Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Watu 24 wapatikana na maambukizi ya corona kwa siku moja Kenya
Kenya imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya corona kwa siku moja , kuwahi kushuhudiwa tangu kisa cha kwanza cha maambukizi hayo kilipotangazwa tarehe 12 Machi
Akitangaza upatikana kwa visa vipya 24 vya maambukizi ya corona Katibu mkuu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi amesema watu hao wamepatikana na Covid-19 kufuatia upimaji wa sampuli 1,195 katika kipindi cha saa 24.
Dokta Mwangangi amesema kuwa saba kati ya visa hivi vipya vilipatikana katika kitongoji cha jiji la Nairobi cha Kawangware kinachokaliwa na idadi kubwa ya watu. Idadi ya visa vipya vya maambukizi iliyopatikana kwa ujumla jijini Nairobi imefikia 20.
Amesema 10 kati ya visa vipya vimepatikana katika eneo la Eastleigh jijini Nairobi huku watano wakitoka Mombasa na wawili kutoka Kuria West katika kaunti ya Migori.
Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Afria ametangaza pia kwamba mtu mmoja zaidi amekufa kutokana na virusi hivyo , na hivyo kuifanya jumla ya idadi ya vifo vya corona Kenya kufikia watu 22.
Wizara hiyo pia imeripoti kuwa watu wawili zaidi wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kukutwa bila virusi, na hivyo kuongeza idadi ya watu waliopona kufikia 152.
Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta za kukabiliana na janga la corona.
1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona
2. Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19
3. Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.
4. Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitafaidi kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kusaidia familia zisizojiweza
5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.
6. Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wanasaidiana kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu
7.Afisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.
Awali Bwana Kenyatta alisema , kwa mujibu wa agizo la kuepuka maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, watu waepuke maeneo yenye umati wa watu, agizo lake likisema watu :
- waepuke mikusanyiko ikiwemo maeneo ya kuabudu
- wapunguze mikusanyiko ya kijamii mkiwemo harusi na mazishi, na masharti hayo yazingatiwe mara moja na wanafamilia
- waepuke maeneo yenye msongamano wa watu mkiwemo maduka ya jumla na maeneo ya burudani
- wapunguze mikusanyiko katika maeneo ya usafiri wa umma na kwingineko iwezekanavyo.
- Kuwepo ukomo wa wageni wanaotembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali za umma na za kibinafsi.