Virusi vya corona: Trump afuta kongamano la chama cha Republican kwa kuhofia maambukizi

Iliyochapishwa

"Huu sio wakati mwafaka wa kufanya hivyo," alisema, na kuongeza kwamba bado atatoa hotuba aliopanga kwenye mkutano huo kwa njia tofauti.

Baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican wataendelea kukutana Charlotte, North Carolina, eneo ambalo mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika awali.

Bwana Trump alikuwa amehamisha sehemu ya mkutano huo Florida kwasababu ya kanuniza kutokaribiana zilizoanzishwa North Carolina.

Katika tukio hilo la nusu siku, Agosti 24, rais atachaguliwa rasmi na chama chake kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama katika uchaguzi wa urais unaofanyika Novemba.

Rais alisema nini?

Katika mkutano kuhusu taarifa za ugonjwa wa virusi vya corona, akiwa Ikulu ya Marekani Bwana Trump, Alhamisi amesema kwamba usalama ndio angalizo lake kuu huku akitoa wito wa kufutiliwa mbali kwa matamasha manne ya usiku.

"Ni dunia tofauti, na hali hii itaendelea kwa muda kidogo," rais alisema akiongeza kwamba "alihisi kufanya hivyo itakuwa makosa" kuhatarisha maisha ya maelfu ya watu.

"Hatukutaka kuhatarisha maisha hata kidogo," aliwaambia wanahabari. "Ni lazima tuwe waangalifu. Lazima tuwe makini na ni lazima tuwe mfano wa kuigwa na wengine."

Ofisi ya Jacksonville sheriff shirika la kaunti linalosimamia utekelezaji wa sheria lilionya wiki hii kwamba mji huo hauko tayari kwa mkutano mkubwa wa kisiasa uliopangwa kufanyika mwzi ujao.

Florida - jimbo muhimu katika matumaini ya kuchaguliwa tena kwa rais kwenye uchaguzi wa urais - uko nyuma tu ya California na New York kwa idadi jumla ya maambukizi ambayo imerekodiwa.

Bwana Trump alibadilisha eneo la kufanyia mkutano hadi Florida baada ya gavana wa chama cha Democratic wa North Carolina kusisitiza mwezi Mei umuhimu wa kupunguza mikusanyiko katika mkutano ulipangwa kufanyika wa chama cha Republican akitaja suala la kutokaribiana.

Kura za maoni zinaonesha kwamba Bwana Trump anakibarua kigumu cha kufanya wakati anawania kuingia madarakani kwa muhula wa pili huku akiendelea kukosolewa na jinsi anavyoshughulikia janga la virusi vya corona.

Hatua hiyo imepokelewa vipi?

Maafisa wa chama cha Democratic wamemkejeli rais kwa tangazo lake. Itakapofika Agosti, watafanya karibu kila mkutano kwa njia ya video, ule wa Milwaukee, Wisconsin, ambapo mpinzani wa Bwana Trump, Joe Biden, atakubali rasmi hatua ya kuchaguliwa kwake na chama.

Mpangaji wa mikakati wa chama cha Democratic kwa mikutano ya chama hicho alisema: Najiuliza ni nani atakayekuwa na mkutano wa kufana, chama ambacho kilitambua umuhimu wa mikutano ya njia ya video kitambo na kuanza kujipanga ikilenga mamilioni ya watazamaji wakati ambao wanapatikana au wanasarakasi wanaohamisha mikutano yao kutoka sehemu moja hadi nyingine na wasio na mpango madhubuti."

Katika mkutano ambao ulikuwa unazingatia kutokaribiana, Alhamisi, Bwana Biden na aliyekuwa rais Barack Obama, walimkosoa Bwana Trump kwa alichosema Machi "Mimi siwajibiki kabisi" - alipoulizwa kuhusu kuhusu kuchelewa kwa shughuli ya kupima raia kubaini ikiwa wamepata maambukizi ya ugonjwa Covid-19.

"Hebu fikiria umesimama kisha unasema 'Sio jukumu langu na wewe ndio rais?" amesema Bwana Biden, aliyekuwa makamu rais, katika mazungumzo yao yaliyokuwa yamerekodiwa wiki iliyopita.

Bwana Obama alijibu: "Maneno kama hayo hayakuwahi kutoka kinywani mwetu wakati tupo uongozini."

Hali halisi ikoje nchini Marekani?

Maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani yamepita milioni 4 Alhamisi huku idadi ya vifo ikiwa ni zaidi ya 144,000.

Jumatano, idadi ya maambukizi California ilipita idadi ya New York - eneo lililokuwa kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo Marekani - huku maambukizi yaliyothibitishwa yakiwa 409,000.

Siku hiyo hiyo, miji ya Missouri, North Dakota na West Virginia yote hayo yalivunja rekodi zao kwa mara ya kwanza katika idadi ya maambukizi iliyoripotiwa ndani ya saa 24.

Miji ya Alabama, Idaho na Texas pia imerekodi idadi ya juu ya vifo kwa siku.

Jumatatano, kote Marekani idadi ya maambukizi mapya ilikuwa 69,707.

Wabunge wa Republican na Democrats wanajadiliana kufikia makubaliano ya kupitisha pesa kwa mara tano za kuchechemua uchumi.