Virusi vya corona: Makundi ya kidini yanayopinga hatua za kukabiliana na Covid-19

Chanzo cha picha, AFP
Nchini Chile, kingozi wa kanisa ya Kievanjeli aliaga dunia baada ya kujumuika katika mkusanyiko wa watu wengi.
Nchini Peru au Colombia, walishangaza makasisi kwa kujumuika pamoja kwa misingi ya Imani zao licha ya kwamba watu mikusanyiko imepigwa marufuku.
Na nchini Brazil au Marekani viongozi wengi wa kidini wa Kievanjilisti walichukulia mzaha tishio la virusi vya corona.
Kuanzia Kusini hadi Amerika Kaskazini makundi mbalimbali ya Kievanjelisti yalikuwa yanaongoza kati ya yale yanayokiuka hatua ya kutokaribiana kama njia ya kukabiliana na janga la corona ambalo linaendelea kusababisha maafa makubwa katika bara hilo.
Tabia hiyo imesababisha mgawanyiko katika jamii ya Waevanjelisti ambapo wengine wanaonya kuhusu hatari ya virusi vipya vya corona na kuamua kufanya ibada zao kwa njia za mtandao.
Lakini hali hiyo imesababisha dhehebu hilo kuangaziwa zaidi hasa kutokana na waumini wake wengi ambao wanawaunga mkono marais Donald Trump au rais wa Brazilian Jair Bolsonaro, ambao wanataka hali ya kawaida kurejelelewa licha ya kwamba janga la virusi vya corona linaendelea kuongezeka katika nchi zao.
Licha ya hayo kuna sababu zingine kwa baadhi ya makanisa kuanzia imani hadi kiuchumi ambazo wanahofia kuwa janga la corona huenda likapunguza umaarufu wake kuanzia kupunguza ustawi wao na pia michango ya sadaka wanazopokea kutoka kwa waumini wao, kulingana na wataalam.

Chanzo cha picha, AFP
Dhehebu la Waevanjelisti limekuwa sana miaka ya hivi karibu huko Amerika Kusini: ambapo mmoja kati ya watu ni muumini wa kanisa hilo (2017), kulingana na utafiti uliofanywa katika nchi 18.
Hilo pia limechangia ushawishi mkubwa katika ulingo wa kisiasa kwenye mijadala inayoghubika kanisa hilo katika masuala kama vile kupinga uavyaji mimba au kutambuliwa kwa haki za wapenzi wa jinsia moja.
Lakini makundi hayo yamekumbwa na mtihani mkubwa kwa janga hili la corona.
Nchini Argentina, mhubiri wa Kievanjelisti na seneta kutoka mtaa wa Mendoza alisababisha mjadala mkali wiki jana kwa kukosoa hatua ya kutokaribiana iliyowekwa na serikali ili kukabiliana na janga la corona.
"Vifo vingi bado vinatokana na uavyaji wa mimba kuliko ugonjwa wa Covi-19, kwa hiyo tungefungiwa ili watu wasitoe tena mimba," Héctor Bonarrico alisema hivyo kupitia mkutano wa wabunge na njia ya video na kudai kwamba makanisa ya Kievanjelisti yatapokea ruzuku.
Pendekezo lake lilileta mgawanyiko mkubwa na ulinganisho wao ukazua maswali mengi.
"Mungu ndio Mtoaji "
Nchini Brazil, ambapo virusi vya corona vinaendelea kuzua taharuki tayari vimesabaisha vifo vya zaidi ya watu 10,000 kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Rais Bolsonaro anakosolewa vikali kwa kupinga hatua ya kusalia ndani kama njia moja ya kupunguza maambukizi ya covid-19 na kuitambua kama "homa tu".
Hata hivyo Waevanjilisti wengi bado wanamuunga mkono rais Bolsonaro.

Chanzo cha picha, AFP
Kulingana na utafiti uliofanywa na kampuni ya Datafolha Aprili, waevanjilisti nchini Brazil walitathmini utawala wa rais kama wenye mtazamo chanya na pia wanapinga vikali kufungiwa ndani kuliko jamii nyengine yoyote ile nchini humo.
Viongozi wenye ushawishi wa Kievanjelisti kama Edir Macedo, kutoka Kanisa la Universal Church of the Kingdom of God, na Silas Malafaia, kutoka Assembly Church of God Victory in Christ, ndio wakosoaji wakubwa wa kuchukuliwa kwa hatua ya kujitenga na kutokaribiana nchini Brazil, mitanzamo inayoendana na Bolsonaro.
Katika makanisa mengine ya Kievanjelisti nchini Brazil, bado waumini wanahudhuria ibada licha ya hatua ya kutokaribiana kuchukuliwa ambapo waumini wanapewa vitakaza mkono mlangoni na waumini hadi 3,000 wanafanya ibada katika eneo hilo hilo ambalo wengine wapo kwenye karantini.
"Wanaamini kwamba Mungu ndio suluhisho kwa yote," amesema Mariz. "Kilichopo ni kwamba Mungu ndio mtoaji wa kila jambo na huna haja ya kujitenga."

Chanzo cha picha, AFP
Hali hii imesababisha waubiri wengine kuendesha ibada zao kwa njia ya mtandao.
"Lakini hao ni wale walio wachache," amesema mwanatheolojia Kenner Terra, ambaye anakosolewa vikali kwa kuunga mkono hatua ya kutokaribiana.
"Ukilinganisha na mapendekezo ya WHO, ni sawa na kusema kuwa yanakutana na upinzani mkubwa sana," Terra ameiambia BBC Brazil.
"Wito kutoka kwa Mungu"
Makanisa mbalimbali Amerika Kusini yamefungwa kwa muda kwa sababu ya jangala virusi vya corona na kugeukia mtandao ya kijamii kama njia ya kufanya ibada.
Lakini wengine bado wanapendelea mikusanyiko ya ana kwa ana.

Chanzo cha picha, AFP
Makundi ya Kievanjelisti huko Nicaragua yameshiriki shughuli nyingi kama kawaida, matukio mengine yaandaliwa na serikali ya Daniel Ortega. Hio limepata ukosoaji mkubwa nje ya nchi kwa kutochukua hatu za kukabiliana na Covid-19 kama inayopendekezwa na wataalamu wa afya.
Kutoka kwa kanisa Katoliki, Kadinali wa Nicaragua, Leopoldo Brenes alionya Jumapili kwamba kwenda nje ni kujiweka katika hatari.
Katika maeneo ya Colombia na Peru mbali na maeneo ya mjini, maafisa wa polisi wamekuwa wakiingilia kati na kusitisha mikutano inayoendelea ya waumini wa Kievanjilisti.
Nchini Chile kumeshuhudiwa visa ambapo wachungaji walioambukizwa ugonjwa wa Covid-19 wanaendesha ibada pamoja na waumini wao.
Mchi 16, Mario Salfate, mhubiri mmoja alihudhuria mkutano wa kidini na waumini karibia 300 wakati ambapo tayari hatua za kukabiliana na virusi vya corona zilizuwa zimeshachukuliwa.
Siku chache, Bwana Salfate alithibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 pamoja na washirika wengine watatu waliokuwa wamekusanyika hapo awali.
Bwana Salfate aliaga dunia katika ya Aprili.

Chanzo cha picha, AFP
Nchini Marekani mhubiri wa Kievanjelisti Gerald Glenn, aliaga dunia mwezi huohuo baada ya kukiuka onyo na tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona na kudai kuwa "Mungu ni Mkubwa" na kuwa ataendelea kuhubiri tu katika kanisa lake la Virginia.
Na licha ya hatua za Trump zinazokinzana hatua za kukabiliana na virusi vya corona, waumini wa Kievanjilisti watatu kati ya wanne walionyesha kumuungamkono Trump katika kura ya maoni iliyofanywa juu ya mlipuko wa maambukizi.
Mkurugenzi wa utafiti, Greg Smith kutoka kampuni ya utafiti ya Pew, alisema kwamba wengine walihoji kuwa hatua zilizochukuliwa dhidi ya janga hilo zinaminya uhuru wao huku wengine wakiunga mkono wito wa Bwana Trump wa kutaka kurejelelewa kwa shughuli za kawaida.

Chanzo cha picha, Getty Images
Asilimia kubwa ya raia wa Marekani ambao huudhuria ibada makanisani kwa sasa hivi wanapokea ibada zao kupitia Televisheni na mtandaoni, kulingana na kura ya maoni iliyofanywa na kampuni ya Pew mwishoni mwa Aprili.
Lakini baadhi ya wahubiri bado wanafanya mikutano mafano akiwa Rich Vera, aliyeongoza hafla iliyofanyika Florida Jumapili na kutaka waliohudhuria kukaa karibu na yeye: "Hapa hakuna virusi vya corona," alisema, bila ya uthibitisho wa kisayansi.
"Wito aliouweka Mungu ndani yangu ni kuhubiri injili, kuuekelea mikono wagonjwa ili wapone," Vera alijibu hivyo hivi karibuni baada ya BBC ikiwa inahakikisha kwamba hatua ya kutokaribiana kati ya waumini wake inatekelezwa. "Huo ndio wito wangu."












