Shambulio la simba la muacha mlinzi wa hifadhi na majeraha mabaya

A lion

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinzi huyo alishambuliwa na simaba wawili (si huyu aliye pichani)
Iliyochapishwa

Mhifadhi wa wanyama pori amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na simba wawili huko nchini Australia.

Siku ya Jumanne, mwanamke mwenye umri wa miaka 35, amejeruhiwa vibaya shingoni na usoni alipokuwa katika hifadhi ya Shoalhaven, ambayo ipo kilomita 150 (maili 90) kusini mwa Sydney.

Alishambuliwa wakati akiwa anafanya usafi , polisi wa New South Wales alieleza.

Hifadhi hiyo itasaidia polisi kufanya uchunguzi na kusaidia wafanyakazi wengine.

Mhudumu wa afya wa dharura alisema mwanamke huyo alikutwa amezirahi akiwa na majeraha kadhaa.

"Shambulio lilikuwa kubwa sana," alisema Faye Stockmen wa gari la dharura la New South Wales.

Aliongeza kuwa wanyama hao walifungiwa baada ya shambulio kubwa la kutisha.: "Tunapaswa kwenda kwenye sehemu ya simba."

Mwanamke huyo aliyejeruhiwa na simba alikimbizwa kupelekwa tu hospitali ya Sydney akiwa katika hali mbaya.

Hifadhi ya Shoalhaven ilikuwa imefungwa tangu Machi 25, kutokana na marufuku ya kuzuia watu kutoka nje kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Map

Mwaka 2014,mlinzi wa hifadhi ya wanyama alivutwa na mamba majini wakati akiwa anatoa maelekezo kwa wageni.

Ingawa alinusurika na kupata majeraha ya mikono tu.