Virusi vya corona: Wimbi la pili la corona likoje na linaweza kutokea vipi?

Graph

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Virusi vya corona havitaisha hivi karibuni. Baadhi ya nchi bado zinashughulikia mlipuko mkubwa, lakini hata zile ambazo zimeweza kudhibiti virusi zinahofia "wimbi la pili".

Awamu ya pili ya Spanish flu karne iliyopita ilikua mbaya kuliko awamu ya kwanza.

Kwahivyo, ni lazima kutakuwa na wimbi jingine? na je wimbi la pili linaweza kuwa baya kiasi gani?

Kwanza kabisa, Wimbi la pili ni nini?

Unaweza kulifikiria kama mawimbi ya baharini. Idadi ya maambukizi yanapanda na halafu yanashuka tena-kila mzunguko ni mmoja''wimbi'' la virusi vya corona.

Hakuna maelezo rasmi juu ya sababu yake.

"Si jambo la kisayansi, jinsi unavyofafanua wimbi ," Dkt Mike Tildesley, kutoka Chuo kikuu cha Warwick, aliiambia BBC.

Waves

Chanzo cha picha, Getty Images

Baadhi wanaeleza kuwa kupanda kokote kwa wimbi la pili huwa ni kwa kiwango kikubwa zaidi ya wimbi la kwanza. Hii inatokea katika baadhi ya majimbo ya Marekani.

Kusema wimbi moja limeisha, viirusi vingekua vimeweza kudhibitiwa na maambukizi yangekua yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa wimbi la pili kuanza unahitaji ni pale kiwango cha maambukizi kinapopanda bila kukoma.New Zealand, ambayo ilikua na kisa cha kwanza cha maambukizi baada ya siku 24 bila virusi vya corona, na Beijing ambayo inakabiliwa na mlipuko baada ya kuwa na siku 50 za bila maambukizi ya virusi haziko katika nafasi hii.

Je wimbi la pili litakuja Uingereza?

Jibu linategemea maamuzi yatakayofanywa ili kuvifanya virusi viishe.

"Ninadhani kusema ukweli kuna hali kubwa ya sintofahamu…lakini kusema kweli ni jambo linalonitia hiofu sana,'' anasema Dkt Tildseley.

Uwezekano uko wazi huko-virusi bado vipo Uingereza na si kwamba vimepungua uwezekano wa kuuaau vinaambukiza zaidi ya vilivyokua mwanzoni mwa 2020.

Ni karibu 5% ya watu wa Uingerezatu wanaodhaniwa kuwa wameambukizwa na hakuna hakikisho kwamba wote wana kinga ya mwili dhidi ya virusi.

"Ushahidi ni kwamba wengi wa watu bado wamo hatarini, iwapo hatua za kudhibiti maambukizi zitaondolewa hali itakua kama ilivyokua mwezi Februari,anasema Dkt Adam Kucharski kutoka taasisi ya mafunzo ya usafi na tiba ya magonjwa ya maeneo ya joto- London School of Hygiene and Tropical Medicine.

"Ni karibu sawa na kuanzia mwanzo tena."

Coronavirus
Banner

Ni nini kinaweza kusababisha kuwepo kwa wimbi la pili la corona?

Kuondoa amri ya kutotoka nje.

Amri za kutotoka nje imesababisha kuvurugika kwa shughuli nyingi kote duniani, watu wengi kukoasa ajira, imeathiri afya za watu wengi na kuwatoa watoto shuleni-lakini zimeweza kudhibiti virusi.

"Tatizo ni jinsi ya kudumisha udhibiti wa maambukizi huku ukibunguzwa uvurugwaji wa shughuli za kila siku za maisha ," anasema Dkt Kucharski.

Hakuna mtu mwenye uhakika 100% tunaweza kusonga kufikia.

Maelezo ya video, Mume azungumzia machungu ya kumpoteza mke wake aliyekuwa mjamzito kwa corona

Hiyo ndio maana hatua za kudhibiti maambukizi zinaondolewa kwa hatua na njia mpya za kudhibiti virusi vya corona zinaanzishwa, kama vile kutafuta watu waliokutana na wenye maambukizi ya awali- contact tracing au kufunika nyuso kwa barakoa.

"Nchini Uingereza nan chi jirani-maambukizi mapya yanaweza kutokea kama hatua za kudhibiti virusi zitaondolewa na maambukizi yanaweza kufikia kiwango kisichoweza kudhibitiwa '', anasema Dkt. Kucharski.

Hii tayari imeanza kushuhudiwa nchini Ujerumani ambako watu 650 wamepatikana na viriusi baada ya mlipuko uliotokea katika kichinjio.

Shoppers

Chanzo cha picha, Getty Images

Sio tatizo kubwa kama maambukizi yanaweza kubainika haraka, kuanzishwa kwa amri ya kutotoka nje na kusitishwa kwa usambazaji wa virusi vitafanyika.

Vinginevyo, vitachangia kuwepo kwa wimbi la pili la maambukizi.

Korea Kusini ambayo imekua ikisifiwa sana kwa namna ilivyoshughulikia virusi vya corona imelazimika kuweka tena baadhi ya vikwazo kutona na mtandao kama huo wa wa maambukizi.