Jinsi Marekani, Israel na Hezbollah zilivyohusishwa na mlipuko wa Beirut katika mitandao

Large warehouse destroyed by a huge explosion in Beirut port

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mlipuko ulisababisha uharibifu mkubwa katika bandari ya Beirut
Iliyochapishwa

Ripoti za mapema kuhusu mlipuko wa bandari ya Beirut zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya mlipuko.

Huku kanda nyingi za video zikionekana kuwa halisi, zikirekodiwa na wakaazi kutoka nyumba zao, uvumi kuhusu chanzo cha mlipuko ulisambaa katika mitandao mingi ya kijamii kama vile Twitter na WhatsApp.

Je ni habari gani za kupotosha zilizosambaa?

Kuanzia za fataki hadi bomu la kinyuklia

Kanda za video zilizokuwa zikisambaa zilionesha milipuko na moto na kufuatiwa na mlipuko mkubwa.

Hatua iliopelekea machapisho ya twitter kusema kwamba mlipuko huo ulitokea katika kiwanda cha kutengeneza fataki.

Madai kuhusu fataki yalionekana kuwa ya kweli wakati huo , lakini machapisho mengine yaliosambaa yalionesha kwamba tukio hilo lilisababishwa na bomu la kinyuklia baada ya wingu jeupe lililofanana na uyoga kuonekana wakati wa mlipuko.

Chapisho lililofutwa ambalo lilikuwa likisema kwamba mlipuko huo ulisababishwa na bomu la atomiki lilisambazwa na akaunti moja ya Twitter isiojulikana huku wafuasi 100,000 wakisambaza na hata ku like.

Screenshot of a post making the false claim that the mushroom cloud created by the explosion in Beirut was "atomic". We labelled the post "false"
Maelezo ya picha, Ujumbe wa Twitter wenye madai ya uongo kwamba mlipuko wa Beirut ni bomu la atomiki

Wataalamu wa mabomu wanasema kwamba iwapo bomu hilo lingesababishwa na nyuklia, lingeandamana na mwanga mweupe na kuongezeka kwa viwango vya joto ambavyo vingechoma watu kadhaa.

Pia mawingu ya uyoga hayatokei wakati wa bomu la nyuklia pekee.

Bomu au shambulio la kombora

Madai ambayo hayakuthibitishwa yaliendelea kusambaa yakidai kwamba Marekani, Israel au Hezbollah ndio ya kulaumiwa.

Habari hizo zilisambazwa na tovuti za habari pamoja na watu maarufu.

Uvumi wa kupotosha uliokuzwa na makundi yenye mrengo wa kulia pia ulisambazwa katika Facebook, 4chan, Reddit na programu za ujumbe kama vile telegram, kulingana na utafiti kutoka kwa taasisi ya mazungumzo ya kimkakati.

Ujumbe umeangazia madai ya uongo kwamba hilo lilikuwa shambulio la Israel, lililolenga ghala la kuweka silaha la Hezbollah.

Screenshot of a post making the false claim that a missile was responsible for the explosion in Beirut - suggesting the target was a Hezbollah missile storage facility
Maelezo ya picha, Madai ya uwongo yanayosambaa mtandaoni yanaonesha bomu ndio lilisababisha mlipuko Beirut

Chloe Colliver, kutoka taasisi ya mazungumzo ya kimkakati aliambia BBC: Tumeona vyanzo visivyo na udhibiti wa habari likiwemo kundi la mrengo wa kulia vikisambaza madai kuhusu sababu za mlipuko huo.

Hii imeshirikisha nadharia zinazojaribu kuhusisha mlipuko huo na Israel ama mataifa mengine.

Mamlaka nchini Lebanon na Israel zimefutilia mbali madai kwamba Israel ilihusika kwa njia moja aeu nyengine.

Nadharia za mrengo wa kulia, ikiwemo wafuasi wa QAnon, wameanza kusambaza madai ya uongo kuhusu mlipuko huo katika mtandao wa facebook.

Wanasema kwamba shambulio hilo linahusishwa na vita kati ya serikali na mfumo wa kati wa benki.

QAnon ni nadharia potofu inayosema kwamba rais wa Marekani Donald Trump ameanzisha vita baridi dhidi ya watu wanaoabudu shetani katika serikali , biashara na hata vyombo vya habari.

Waziri mkuu wa Israel hakuotesha eneo la mlipuko wa 2018.

Picha za waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akilihutubia baraza kuu la umoja wa mataifa 2018 zilichapishwa katika mitandao ya kijamii huku kukiwa na madai kwamba alikuwa akiotesha eneo la mlipuko wa Beirut.

Baadhi ya watuamiaji wa mitandao wanatumia picha kama thibitisho kwamba israel ilikuwa na mkono katika mlipuko huo.

Waziri Mkuu wa Israel hakuzungumzia mlipuko wa 2018

Benjamin Netanyahu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Israeli katika Umoja wa Mataifa 2018

Ukweli ni kwamba bwana Netanyahu anaotesha wilaya tofauti katika mji huo wa Beirut ambapo alidai kwamba Hezbollah inaficha silaha zake. Eneo la mlipuko huo lipo kilomita kadhaa kaskazini mwa Eneo la tukio katika ramani ya bwana Netanyahu.

Matamshi ya Trump

Uvumi kuhusu uwezekano wa shambulio ulisambaa baada ya rais Trump kuelezea tukio hilo kama shambulio baya katika mkutano na vyombo vya habari katika Ikulu ya Whitehouse.

Two screenshots labelled "false" featuring Donald Trump at a press conference with fabricated quotes attributed to him suggesting the US president called the explosion a terrorist attack
Maelezo ya picha, Ujumbe wa kwenye mitandao wa kijamii unaonesha ujumbe wa uwongo kwa Rais Trump

Pia kuna madai kutoka kwa taarifa ya rais Trump kuhusu mlipuko huo, ambazo zimetia moto uvumi na habari potofu katika kipindi cha saa 24 baada ya mlipuko.

Machapisho mengine ya mitandao yalitoa madai ya uongo kwamba bwana Trump alisema kwamba Marekani ilionywa kuhusu mlipuko huo.