Virusi vya corona : Watu waliolewa hawawezi kufuata kanuni ya kutochangamana

Maafisa wa polisi wakitembea katikati ya makundi makubwa ya watu Soho, katikati ya Jiji la London

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

''Ni wazi kabisa'' kuwa watu waliolewa hawawezi kufuata kanuni ya kutochangamana, mkuu wa polisi alieleza vile anavyoona hali ya shangwe ilivyokuwa baada ya vilabu vya pombe kufunguliwa tena siku ya Jumamosi.

Mawaziri walitoa angalizo wakati wa kuelekea kufunguliwa kwa maeneo yanayoruhusu mikusanyiko nchini Uingereza baada ya kufungwa kwa miezi mitatu, watu wakibaki nyumbani.

Hali ilikuwa ya heka heka nyingi John Apter anasema alishughulika na watu wa kila namna '' watu walio uchi'' waliolewa wakiwa na furaha, walevi wenye hasira, na wenye hasira zaidi'' alipokuwa zamu mjini Southampton.

Watu walionekana wamepiga kambi nje ya vilabu vya pombe saa za asubuhi siku ya Jumapili.

Polisi wa kaunti za Devon na Cornwall walipokea zaidi ya ripoti 1,000, nyingi miongoni mwao zenye uhusiano na ''ulevi''.

Vilabu vya pombe katika mtaa wa Hilton jijini Manchester viliandaa meza kwaajili ya wateja

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika maeneo mengine, watu walishindwa kabisa kufuata kanuni za wataalamu wa afya ya kutochangamana, huku wamiliki wengine wa vilabu kadhaa vya pombe wakiamua kufunga baada ya watu waliokuwa wamelewa kushindwa kabisa kujizuia kuonesha nidhamu, hali iliyosababisha watu wanne kukamatwa katika kaunti ya north Nottinghamshire.

Wakati umati wa watu ulipojitokeza katika maeneo mbalimbali, kulikuwa na hofu ya kuhitajika kwa huduma za dharura kama vile ilivyo kwenye shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya.

Bwana Apter, kutoka idara ya polisi alisema: ''Kilichokuwa bayana ni kuwa watu waliolewa hawawezi/hawataweza kufuata kanuni ya kutochangamana.

''Ulikuwa usiku wenye pilikapilika. Ninajua maeneo mengine maafisa wa polisi walishambuliwa.''

Watu waliokuwa kwenye shamrashara walikunywa na kukutana katika mtaa mmoja Soho, jijini London

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Watu waliokuwa kwenye shamrashara walikunywa na kukutana katika mtaa mmoja Soho, jijini London

Watu nchini Uingereza bado wametakiwa kukaa umbali wa mita mbili, lakini umbali huu unamaanisha kuwa wanawaweza kukaribiana kama wanatumia njia kama za kufunika uso na kutokaa karibu karibu.

Watu wakiwa kwenye makundi makundi katika soko la Borough, jijini London

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Watu wakiwa kwenye makundi makundi katika soko la Borough, jijini London

Waziri Mkuu, Boris Johnson na wataalamu ndani ya serikali waliwaasa watu kufuata kanuni kuepuka wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona, huku afisa mkuu wa idara ya afya nchini Uingereza Chris Whitty akisema kuwa kupunguza makali ya masharti ya kutotoka nje hakuna maana kuwa ''hatari ya maambukizi imekwisha.''

Takwimu zilizotolewa Jumamosi, zilieleza kuwa watu 67 wamepoteza maisha nchini Uingereza baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona, na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 44,198.

Kundi la watu wakiwa nje ya mgahawa Whitby

Saluni za nywele na harusi

Saluni za wanawake na wanaume zimefunguliwa tena England siku ya Jumamosi.

Misururu mirefu ya watu ilikuwa nje ya saluni za kiume na wengine waliweka ahadi ya usiku kupata huduma hiyo.

Maeneo mengine yaliyofunguliwa England ni;

  • Maeneo ya kufanya mazoezi
  • Maktaba, maeneo ya Umma, sinema, makumbusho na sehemu za maonesho ya picha
  • Bustani, sehemu za michezo , vilabu.
  • Maeneo ya kuabudu yatakuwa wazi na huduma nyingine,pia shughuli za harusi zimeruhusiwa kufanyika.
Coronavirus

Unaweza pia kusoma: