Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Sheria za amri ya kutotoka nje zinavyowaathiri makahaba Afrika
Janga virusi vya corona umesababisha nchi mbali mbali duniani kulazimika kutangaza amri ya kutotoka nje ili kuzuwia maambukizi ya virusi ambavyo tayari vimesababisha vifo zaidi ya 2000 barani Afrika vilivyorekodiwa.
Wafanyabiashara wa ngono ni miongoni wa watu ambao kazi zao zimeathiriwa pakubwa kutokana na amri za kutotoka nje barani Afrika.
Mmoja wa wafanyabishara wa ngono nchini Nigeria ameimbia BBC jinsi virusi vya corona vimeathiri maisha yake.
Anaishi katika jimbo linalokaliwa zaidi na Waislamu la Kano, ambalo liko katika wiki ya nne ya ya amri ya kutotoka nje.
Hakuna hata mmoja anayeruhusiwa kuondoka nyumbani kwake, isipokua katika siku za Jumatatu na na Alhamisi kati ya saa nne asubuhi na saa kumi jioni kupata chakula.
Na licha ya kuwa katika mwezi mtukufu wa Ramadan, Waislamu hawajaruhusiwa kukusanyika kwa maombi au kwa chakula cha Iftar au Daku.
Aisha, ambalo sio jina lake halisi, anasema anahangaika kuishi kutokana na masharti
'' Nimejaribu kukuendelea na kufanya kazi , lakini haiwezekani kwasababu ya amri ya kukaa nyumbani, na kwasabu ya kipindi cha Ramadhani.
Anasema kila mmoja Kano ni Muislamu, kwahiyo haiwezekani kwasababu mchana wote wako nyumbani na familia zao na jioni wanataka kwenda kufungua na familia zao.
''Wengi wa wateja wetu ni wanaume waliooa, kwahiyo sio rahisi kwao kutoka nje.''
Sheria ya Kiislamu inayofahamika kama Sharia, ilianzishwa katika Jimbo la Kano mwaka 2000, na katika maeneo mengine ya Kaskazini mwa Nigeria.
Tangu wakati huo ukahaba, kamali na unywaji wa pombe vilipigwa marufuku katika jimbo la Kano.
Nchini Nigeria polisi ni wakali sana sana, kwasbabu kazi ya ngono hairuhusiwi, hasa Kaskazini mwa Nigeria: '' Kama ukipatikana unauza ngono, unaweza kukamatwana kufungwa jela. Tupo katika jimbo hili la Sharia", anasema Aisha.
Aisha anasema hajapokea aina yoyote ya malipo rasmi ya kijamii wakati huu wa amri ya kutotoka nje: ''Nchini Nigeria hakuna kabisa usaidizi wowote kwa makahaba...Hakuna''. alisisistiza Aisha na kuongeza kuwa : ''Msaada pekee ambao tumeupokea ni kutoka kwa NSWA - Shirikisho la Wafanyakazi wa ngono la Nigeria - kwasababu tumekua tukiweka pembeni pesa za akiba tunazopata kwa siku.''
Anasema wanalazimika kutafuta njia nyingine mbadala kupata mapato. '' Serikali hata haitaki kujua wafanyabiashara ya ngono wanavyoendelea hapa nchini Nigeria'', alilalamika Bi Aisha ambaye anasema pesa zake zote zimeisha na hana njia mbadala ya mapato.
Amri ya kutotoka nje imewaathiri makahaba Kenya
Biashara ya ngono pia imeonekana kupungua katika miji mikubwa nchini Kenya kufuatia kuweka kwa marufuku ya kutotoka nje ili kuzuwia maambukizi zaidi ya virusi.Serikali ya Kenya ilitangaza marufuku ya kutotembea je katika kaunti za Nairobi Mombasa, Kilifi na Kwale jambo lilisositisha biashara za ukahaba ambazo hufanyika zaidi kutoka kwenye mitaa ya miji hiyo.
Mwezi uliopita polisi katika mji wa pwani mwa Kenya walivamia nyumba za malazi na kuwakamata wafanyabiashara ngono takriban 30 na wateja wao kwa kukiuka sheria za kutosogeleana zilizowekwa kwa ajili ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.
Polisi ilisema kuwa makahaba hao watafikishwa mahakamani baada ya janga la corona kwa kukiuka maagizo ya kukaa nyumbani ili kupunguza kuenea kwa Covid-19.
Wengi miongoni mwa wafanyabiashara ya ngono hutegemea zaidi madereva wa malori wanaotumia barabara ya Nairobi-Mombasa kupata kipato chao cha siku. Amri ya 'kaa nyumbani 'imeathiri pakubwa mapato kutoka kwa wateja wao kutokana na kudhibitiwa kwa matembezi.
Kilio cha wafanyabiashara wa ngono Afrika Kusini.
Wafanyabiashara wa ngono kote nchini Afrika Kusini wameachwa bila mapato yoyote kutokana mlipuko wa virusi nvya corona jambo ambalo limewafanya wabaki bila chaguo bali kutegemnea ukarimu wa usamalia wema wa watu kuwawezesha kuishi, kulingana na vyombo mbali mbali vya habari nchini humo.
Serikali bado haijawapatia msaada wowote tangu ilipotangaza sheria ya kukaa nyumbani.
Raia wa Afrika kusini waliwaliamrishwa kukaa nyumbani kwatika kipindi cha wiki tatu, ambapo biashara zisizo muhimu zilifungwa na huduma muhimu pekee ndizo zilizoruhusiwa kuendelea kufanya kazi.
Katika taarifa ya pamoja, Sweat na Sisonke, vuguguvu la makahaba, lilielezea kuhofia kwamba ,uamuzi huo unawaathiri wafanyakazi wasio na ujuzi nchini humo, mkiwemo wafanyabiashara wa ngono.