Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Rais alitangaza naugua Covid-19 kwenye TV
Kuwa na joto jingi, kuhisi kuchefu chefu na kikohozi kikavu kinachoogopewa.
Sita Tyasutami alionesha dalili zote za mgonjwa wa corona. lakini amekuwa akilala katika kitanda cha hospitali mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, na hali yake haijatibiwa. Hata mama yake, Maria Darmaningsih, ambaye amelazwa katika hospitali hiyo pia hajapewa matibabu.
Wakiwa wamezuliwa katika vyumba tofauti, Tyasutami na mama yake wamekuwa wakisubiri matokeo ya vipimo vya corona,, wakati ambapo rais wa Indonesia alito atangazo la kushangaza kuwahusu
Katika hotuba yake kwa taifa, rais Joko Widodo alisema raia wawili wa Indonesia wamepatikana na ugonjwa wa Covid-19, na kuongeza kuwa ndio visa viwili vya kwanza vya corona kuthibitishwa nchini humo.
Wawili hao alisema ni mwanamke wa miaka 64- na binti yake wa miaka 31 - ambao wanapokea matibabu katika hospitali ya magonjwa ya kuambukiza mjini Jakarta, rais alisema.
Hotuba hiyo iliyotolewa moja kwa moja kutoka ikulu ya rais ilithibitisha kuwa ugonjwa wa corona kwa kweli imefika Indonesia.
Tangazo la rais liliwaacha Tyasutami na mama yake kwa mshangao. Je rais Widodo alikuwa anawazungumzia wao?
Japo katika tangazo hilo rais hakutaja majina ya wagonjwa Tyasutami, alihisi hakuwa na sababu ya kufikiria vingine kwasababu maelezo yaliyotolewa kuwahusu wagonjwa hao wawili yalishabihiana na wao.
Moja kwa moja, Tyasutami alimuuliza muuguzi ikiwa hospitali hiyo inawatibu wagonjwa wengine wa corona. Muuguzi alipomjibu la, alifahamu fika wagonjwa waliotajwa na rais katika tangazo lake ni yeye na mama yake.
"Nilichanganyikiwa, Nilikasiriaka, Nilisikitika sana," Tyasutami aliiambia BBC. "Sikujua nifanye nini kwasababu taarifa hizo zilikuwa katika vyombo vyote vya habari."
Kabla ya kupatikana na ugonjwa, Tyasutami alikuwa mcheza densi, msimamizi wa sanaa ya kuigiza, dada, binti na rafiki.
Lakini baada ya hapo mataji yote hayo yalibadilika kuwa jina moja: ''kisa cha kwanza''.
Rekodi yake ya afya ilivujishwa. Maelezo ya hali yake ikapotoshwa. Uvumi na uongo ukaanza kusambaa mitandaoni.
Chini ya lisali moja, aligeuka kuwa sura ya mlipuko wa corona nchini Indonesia.
Ilianza na koo kuwasha.
Tyasutami alipuuza. Kwani haikuwa kitu cha kutia hofu, alidhania. Kisha, asubuhi ya Februari 17, aliamka na dalili ambazo zitageuka kuwa maradhi yatakayobadilisha maisha yake.
Mama yake Darmaningsih, mkufunzi wa densi katika taasisi ya sanaa ya Jakarta (JIA), alikuwa mgonjwa baada ya wiki moja.
Hali ya Darmaningsih ili kuwa mbaya zaidi baada ya tamasha la densi la Februari 23, hali iliyomfanya kuwa "mgonjwa sana".
Kufikia hapo, Darmaningsih na Tyasutami walienda kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika hospitali ya Depok, viungani mwa mji wa Jakarta.
Awali walipofanyiwa uchunguzi Darmaningsih alipatikana alipatikana na typhus - ugonjwa wa bakteria unaosambazwa na chawa au nzi - naye Tyasutami akapatikana na homa ya mapafu.
"Tuliomba kufanyiwa vipimo vya Covid-19, lakini ombi letu lilikataliwa, wakati huoa, kwasababu hospitali haikuwa na vifaa maalum vya kufanya vipimo hivyo," Tyasutami alisema.
Mnamo Februari 27, walilazwa hospitali, wasijue virusi hivyo vilikuwa vimeanza kuwashambulia.
Ilichukua saa 24 kabla adokezewe na rafiki yake Tyasutami aliyekuwa pamoja naye katika tamasha la densi kwamba walitangamana na mgonjwa wa corona.
Rafiki yake alimfahamisha kuwa mwanamke kutoka Japan aliyehudhuria hafla hiyo amethibitishwa kuwa na virusi vya corona vinavyosababisha maradhi ya Covid-19.
Tyasutami hakumjua mwanamke huyo wa Kijapani, lakini alifahamu hatari ya kutangamana nae .
"Hiyo ndio sababu ilinifanya nimsisitizie daktari kwa mara nyingine kutufanyia vipimo vya kubaini kama tumeambukizwa virusi vya corona," Tyasutami alisema.
Madaktari walipokubali ombi lao, yeye na mama yake walihamishiwa hospitali ya Sulianti Saroso, Jakarta ambako walifanyiwa vipimo vya Covid-19.
Tyasutami na Darmaningsih walitarajia daktari atawafahamisha matokeo ya uchunguzi. Lakini matokeo hayo yalitangazwa na rais Widodo Machi tarehe 2.
Walishangzwa sana na hatua hiyo kwasababu yalitolewa kwa umma kabla ya wao kufahamishwa .
Siku kadhaa zilipita kabla ya Tyasutami na Darmaningsih waliambiwa kuhusu hali yao ya afya, na kufahamishwa kwamba katika mazingira ya mlipuko wa ugonjwa rais lazima afahamishwe kwanza kabla ya mgonjwa, kulingana na sheria.
Achmad Yurianto, msemeji wa serikali ya Indonesia, aliiambia BBC kuwa hakuna ubaya wowowte rais kutangaza hadharani hali ya mtu ya afya.
Sheria ya afya ya mwaka 2009 inasema faragha ya mgonjwa haizingatiwi wakati anachougua kunaangaziwa kwa maslahi ya umma.
Kwa hivyo, tangazo la rais lilikuwa sawa, kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya sheria mjini Jakarta, Bivitri Susanti.
Ilikuwa kitu kizuri kufanya, lakini, sheria inalinda rekodi ya afya ya mgonjwa? "Sidhani hilo linafanyika," alisema Bi. Susanti.
Katika kipindi cha saa chache ujumbe unaoonesha majini, mahali anakotoka na rekodi ya matibabu ya mgonjwa wa kwanza (Tyasutami) na mgonjwa wa pili (Darmaningsih) ilivujishwa na kusambazwa katika mtandao wa WhatsApp.
Mjadala wa ikiwa ni sawa au sio sawa, kutangaza kwa taifa hali ya mgonjwa wa kwanza na mgonjwa wa pili unaendelea kupamba moto nchini Indonesia.