Shambulio la bomu lawaua watoto 3 Burundi huku wengine 8 wakijeruhiwa

Iliyochapishwa

Shambulio la guruneti limewaua watoto watatu waliokuwa wakitazama runinga katika dula moja la ususi karibu na mji mkuu wa Burundi. Bujumbura, maafisa wa usalama wamesema.

Watoto wengine wanane walijeruhiwa katika mlipuko huo mapema Alhamisi katika makaazi ya Gahahe kandokando ya mji wa Bujumbura , msemaji wa polisi amesema.

Picha za watoto waliojeruhiwa na akina mama waliokuwa wakilia katika eneo hilo la mkasa zimechapishwa katika mitandao ya kijamii.

Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na shambulio hilo , kulingana na polisi.

Haijulikani iwapo watoto hao walio kati ya umri wa miaka sita hadi 12 ndio waliokuwa wakilengwa.

Watoto wa shule kwa sasa wako likizo nchini Burundi.

Watoto kutoka familia masikini ambazo hzina runinga mara nyingi husimama nje ya maduka hayo ya kusuka nywele ili kutazama vipindi kupitia madirisha.