Virusi vya corona: Trump amekatisha uhusiano wa Marekani na WHO

Donald Trump

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Trump amesema kuwa WHO ni "kibaraka wa China"
Iliyochapishwa

Trump akosolea pakubwa baada ya Marekani kukatiza uhusiano wake na WHO

Bwana Trump amekosolewa nyumbani na nje ya nchi baada ya Maekani kujiondoaa kama mshirika wa Shirika la Afya Duniani - WHO.

Umoja wa Ulaya umemsihi kufikiria tena uamuzi wake huku waziri wa afya wa Ujerumani akiitaja hatua hiyo kuwa ni wenye kukatisha tamaa kwa afya kimataifa.

Mkuu wa kamati ya afya ya bunge la seneti Marekani, ambaye ni wa Republican kama Trump amesema kuwa huu sio wakati wa kujiondoa kwenye shirika hilo.

Bwana Trump amesema WHO imeshindwa kuwajibisha China juu ya mlipuko wa virusi vya corona.

The WHO, shirika linalosaidia kuimarisha masuala ya afya na kukabiliana na milipuko ya magonjwa imekuwa ikikosolewa kila wakati na Rais huyo wa Marekani kutokana na jinsi ilivyo shughulikia janga la corona.

Trump speaks at the White House

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, RaisTrump ameshtumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China

Kuna maoni gani dhidi ya maamuzi yaTrump?

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa wahudumu wa afya na wanasiasa, wengi wakiwa wanahofia kuwa maamuzi ya Trump yanaweza kuharibu jitihada ambazo tayari dunia imezifanya kukabiliana na mlipuko huu.

Tayari, Umoja wa Ulaya umeandika maelezo ya pamoja ikimtaka rais Ursula von der Leyen na mkuu wa masuala ya kigeni bwana Josep Borrell, ambaye alitaka Marekani kufikiria tena maamuzi yake.

Inadaiwa kuwa ili WHO ipambane na mlipuko huo vilivyo, "inahitajika kila mmoja aunge mkono jitihada inazofanya na kusaidia kadri wanavyohitaji msaada ".

"Tumeiambia Marekani kufikiria mara mbili maamuzi yake," Taarifa hiyo ilieleza aliongeza.

Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn pia alikosoa uamuzi wa Marekani na kusema kuwa anarudisha nyuma jitihada za kimataifa.

Marekani kwenyewe, amekosolewa vikali na wapinzani wake wa kisiasa kwa hatua aliyoichukua.

Seneta wa Republican Lamar Alexander alisema hakubaliani na maamuzi ya rais kwa sababu bila Marekani kufadhili katika wakati huu mgumu wa kiafya suala la upatikanaji chanjo litakuwa gumu.

"Kiukweli kuna uhitaji wa kuangalia vizuri na kubaini kama kuna makosa Shirika la Afya Duniani lilifanya kuhusiana na virusi vya corona, lakini wakati wa kufanya ukaguzi huo wa makosa ya nyuma ni baada ya kutoka katika janga hili la corona na sio katikati ya janga," alisema seneta wa kamati ya afya nchini Marekani.

Mgombea wa zamani wa nafasi ya urais na seneta wa Marekani Elizabeth Warren ameandika katika kurasa yake ya tweeter: "Maamuzi ya rais Trump kuondoka WHO wakati wa mlipuko wa dunia inaathiri jitihada za ulimwengu na kushusha hadhi ya uongozi wetu na kutishia afya za raia wa Marekani."

Anders Nordstrom, kiongozi wa zamani wa WHO alisema amesikitishwa sana na kuongezeka kwa msukumo wa kisiasa katika wakati ambao tunahitaji mshikamano wa pamoja kama dunia.

Waziri wa afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize anasema kuwa maamuzi hayo ni "mabaya sana".

Wanachama wa WHO wamekubaliana kuwa Mei, 19 watafanya uchunguzi huru kuhusu janga hili.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha uhusiano wa Marekani na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Trump ameshutumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

"China ina mamlaka yote kwenye Shirika la Afya Duniani ," rais alisema hayo wakati akitangaza hatua ambazo zilipaswa kuchukuliwa dhidi ya China.

Marekani ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo la afya, lakini ufadhili huo kwa sasa utaenda kwenye mashirika mengine sasa, alisema.

Marekani ni mfadhili mkubwa ambaye alichangia zaidi ya dola milioni 400 kwa mwaka 2019.

Bwana Trump, ambaye anafanya kampeni za kuwania kuchaguliwa tena kuwa rais amekuwa akikosolewa kwa namna anavyokabiliana na mlipuko wa corona, na amekuwa akiilaumu China kwa kuficha taarifa za mlipuko huo wa virusi vya corona.

Zaidi ya watu 102,000 nchini Marekani wamepoteza maisha kutokana na Covid-19 na taifa hilo ndio limetajwa kuwa na takwimu kubwa zaidi ya vifo vilivyosababishwa na corona duniani kote.

Trump alisema nini?

"Leo tutasitisha uhusiano wetu na Shirika la Afya Duniani na kuhamisha ufadhili tunaotoa hadi kwenye mashirika mengine ya afya", Bwana Trump alisema akiwa White House katika bustani ya Rose.

"Dunia inahangaika sasa hivi kwa sababu ya makosa ya serikali ya China," alisema.

Aliongeza kuwa China imesababisha maisha ya Wamarekani zaidi ya 100,000 kupotea kutokana na mlipuko huo wa virusi.

Rais Trump ameishutumu China kwa kullipotosha shirika la afya duniani WHO kuhusu virusi.

WHO director-general Tedros Adhanom Ghebreyesus

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Dr Tedros ametetea WHO jinsi ilivyoshughulikia janga la corona

Siku ya Jumamosi, Umoja wa Ulaya ilifikia uwamuzi wa kuwapigia na kuonya mamlaka ya Trump kwa kuridhia maamuzi yao huku ikitoa angalizo kuwa maamuzi yake yataathiri jitihada za dunia katika kukabiliana na virusi vya corona.

Bwana Trump alitangaza mwezi mmoja uliopita kuwa itakata ufadhili ambao Marekani inatoa katika shirika la Afya duniani kama hakutakuwa na unafuu wowote wa ugonjwa wa corona kwa kipindi cha siku 30.

Mkurugenzi wa WHO bwana, Tedros Adhanom Ghebreyesus,alihaidi kuangalia tena namna nzuri ya kukabiliana na mlipuko wa corona kama chombo huru.

Marekani ndio mfadhili mkubwa wa WHO duniani, alitoa Zaidi ya dola milioni 400m kwa mwaka 2019, ambayo ni 15% ya bajeti yake yote.

Mataifa mengine yakiwemo Ujerumani na Uingereza yanasema hayana mpango wa kuondoa ufadhili wao WHO,ambayo inasaidia inaratibu harakati za kukabiliana na ugonjwa wa corona duniani.

Ufadhili gani WHO inapokea -na nani anafadhili?

Shirika la afya duniani lilianzishwa mwaka 1948 na makao yake makuu ni Geneva, Switzerland, ni shirika la Umoja wa Mataifa linalohusiana na masuala ya afya duniani.

Shirika hilo lina wanachama 194 na lengo lake kuu ni kuhamasisha masuala ya a fya, kulinda ulimwengu na kuhudumia wasiojiweza.

Inafanya kampeni za chanjo, huduma za dharura za afya na kuunga mkono huduma muhimu za afya

Huwa inapata ufadhili kutoka kwa wanachama kulingana na utajiri wan chi husika, idadi ya watu na kadri nchi inavyowiwa kuchangia.

Chanzo cha mazozo kati ya Marekani na WHO ni nini?

Bwana Trump aliikosoa WHO kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko wa corona mwezi uliopita na hivyo kutishia kuondoa moja kwa moja ufadhili wa Marekani katika shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa kwa sababu wameshindwa kutimiza wajibu wao.

"Ni wazi kuwa makosa yako na shirika lako kumegharimu sana dunia kwa jinsi lilivyokabiliana na mlipuko wa corona," aliandika barua kwa mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mei, 18.

Na baadae akaliita Shirika la WHO kuwa kibaraka wa China"

Bwana Trump ameikosoa China mara kadhaa kwa namna ilivyokabiliana na janga hili hapo awali.

Coronavirus
Maelezo ya video, Bwana Trump amekosoa China mara kadhaa kwa hatua zake awali katika kushughulikia mlipuko wa virusi vya corona

Aidha, China pia imeishutumu Marekani kwa kuhusika katika kusambaza virusi hivyo katika ardhi yake, na kudai kuwa 'wanasiasa wanaodanganya.'

Mapema mwezi huu, waziri wa mambo ya nje wa China Zhao Lijian alisema Bwana Trump alikuwa anajaribu kupotosha umma na kurushia kidole cha lawama China kwa madia ya kushindwa kuwajibika.

Nchi wanachama wa WHO wameamua kuwa huru katika namna ya kukabiliana na mlipuko huu.

WHO, Geneva

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Marekani imekuwa mchangiaji mkubwa wa WHO

Je WHO ilishindwa kuikabili China?

Rais Trump amelishutumu shirika la WHO kwa kushindwa kuhoji maelezo ya mwanzo ya Uchina iliposema hapakua na ushahidi wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu ya virusi vya corona.

China iliifahamisha kwa mara ya kwanza WHO kuhusu "homa ya mapafu ambayo chanzo chake hakifahamiki, tarehe 31 Disemba

Tarehe 5 Januarii, shirika hilo lilisema kuwa taarifa lilizokua nazo zilionyesha kuwa "hakuna ushahidi muhimu wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu''.

Na tarehe 14 Januari, shirika hilo lilituma ujumbe wake wa twitter kwamba uchunguzi wa awali wa Wachina umebaini kuwa "hakuna ushahidi wa wazi wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu" ya virusi.

Siku hiyo hiyo, hata hivyo , Tume ya afya ya Wuhan ilisema kuwa Wuhan ilisema uwezekano wa maambukizi ya binadamu na binadamu hauwezi kuondolewa, ingawa hatari ya kuhama kwa virusi kutoka kwa mnyama hadi binadamu ni ya kiwango cha chini.

Katika kipindi hicho hicho, taarifa nyingine za WHO zililiibua kuwepo kwa baadhi ya uwezekano wa maambukizi baina ya binadamu, ikiweleza kile kilichofahamika juu ya virusi vingine vya corona kama dalili ya ugonjwa mbaya wa mfumo wa kupumua (Sars).

Na Januari 22, WHO, kufuatia ziara fupi ya kikazi nchini Uchina , alitoa taarifa ya wazi zaidi iliyosema kwamba maambukizi ya binadamu kwa binadamu yapo Wuhan.

Pia unaweza kusoma: