Virusi vya corona: Uwezekano wa ufanisi wa kipimo cha kutema mate kumaliza janga la corona

Iliyochapishwa

Tatizo la kwanza ni kwamba ni wachache chini ya mtu mmoja kati ya watu wanne wanaopatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa ambayo huwa wanakuwa na dalili za ugonjwa huo siku wanayopimwa.

Hilo linaonesha hatari ya virusi kuenezwa na watu ambao hawajui kuwa wameambukizwa.

Suala la pili ni kipimo chenyewe cha Covid -19. Kwa sasa njia inayokubalika ya kubaini virusi vya corona ni kuingizwa kwa mrija wenye pamba unaopitishwa puani hadi nyuma ya koo ambako huchukua mate yanayopimwa kwenye maabara ili kutambua kuwa una virusi au hauna.

Japo ni kitendo kinachofanyika sekunde chache, watu wengi hawapendi njia hiyo ya kupima corona kwani huhisi haiwafurahishi.

Tatizo jingine ni muda. Sampuli inapochukuliwa ni lazima ipelekwe maabara na kuchukua mchakato wa saa kadhaa. Wengi hupata majibu baada ya saa 24, na pengine usipate huduma hiyo kwa wakati unaoutaka wewe.

Kwahiyo kile tunachokihitaji ni kipimo cha haraka, rahisi na cha kuaminika cha Corona.

Baadhi ya vipimo vya haraka vya sampuli vinafanyika , ambavyo itakua ni hatua kubwa katika katika kukabiliana na maambukizi ya corona.

Lakini vipimo vya mate vinaweza kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika vita dhidi ya Covid-19.

Fikiria kama ungekua unahitajika tu kutema mate kwenye chupa ya maabara na kuweza kubaini kuwa una virusi vya corona au hauna.

Ni kweli kwamba haitakua rahisi kiasi hicho, kwani sampuli ya mate yako itapelekwa kwanza maabara, lakini matokeo yanaweza kupatikana haraka zaidi kuliko yale ya vipimo vilivyopo sasa.

Jayne Lees na familia yake wamejitolea kuwa sehemu ya majaribio ya vipimo vya mate vinavyofanyika katika mji wa Southampton Nchini Uingereza.

" Tunafikiri mate ni kimiminika muhimu kukifanyia vipimo kwa kweli ,"anasema says Keith Godfrey katika Chuo kikuu cha Southampton nchini Uingereza ambaye anasaidia kuratibu majaribio ya kipimo cha mate.

" Vyanzo vya mate (salivary glands) ni sehemu ya kwanza inayopatwa na maambukizi virusi mwilini. Inaonekana virusi hupatikana kwenye mate ya watu kabla ya kusambaa kwenye mifumo ya upumuaji

Mafanikio ya jaribio la kipimo hiki yatatokana na jinsi kipimo cha mate kitakavyoweza kupima kwa uhakika na kubaini virusi vya corona.

Sampuli kutoka katika utafiti wa mji wa Southampton nchini Uingereza zinapitia mchakato wa kuhakikiwa katika maabara ya serikali ya wanyama na mimea lililoko eneo la Surr nchini humo. Sampuli hizo zinaongezewa kemikali na kuchemshwa ili zitoe jeni za virusi. Njia hii inayofahamika kama - RT-Lamp kwa lugha ya kitaalamu, huchukua takriban dakika 20, ikilinganishwa na ile inayotumiwa sasa ya kipimo cha PCR ambacho huchukua saa kadhaa kutoa matokeo.

"Tunafurahi sana ," anasema Profesa Ian Brown, mkuu wa kitengo cha kupambana na virusi. "Tulikua na mafanikio makubwa katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, katika kuzikabili changamoto za kiufundi kwa kuweza kutumia kipimo cha mate ."

Hapa ndipo mambo yanakua ya kufurahisha. Kama majaribio ya awali yatafanikiwa, mji wote wa Southampton, watu zaidi ya 250,000, wanaweza kufanyiwa vipimo vya mate kila wiki.

Baadhi wangetaka mambo yafike hata mbali zaidi. Kikundi cha wanasayansi kinachoongozwa Profesa Julian Peto wa Chuo cha tiba jijini London anasema watu wote wa Uingereza wanapaswa kufanyiwa kipimo hiki cha kutema mate kubaini virusi vya corona.

Jinsi itakavyofanyika ni hivi;

Utakapotema mate na kupeleka kwenye maabara . Utapata majibu katika kipindi cha saa 24 kwa njia ya ujumbe mfupi. Kama majibu ni chanya wewe na familia yako mtatakiwa kujitenga. Migahawa ya chakula na maeno mengine ya Umma inaweza kuwataka watu kutoa ushahidi wa vipimo vyao vya karibuni kabla ya kuingia kupata huduma. Matumaini ni kwamba kuwatambua mapema wale walioambukizwa kutamaliza haraka janga.

Kama kipimo cha mate kitakuwa cha ufanisi, itamaanisha kwamba utakua ndio mwisho wa uvaaji wa barakoa na kujitenga kwa mamilioni ya wazee na watu wengine wenye uwezekano wa kupata maambukizi kwa urahisi. Utaweza kumkumbatia rafiki yako na babu au bibi yako tena.

Shule zitaweza kuwapima wanafunzi na wafanyakazi wa shule kila wiki. Vipimo vya mara kwa mara vya mate pia vinaweza kufanywa katika nyumba za wazee au katika maeneo yenye maambukizi zaidi ya mengine. Maabara zinaweza kuwekwa katika viwanja vya ndege , kwa hiyo abiria wanaoingia na kutoka wataweza kupimwa wakati wanasubiri ndege zao kuondoka