Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Onyo latolewa kufuatia wizi wa sampuli za damu ya virusi vya corona Afrika kusini
Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza wizi wa lori lililokua limebeba sampuli za Covid-19 katika mji wa Port Elizabeth siku ya Jumatatu.
Sampuli hizo zinaripotiwa kupotea. Zilikuwa zimewekwa ndani ya maboksi yaliyokuwa yamejazwa barafu.
Maafisa wa afya nchini humo wamewaonya walioiba sampuli hizo pamoja na umma wasiziguse kwasababu zina uwezekano mkubwa wa kuwa na maambukizi , umeripoti wavuti wa habari wa - Newa24 ambao ulinukuu mamlaka ya hutuma za maabara za kitaifa katika jimbo la Eastern Cape.
''Mtu yeyote ambaye ataliona kasha hilo jeupe anatakiwa kuripoti kwa polisi. Tumetoa onyo hilo ili kuhakikisha kuwa kila mtu ana ufahamu. Tunafuraha kwamba suala hili linachunguzwa . Tunashirikiana na mashirika yote na taaissi za serikali katika sekta ya Afya kukabiliana na changamoto kama hizi huku tukisonga mbele''.
Maafisa wanachunguza idadi ya sampuli zilizoibwa kabla ya kubaini ni watu wangapi watakaopimwa tena, umeripoti wavuti huo.
Lori hilo liliibiwa katika eneo la kuegesha magari la kliniki na kutelekezwa muda mfupi baadae, kulingana na Shirika la habari la Afrika Kusini SABC.
Tayari watu wapatao milioni 2.5 wamefanyiwa vipimo vya virusi vya corona nchini Afrika Kusini. Kwa sasa kuna watu 871 waliofariki kutokana na corona mashariki mwa Cape huku wagonjwa 65, 316b
Nchi hiyo ina idadi ya juu zaidi ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya corona barani Afrika.