolojia ambayo atasalia nao katika kipindi chote cha maisha yake.

"Sasa nahisi afueni kubwa nikilinganisha na siku niliyotoka kufanyiwa upandikizaji. Niliketi kwenye makazi ya kujifunza tena kutembea na kupata ushauri nikiendelea kupata uponyaji kwa wiki tatu ambako kumenisaidia kuimarisha afya yangu na uwezo wa viungo vyangu lakini bado najaribu kukabiliana na janga hili kwa mtazamo wa afya ya akili."

"Ni mchakato unaokwenda kwa kasi ya polepole, lakini nina nafuu kubwa."

Pia unaweza kusema: