Donald Trump: Kikosi chake cha kampeni chakanusha madai ya udanganyifu yalisababisha idadi ndogo ya watu katika mkutano wa kampeni

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kampeni inayopigania kuchagliwa tena kwa Rais Donald Trump imepinga madai kwamba kampeni ya mitandao ya kijamii kwa njia ya Tik-Tok na K-Pop fans ndizo zilizosababisha kujitokeza kwa idadi ndogo ya watu katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi iliyofanyika Oklahoma Jumamosi usiku kuliko ilivyotarajiwa.

Vijana wadogo wanasemekana kuwa walijiandikisha kununua tiketi wakiwa na nia ya kutohudhuria mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha viti vinabaki tupu katika mkutano huo.

Lakini kikosi cha kampeni cha 2020 cha Trump 2020 kilisema kuwa kilikua kimeondoa tiketi hizo feki.

Bwana Trump alisema kuwa Bwana Trump anatarajia watu milioni moja kuja kwenye mkutano huo wa kampeni.

Kituo cha mkutano huo maarufu kama The Bank of Oklahoma Center kilichopo eneo la Tulsa ambako mkutano huo ulifanyika kina jumla ya viti 19,000.

Ilitarajiwa kuwa watu wangejaa hadi nje ya uwanja wa kituo hicho na mipango ikawekwa ili kuhakikisha watu wa ziada wanashiriki kikamilifu tukio hilo, lakini mipango hiyo ilifutwa kutokana na kwamba idadi viti vilibaki wazi.

Kikosi cha zimamoto cha Tulsa kimenukuliwa kikisema kuwa zaidi ya viti 6,000 ndivyo vilivyokaliwa katika ukumbi huo, lakini kampeni ya Trump ilisema kuwa idadi ya waliohudhuria ilikua ni ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa kikosi cha kampeni ya Trump alisema katika taarifa aliyoitoa kuwa "maombi ya tiketi za simu hatukuyafikiria" kwani tuliwapokea watu kwa misingi ya yule anayefika ndiye anayehudumiwa kwanza .

Brad Parscale alivilaumu vyombo vya habari na waandamanaji kwa kuzishawishi familia zisihudhurie kampeni hiyo.

"Watu wa itikadi za mrengo wa kushoto na kampeni za mtandao wanafanya kampeni, wakidhani kuwa kwa namna Fulani wataathiri mahudhurio ya mkutano wa kampeni, hawajui wanachokizungumzia au namna mikutano ya kampeni inavyofanyika ," Bwana Parscale alisema.

"Kujisajili kwa mkutano wa kampeni inamaanisha kuwa umethibitisha kuwa utahudhuria kwa namba ya simu na tunatoa mara kwa mara wajumbe gushi, kama tulivyowafanya maelfu katika mkutano wa Tulsa, kwa kuhesabu watu wenye uwezekano wa kuhudhuria."

Marafiki wa zamani wa Republican walikua wameomba "mamia" ya tiketi.

Idadi kubwa ya wazazi walijibu ujumbe uliotumwa na Bwana Schmidt wakisema watoto wao walikua wamefanya sawa na hivyo.

Alexandria Ocasio-Cortez, mtu maarufu, aliwasifu vijana na kampeni mtandao wa kijamii ta K-pop fans akisema kuwa walikua "wamefurika kampeni ya Trump na kujisajili kwa tiketi gushi za kuhudhuria mkutano wa kampeni yake ".

Haijawa wazi ni maelfu mangapi ya yaliyosajiliwa kuwa gushi na kikosi cha kampeni ya Trump, lakini video moja ya mtandao wa kijamii ya Tiktok kuanzia June iliwashawishi watu kujiandikisha kwa ajili ya kupata tiketi za bure ili kuhakikishakunakua na viti vitupu katika uwanja, imepata alama za kupendwa ama LIKES zaidi ya 700,000.

Video hiyo ilitumwa mtandaoni baada ya tarehe ya awali ya mkutano wa kampeni kutangazwa kuwa ni tarehe 19 Juni.

Taarifa ya mkutano huo iliibua ghadhabu kwani ilikuwa ni tarehe ya sherehe za Juneteenth inayosherehekewa nchini Marekani kama siku ya kumalizika kwa Utumwa Marekani. Eneo la mkutano pia lilileta utata, kwani lilikua ni eneo hilohilo ambako yalifanyika mauaji mabaya zaidi yaliyohusishwa na ubaguzi wa rangi katika historia ya Marekani.

Baada ya taarifa ya idadi ndogo ya watu kujitokeza, mmiliki wa akaunti Mary Jo Laupp aliwasifu vijana ,akiwambia vijana ambao hawajafikia umri wa kupiga wapige kura : "Kumbukeni kuwa wewe, katika kufanya jambo moja na kushirikisha watu wengine taarifa, imeleta athari ."

Kama ni ukweli, haitakua mara ya kwanza watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonyesha athari yao kisiasa katika wiki za hivi karibuni.

Mtandao wa Fans of K-pop, kampuni maarufu ta muziki ya Korea Kusini, imekuwa ikitangaza kampeni kupitia hashtags zinazotumiwa na wanaopinga Black Lives Matter (BLM) katika wiki za hivi karibuni, na kuchangisha pesa kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi -American George Floyd mwezi uliopita.

Kampeni za Trump za kuwania kuchaguliwa tena kama rais wa Marekani zilikua ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu katika eneo lililofungwa kuwahi kushuhudiwa tangu Marekani ilipotangaza mlipuko wa Covid-19, na unafanyika wakati Oklahoma ikishuhudia ongezeko la visa vya corona vilivyothibitishwa.

Zaidi ya wagonjwa milioni 22 wa Covid-19 na vifo 119,000 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa nchini Marekani, kwa mujibu wa data kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Trump alisema nini?

Katika hotuba yake ya ufunguzi , Bwana Trump alisema kuwa kumekua na "watu wabaya sana nje, wanafanya vitu vibaya sana", lakini hakufafanua zaidi. Wanaharakati wa Black Lives Matter walikua ni miongoni mwa waandamanaji waliokua wamekusanyioka nje ya uwanja wa kampeni ya Trump kupinga mkutano huo kabla kampeni hazijaanza.

Kuhusu virusi vya corona, Bwana Trump aliwatia moyo maafisa kupunguza kasi ya kupima virusi kwasababu ilisababisha kugunduliwa kwa watu wengi wenye virusi.