Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Kinga ya mwili inaweza kusambaa kuliko vipimo vinavyoonesha
Watu wanaopimwa na kukutwa hawana kinga za virusi vya corona wanaweza bado kuwa na kinga ya kukabiliana na virusi, utafiti umebainisha.
Kwa kila mtu anayepima na kukutwa na kinga ya mfumo wa kinga unaopambana na a bakteria, wawili walibainika kuwa na seli maalumu zinayojulikana kama T-cells ambazo hutambua na kuua seli zilizoathirika.
Hii ilionekana hata miongoni mwa watu ambao walikuwa na dalili ndogo au za mapema za virusi vya corona.
Lakini haijawekwa wazi kama hali hiyo inamlinda mtu husika au kama, inaweza kusaidia kuwazuwia kueneza maambukizi hayo kwa mtu mwingine.
Watafiti katika taasisi ya Karolinksa nchini Sweden waliwapima watu 200 kwenye upande wa kinga ya virusi na T-cells.
Baadhi walikuwa wachangiaji damu huku wengine wakibainika kutoka katika kikundi cha watu wa kwanza walioathirika na maambukizi nchini Sweden, hasa wale waliokuwa wamerejea kutoka katika maeneo ambayo yalikuwa yameathirika na corona kama vile kaskazini mwa Italia.
Hii ikimaanisha kuwa kundi kubwa la watu wana kinga ya Covid-19 zaidi ya takwimu za waliopima virusi, kama takwimu ambayo ilichapishwa na sehemu ya ofisi ya takwimu za taifa za utafiti wa maambukizi nchini Uingereza.
Kuna uwezekano watu wale walikuwa na kinga ya virusi , lakini labda ilikua imeshuka au haivikuweza kuonekana katika vipimo vya sasa.
Na watu hawa wanapaswa kukingwa iwapo wana uwezekano wa kupata virusi kwa mara nyingine.
Prof. Danny Altmann kutoka chuo cha Imperial mjini London anaueleza utafiti huo kama "imara, wa kuvutia na usio na makosa" na akasema umeongezea ushahidi katika ushahidi unaoendelea kupataikana kwamba kwamba "kinga kupima kinga inayopambana na maradhi pekee haitoshi kubaini ufanisi wa kinga nzima ya mwili ".
Kinga inayozuwia kusambaa kwa ugonjwa
Hii si lazima kinga yoyote ya kundi la aina ya watu fulani, kwa mujibu wa Profesa msaidizi, Marcus Buggert, ambaye ni miongoni mwa waandishi wa utafiti huo.
Tathmini zaidi inahitajika kufanyika ili kuelewa kinga ambayo inatolewa na 'T-cells' (seli ambazo hutambua na kuua seli zilizoathirika ) ambayo ni kinga ya kipekee inayoweza kuzuia watu kupata virusi au inaweza kumlinda mtu dhidi ya magonjwa lakini pia sio kumzuwia mtu kupata virusi na kuvisambaza kwa wengine.
Majadiliano mengi kuhusu kinga ya Covid-19 yanaangazia kinga ya mwili - ambayo inamlinda muhusika, Profesa msaidizi Buggert anaelezea.
Kinga hiyo inazuia virusi kuingia kwenye seli za mwili na kupata maambukizi.
Kama kinga ya mwili ikishindwa kukabiliana navyo basi virusi hivyo vinaweza kuingia na kubadilika kuwa sehemu ya kutengenezea virusi.
Kwa upande mwingine 'T-cells', inalenga seli zilizoathirika na kwa ujumla, kuzuia virusi hivyo kusambaa kwa wengine, na seli ambazo ni imara.
Mara tu virusi vya aina fulani vitakapobainika, inaweza kulenga kwa haraka seli zilizoathirika na kuziangamiza.
Dawa inayoitwa interleukin 7,inafahamika kama uzalishaji wa T-cell ambazo zinatoa kinga katika mwili, jaribio ambalo lilifanyika Uingereza linaonyesha kuwa inaweza kusaidia wagonjwa kupona.
Kuharibika kwa T-cell
Watafiti kutoka taasisi ya Francis Crick, King's College London na wengine kutoka hospitali ya St. Thomas wameelezea jinsi seli ilivyojitenga katika kundi la wagonjwa 60 ambao walionekana kushambuliwa na T-cells ambayo imeathirika.
Suala hili halikuonekana katika utafiti uliofanywa Karolinska ambayo inafanya mgonjwa kuwa mgonjwa zaidi na kiwango cha kinga ya virusi katika mwili kuwa ya juu zaidi na seli za kinga ya mwingine kutengenezeka.
Watafiti hao wanasema kuwa utafiti zaidi unahitajika.
Wakati utafiti mkubwa uliofanywa katika T-cell mpaka sasa ambao ulijumuisha kundi dogo la wagonjwa.
Si rahisi kubaini 'T-cells' katika kinga ya mwili, kwa kuwa ni vigumu kuonekana na huhitaji vipimo maalumu na kiwango kidogo cha sampuli kupimwa huwa inachukua siku kadhaa.
Hivyobasi upimwaji wa 'T-cells' kwa ujumla si rahisi kuonyesha matarajio yako kwa wakati.