Virusi vya corona: Jinsi amri ya kukaa nyumbani ilivyoibua mjadala kwa wafanyakazi wa ndani India

Wanawake wa India

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mwishoni mwa wiki, India iliongeza muda wa marufuku ya kutoka nje katika taifa zima kwa muda wa usiku kwa siku 40 nyingine lakini wafanyakazi wa ndani wanaweza kuwa wanarundi nyumbani kwao. Maamuzi hayo yamekuja kufuatia mjadala wa mamilioni ya watu wa daraja la kati kubishana kuhusu kama ni sawa kuwaruhusu wafanyakazi waje nyumbani kwao au la? Mwandishi wa BBC, Geeta Pandey mjini Delhi ameelezea utata kuhusu suala hilo.

Rafiki aliwahi kusema kuwa kama itambidi achague kati ya mume wake na mfanyakazi wake wa ndani angeweza kuchagua herufi.

Maoni hayo yalitolewa kama utani , lakini ni mfano wa namna gani India wanavyowategemea wafanyakazi wa ndani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, zaidi ya watu milioni nne wameajiriwa kama wafanyakazi wa ndani, mara nyingi wanalipwa kiasi kidogo cha fedha.

Taarifa ambazo si rasmi, zinadai wafanyakazi hao ni kubwa zaidi na wanaweza kufika milioni 50. Mbili ya tatu ya wafanyakazi hao ni wanawake.

Mahusiano ya wahudumu hao wa nyumbani na waajiriwa wao huwa yanategemea makubaliano yao- maisha yao huwa ya kimaskini zaidi wengi wakiwa wanakaa katika makazi ya watu maskini na wengine wametoka kijiji na wamekuja mjini kupata ajira ya kuendesha maisha yao.

Watu wa daraja la kati.

Huwa ni ajira ambazo kipato chake ni kidogo na watu ambao hawana taaluma yoyote ndio wanafanya ili waendeshe maisha yao.

Lakini kwa kipindi cha wiki sita zilizopita, mamilioni ya watu wa daraja ya kati wameweza kuendelea na maisha yao bila kutegemea wahudu wa ndani kuwafanyia kazi ya kupika, kulea watoto , kuendesha magari na kuangalia bustani baada ya India kuweka marufuku ya kutoka nje nchi nzima kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Tukianza kwa kukubali katazo hilo ambalo lilikuwa lichukue muda wa wiki tatu, Baadhi ya nyota wa Bollywood wameweka video kwenye mtandao wa Instagram zikiwaonyesha wakipika wenyewe na kuoosha vyombo pamoja na kufanya usafi wenyewe.

Coronavirus

Taarifa zaidi kuhus virusi vya corona:

Coronavirus

Lakini marufuku hiyo ya kutoka nje imeongezwa muda , mara mbili ya ule wa awali na wazo la kuwakumbuka wahudumu wa ndani likaibuka.

Mazungumzo yalikuwa yalikuwa ni namna gani wazee wanaweza kumudu kuishi wenyewe. Na vipi kuhusu wale watu ambao wana matatizo ya kiafya maisha bila kupata msaada.

Kuna msongo ambao wafanyakazi wa ndani wanakuwa hawana uchaguzi zaidi ya kurudi kazini.

"Wengi wamepoteza ajira zao na wengine wanasema kuwa wamekuwa hawapokei mshahara wakati huu wa marufuku ya kutoka," Mkuu wa taasisi ya Helper4U Meenakshi Gupta Jain, mtandao ambao unawajumuisha wafanyakazi wa nyumbani na waajiriwa aliiambia BBC.

Sonika Verma anasema wawili miongoni mwa dada zake hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi chote cha amri ya kukaa nyumbani.
Maelezo ya picha, Sonika Verma anasema wawili miongoni mwa dada zake hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi chote cha amri ya kukaa nyumbani.

Kwa mwezi uliopita namba ya Whatsapp ya kuomba msaada kuhusu Covid -19 walikuwa wanapata ujumbe mfupi kwa wahudumu wa ndani mara 10 mpaka 15, kila siku wahudumu wa ndani, madereva, wapishi walikuwa wanapiga simu kuomba msaada.

"Wanasema kuwa hawana fedha ya kujikimu . Sasa wafanyaje? Tunawezaje kuwalisha watoto wetu? Huwa tunawaelekeza katika asasi ya ya kusaidia wahitaji ya karibu walipo ili waweze kupata chakula," Gupta Jain alisema.

Sonika Verma, ni mfanyakazi wa majumbani mjini Delhi amerudi kazini siku ya Jumatatu, anajiona kuwa mwenye bahati kwa sababu waajiri wake walimlipa hata fedha za wakati yuko katika marufuku ya kutoka nje.

"Nilikuwa na msongo wa mawazo sana wiki hizi maana hata mume wangu pia alikuwa nyumbani , yeye ni dereva hivyo haendi kazini na mimi pia nilikuwa siruhusiwi kwenda kazini nilikuwa nawaza ntafanyaje kama nikipoeza kazi yangu pia," aliniambia.

Dada zake wanadai kuwa hawajalipwa hawajalipwa katika kipindi chote cha marufuku ya kutoka nje.

"Waajiri wao wamewalipa siku ambazo walifanya kazi tu mwezi Machi na hawajawalipa fedha yeyote kwa mwezi Aprili.

Na wamewaambia kuwa wataliwa pale tu watakaporejea kazini lakini hawajawapigia tena kwa ajili ya kuendelea na kazi na hawajapigiwa bado", alisema.

Sababu za kutokulipwa kwa dada zake na kutoitwa kurudi kazini.

Mjadala uliokuwepo ni je sawa kwa wahudumu hawa wa majumbani kuruhusiwa kwenda kazini au la?

Baadhi walisema kuwa , makatazo labda yameondolewa lakini corona bado ipo na kuruhusu watu kutoka nje na kuingia kwenye nyumba za watu wa daraja la kati kunaweza kusababisha maambukizi zaidi ya virusi vya corona katika maeneo ambayo tayari yalikuwa salama na corona.

Mwanamke wa India akitazama Televisheni

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini baadhi ya wakazi wanasema kuwa wazee wanahitaji msaada ni jambo ambalo linapaswa kutopuuzwa. Nyumba nyingi za India kwa watu wa kipato cha kati hazina mazingira rafiki kwa kuwa na sehemu za kuoshea vyombo , mashine za kufulia na hivyo kazi za nyumbani zinapelekea kuwa ngumu kwao.

.Anil Tiwari, rais wa posh ATS Greens , wanaojenga majengo mengi nchini India katika mji wa Delhi, alikuwa anawaza kuwaruhusu wafanyakazi wa ndani waende.

"Tuna gorofa 735 ambapo kuna wananchi wengi walio staafu na wanaishi wenyewe. Wengi wao hukumbwa na matatizo mengi. Kwa hiyo inatubidi tuchukue hatua.."

Miongoni mwao ni Bregadia (mstaafu) Kuldeep Singh Chokkar ambaye anaelezea jinsi hali ilivyo ya shida sana.

Ana miaka 80 , ni mgonjwa aliepona kansa, anaishi pia na mke wake wa miaka 75, ambae nae ana magonjwa yanayo mkabili.

" Kama tungekuwa vijana , tungeweza kuhimili , Ila tunakumbana na changamoto nyingi kwenye kutunza nyumba zetu", Alizungumza hayo kwenye simu.

Mpaka wakati wa marufuku ya kutoka nje,Bregadia Chokkar alikuwa na msaidizi ambae alikuwa akimlipa kwa masaa, msaidizi huyu alikuwa akitunza bustani na kusafisha gari, ambapo alikuwa ni wakuja na kuondoka kila siku.

Nilimuuliza kama anamatarajio ya msaidizi kurudi, Alijibu" hakika kurudi kwake kutarahisisha maisha yetu".

Jirani yangu ni mwalimu mstaafu , Pinki Bhatia , ana wasiwasi kidogo kuhusiana na kutaka mtu aje kwake ili kumsaidia na kazi kwa kipindi hiki, yeye huwa anamatatizo ya mgongo ila anajitahidi na kufanya kazi zote mwenyewe bila ya msaada wowote.

Maelezo ya video, Virusi vya corona:Vidokezo tano ya jinsi ya kuimarisha afya yako ya kiakili

Ila hakuna namna tumekuwa tukifanya kazi zote wenyewe Kama, kupika ,kufagia, kufua, na kuosha vyombo.

Bi. Bhatia, anaumri wa miaka kati ya miaka 60, na mume wake anamiaka zaidi ya 70, anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na matatizo moyo.

Serikali imetoa ushauri kwenye maambukizi ya virusi vya Corona ,imesema kuwa watu wenye umri zaidi ya miaka 60 wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi na hawatakiwi kutoka nje, kwa hiyo wanandoa hao wamelazimika kukaa nyumbani kwao kwa wiki sita mpka Sasa .

Bi. Bhatia alisema" jirani yao ni dereva ndie anae wasaidia kwa kuwaletea maziwa na mahitaji yote kutoka sokoni",

Bi. Bhatia alisema kuwa bado hajaamua kuhusu kurudi kazini au kutorudi kazini".

" Watoto wangu wanaishi Mumbai na Switzerland, Niliwapigia na kuwauliza tufanya nini? " Wakajibu tusubiri wiki inayo kuja na tuone hali itakavyokuwa . Kwa hiyo tunasubiri wiki inayo ", alisema.

Bi. Gupta Jain alisema "kwanini wakusanyaji na wasambazaji wa mboga wanaruhusiwa ila kwanini wasaidizi wa ndani na madereva hawaruhusiwi ?

" Unawapa Barakoa na vitakasa mikono na nguo ambazo watazivaa wakiwa nyumbani kwako na utachukuwa tahadhari zote", ni muda wakuwa ruhusu warudi kwenye kazi zao.