Juneteenth: Je haya ni maadhimisho gani na yanahusiana vipi na kampeni ya Black Lives Matter?

Iliyochapishwa

Juneteenth ni moja ya sherehe ya miaka mingi nchini Marekani ya kukumbuka mwisho wa zaidi karne mbili za utumwa nchini humo.

Imekuwa ikisherehekewa tarehe 19 Juni tangu mwaka 1866 na mashirika ya haki za kiraia nchini Marekani kama vile National Association for the Advancement of Coloured People (NAACP) mara nyingi yamekua yakipigania kuifanya Juneteenth siku rasmi ya kitaifa.

Hilo bado halijafikiwa, lakini maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na uamuzi tata wa rais Trump mwaka huu inamaanisha kampeni hiyo sasa hivi iko kiwango cha juu kuwahi kushuhidiwa hapo kabla.

Juneteenth ni nini hasa?

Jina hilo limetokana na kuunganishwa kwa maneno 'June' na 'nineteenth' na ilikuwa ni tarehe ambayo utumwa hatimae ulionekana kumalizika nchini Marekani. Pia inafahamika kama Siku ya Kuachiliwa huru na Siku ya Uhuru.

Rais Abraham Lincoln alikuwa ametoa tangazo rasmi la umma la uhuru - ambalo liliwaachilia huru rasmi watumwa - mapema zaidi ya miaka miwili. Lakini ilichukua muda, na mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kabla ya kila mmoja kutambua mwisho wa utumwa.

Texas ilikuwa ni moja wapo ya majimbo ya shirikisho - kikundi cha utumwa - kilichoyasaidia majimbo yaliyopigana dhidi ya Muungano katika vita vya kiraia.

Lilikuwa ni jimbo la mwisho kukubali kushindwa na Jeshi la Muungano, na la mwisho ambako Watumwa weusi wa Marekani walitambua juu ya uhuru wao.

Ilipofika wakati wa Mkuu wa Muungano Gordon Granger alisoma waraka katika jiji la Galveston, vita vilikua vimeisha na Lincoln alikua ameuawa na waliopendelea Shirikisho katika ukumbi wa michezo.

Kwanini Juneteenth sio sherehe ya kitaifa?

Kwa sasa majimbo 46 kati 50 yanatambua au kusherehekea rasmi Juneteenth. Lakini tarehe hiyo sio siku ya mapumziko ya shirikisho, licha ya wanaharakati wa haki za kiraia kupigania itangazwe kama siku kuu ya kitaifa.

Katika siku chache zilizopita mashirika kadhaa yakiwemo Apple, Nike na Twitter -yametangaza kuwa yatatambua siku hiyo kama ya mapumziko na watawalipa wafanyakazi wao kuanzia sasa.

Pia katika orodha hiyo ipo bodi ya utawala ya mpira wa miguu ya Marekani, National Football League.

NFL imekua ikikosolewa miaka michache iliyopita ya nyuma kwa kumtenga mchezaji wa zamani wa San Francisco mwenye umri wa miaka 49 Colin Kaepernick, ambaye alipiga "goti maarufu" wakati wa wimbo wa taifa kama ishara ya kuunga mkono vuguvugu la Black Lives Matter.

Nikola Hannah-Jones, mwandishi wa habari wa New York Times na mwandishi wa msururuwa makala ya historia ya utumwa nchini Marekani, ni moja ya sauti zinazotoa wito wa taifa kuidhinisha siku ya Juneteenth.

" Kwamba Marekani haipaswi kuathimisha siku ya Emancipation Day ya kukomesha taasisi ya uhuru wetu halisi wa kuongea juu ya njama zinazoendelea za kuficha na kutokua kwetu na uwezo, bado, kutambua kile tulichokifanya na sisi ni akina nani. Juneteenth inapaswa kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa "alituma kwenye ujumbe wake wa twitter tarehe 11 Juni

Ni vipi Trump aliibua utata juu ya Juneteenth?

Ingawa kulikua na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi, tarehe 11 Juni, huku idadi kubwa ya watu wakiandamana katika miji ya Marekani, rais Trump alitangaza kuwa ataendelea na kampeni , ya kwanza tangu alipositisha kampeni hizo mwezi Machi kutokana na masharti ya coronavirus . katika jiji la Tulsa tarehe 19 Juni.

Licha ya tarehe yenyewe, chaguo la Trump la eneo pia lilizua hasira kwani Tulsa ni eneo ambako yalifanyika mauaji mabaya ya watu weusi katika historia ya Marekani , mwaka 1921.

Trump alibadilisha mawazo yake siku chache baadae na kuhamshia mkutano wake wa kampeni tarehe 20- Juni. Alisema kuwa tarehe haikuwa imechaguliwa kwa makusudi kwa ajili ya mkutano na kwamba wataahirisha tukio hilo "kwa ajili ya kuheshimu siku hii ya mapumzik".

Lakini Tulsa limesalia kuwa ndio eneo la mkutabo - ni mojawapo ya miji mikubwa zaidi ya Oklahoma, jimbo ambalo Trump alishinda zaidi ya 65% ya kura katika uchguzi wa mwaka 2016.

Je Juneteenth inahusiana vipi na vuguvugu la Black Lives Matter ?

Wanaharakati wamekua wakijishughulisha katika kushinikiza uelewa wa tarehe hiyo katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuandaa matukio ya kitaifa kunadi viguvugu la Black Lives.

Shinikizo hilo ni pamoja na kuweka mada za Juneteenth- za Black-ish, msururu wa vipindi vya vichekesho vinavyoonyesha maisha ya familia za Wamarekani weusi wa kipato cha kati na cha chini.

Kipindi hicho, kilichotangazwa kwa mara ya kwanza. Oktoba 2017 na kuonyeshwa tena mwaka huu, hutoa wito wa wazi wa kutambuliwa kwa Juneteenth kama siku rasmi ya kitaifa.

Maandamano yanayoendelea na kuongezeka kwa uelewa wa mfumo wa ubaguzi vimeifanya Juneteenth umuhimu mpya . Kuna matukio yaliyoandaliwa kote nchini Marekani siku ya Ijumaa na mwishoni mwa juma.

Je serikali ya Marekani ilishawahi kuomba msamaha kwa utumwa?

Rais Mdemocrat Bill Clinton aliomba msamaha kwa biashara ya utumwa wakati wa zaira yake barani Afrika mwaka 1998.

Miaka kumi baadae, Bunge la wawakilishi la Marekai lilitoa msamaha ambao pia ulijumuisha miongo yasheria za ubaguzi dhidi ya Wamarekani weusi.

Hatua hiyo ilifuatia mwaka baada ya Seneti ya Marekani.

Lakini kwa misamahahii mingi haifiki mbali. Kuna miito nchini Marekani ya kutaka malipo kwa vizazi vya watumwa, lakini suala hili limeleta mgawanyiko mkubwa kulihusu: katika kura ya maoni iliyofanyika mwaka jana , 74% ya Wamarekani weusi walionyesha kuunga mkono malipo hayo, huku 85% ya wazungu wakipinga hilo kufanyika.