Virusi vya corona: Kenya kuanza majaribio ya dawa ya kupambana na virusi vya corona

Sampuli ya virusi vya corona

Chanzo cha picha, ANADOLU AGENCY

Iliyochapishwa

Tayari, wagonjwa kumi nchini Kenya wanashiriki katika jaribio hili la kimataifa unaoitwa EMPACTA katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan.

Wale wanoshiriki katika jaribio hili ni wagonjwa ambao wamepitakana na Covid-19 na CT scan yao inaonyesha kuwa wakona nimonia inayohusiana na corona na wanahitaji oksijeni.

Madaktari watatathmini ufanisi na usalama wa Actemra (tocilizumab) dawa iliyotengenezwa na kampuni ya Roche katika jaribio hili.

Daktari Reena Shah, mtaalam wa magonjwa yanayoambukizwa kwa haraka na mpelelezi ku wa jaribio hili ameitaja kama wakati muhimi nchini Kenya.

"Huu ni wakati wa furaha nchini Kenya na katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kwamba tunaweza kushiriki katika jaribio la kliniki la kimataifa ambalo linajaribu ufanisi wa dawa hii kwa wagonjwa wetu hapa." Dk Reena Shah alisema.

"Hapa ndipo tunachangia maarifa na uzoefu juu ya uwezo wetu na matokeo ya wagonjwa wetu kwa jamii ya kimataifa." aliongeza

Kuongezeka kwa idadi ya sampuli za vi[pimo zinazochukuliwa kutoka kwa raia wa Kenya kumeifanya idadi ya watu waliombakuzwa corona kupanda.

Chanzo cha picha, Getty Images

Dawa hii ya tocilizumab, ambayo inatumika katika matibabu ya saratani na kwa ugonjwa wanaougua arthritis inatumika sasa katika jaribio hili la kliniki la Awamu ya tatu kwa matumaini kwamba itamzuia mtu kuwa na ugumu wa kupumua.

Katika jaribio hili, hakuna atakayejua ni mgonjwa yupi aliye kwenye dawa ya tocilizumab na ni nani yuko kwenye dawa ya kutuliza (placebo).

Matokeo ya awali ya utafiti huu yatajulikana baada ya miezi mitatu.

Mbali na Kenya jaribio hili linafanyika katika mataifa ya Afrika Kusini, Brazil, Mexico na Peru.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Michigan waligundua kuwa uchunguzi uliofanywa kwa wagonjwa 154 wenye ugonjwa kali wa COVID-19 waliohitaji kupewa oksijeni, dawa ya tocilizumab iliripotiwa kupunguza vifo kwa 45%.

Mwanasayansi akifanyia uchunguzi virusi vya corona katika maabra

Chanzo cha picha, EPA

Ni miezi mitatu tangu shirika la afya duniani WHO kutangaza kwamba kusambaa kwa virusi vya Covid-19 kumesababisha janga.

Ilikuwa tarehe 11 mwezi Machi na tangu wakati huo tafiti chungu nzima zimezinduliwa kuhusu tiba ya ugonjwa huo.

Ukweli ni kwamba tayari hatua kubwa zimeafikiwa katika utafutaji wa tiba ya maradhi hayo.

Maabara zilizopo katika mataifa tofauti duniani zimeanza kuchunguza takriban tiba 150.

Baadhi yake tayari zilikua zikiuzwa katika maduka ya dawa na sasa zinafanyiwa vipimo iwapo zinaweza kutibu ugonjwa huo.

WHO imekuwa ikizifanyia majaribio dawa zinazoleta matumaini kwa mgonjwa.

  • Uingereza inasema kwamba majaribio yake kwa jina Recovery ndio makubwa zaidi duniani. Zaidi ya wagonjwa 11,000 wameshiriki katika utafiti huo.
  • Mojawapo ya dawa zinazofanyiwa utafiti dexamethasone , imeonesha kusaidia maisha ya wagonjwa wa corona walio katika hali mahututi .
  • Vituo kadhaa vya utafiti vinajaribu kutumia damu ya wagonjwa waliopona virusi hivyo vya corona kutafuta dawa.
coronavirus

Habari zaidi kuhusu virusi vya corona: