Virusi vya corona Ecuador: Wakati familia zinatafuta wapendwa wao mwanamke apatikana akiwa hai

Family members embrace amidst the health crisis caused by Covid-19

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Guayaquil, mji mkuu wa Ecuador umeathirika vibaya na ugonjwa wa Covid-19
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Ecuador, taifa dogo ambalo limeathirika vibaya na Covid-19, hospitali hakuangaliliki na familia zinahitajika kutafuta miili ya jamaa wao waliokufa.

Lakini taifa hilo la Amerika Kusini linaloendelea kupokea habari mbaya kila upande, mwanamke mmoja ametangazwa amekufa, amepatikana akiwa hai taarifa ambayo imegonga vichwa vya habari nchini humo.

Familia ya Alba Maruri, 74, ilifahamishwa mwezi jana kwamba jamaa huyo amekufa nakutumiwa majivu ya mpendwa wao baada ya mwili wake kuchomwa.

Lakini Maruri alipata fahamu baada ya kuwa katika hali ya kutojijua kabisa kwa wiki tatu hospitali na kumuomba daktari ampigie simu dada yake.

Miili isiyojulikana ilipo

Alba Maruri alilazwa hospitalini katika mji wa Guayaquil, kitovu cha mlipuko wa Covid-19 huko Ecuador.

Hapo, mamlaka tayari ilikuwa inapitia kipindi kigumu kukusanya miili ya waliokufa nyumbani.

Bertha and her family
Maelezo ya picha, Bertha Salinas bado anasubiri kufahamishwa kilichotokea kwa dada na shemeji yake

Nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni 17 ambayo ni kidogo kuliko majirani zao, Ecuador imeathirika vibaya na Covid-19 ikiweka rekodi ya watu zaidi ya 22,000 waliopata maambukizi huku wengine karibia 600 wakiaga dunia.

Inés Salinas na mume wake Filadelfio wote walikufa Machi 30.

Familia hiyo ilizungumza na BBC Mundo na kusema walilazimika kusubiri kwa siku nne kabla ya mamlaka kuwasili nyubani kwao na kuchukua miili hiyo.

Walikuwa wamefunga miili hiyo kwa karatasi ya plastiki wakati wanasubiri, anasema Bertha, dada yake Inés'. Lakini sasa anataka kujua nini kilichotokea baada ya miili hiyo kuchukuliwa kutoka nyumbani.

"Tuliambiwa kwamba tusubiri na kuwa watazikwa muda wowote ule na mamlaka," anasema.

Lakini tangu wakati huo mamlaka haijawahi kuwasiliana nao.

"Hata nimewasilisha malalamiko rasmi. Hatujui cha kufanya."

Mfumo wa afya ulioporomoka

Relatives of deceased people queue outside a cemetery in Guayaquil, April 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi ya vifo iliyoongezeka katika mji wa Guayaquil kumeathiri vibaya mfumo wa afya

Tatizo la Salinas sio jambo geni: makumi ya watu wanajitahidi kuwasiliana na hospitali, wanatembelea vyumba vya kuhifadhia maiti na kuwasiliana na polisi wakati wanapoendelea kutafuta miili ya wapendwa wao.

Idadi kubwa ya vifo katika mji wa Guayaquil imesababisha kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya tangu mwezi Machi.

Hospitali zilipeleka miili ya waliokufa kwenye makazi maalum inapohifadhiwa.

Familia zinahitajika kutembelea nyumba hizo maalum kutafuta wapendwa wao.

Baadhi ya raia wanatembelea sehemu hizo usiku na mchana.

Darío Figueroa ni mmoja ya jamaa waliofanikiwa kupaata mwili wa mama yao, Santa Marianita Barzola Martillo.

Mwili huo ulikuwa kando na miili mingine mingi iliyorundikwa.

A woman outside a hospital in Guayaquil

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jamaa wakiwasiliana na hospitali, vyumba vya kuhifadhia maiti na polisi kutafuta wapendwa wao

Ameiambia BBC Mundo: "Tulikuwa tumesubiri kwa siku kadhaa hospitali na tukaamua kuanza kufuatilia kwa karibu. Tukaamua kwenda kwenye maeneo ambao miili zinahifadhiwa tukiwa wengi na tukafanikiwa kushawishi walinzi na kuturuhusu kuingia ndani ili kujitafutia wenyewe mwili wetu.

"Tulijifunika makaratasi vichwani wengine wakaleta barakoa na glavu. Harufu mbaya ilikuwa imetanda kila sehemu. Ilichukiza sana kuona vile miili ilivyorundikana pamoja mmoja baada ya mwengine ikiwa imevishwa mifuko ya plastiki."

''Maajabu'

Katika ya hali ya sintofahamu, watu wengi huko Ecuador walishtushwa na taarifa za Bi. Maruri hakuwa miongoni mwa wafu waliokufa kwa Covid-19 kama ilivyosemekana awali.

Familia yake ilikuwa na furaha kupindukia lakini bado haikufahamika jivu walilopewa na kulihifadhi nyumbani kwao lilikuwa ni la nani.

Machi 27, familia hiyo iliarifiwa kwamba Bi. Maruri amekufa baada ya kulazwa hospitalini akiwa na kiwango cha juu cha joto na matatizo ya kupumua.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Walioneshwa jeneza hospitalini lakini wakalazimika kusimama mbali ili kuchukua tahadhari kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa corona.

"Niliogopa kuona uso wake," Mpwa wa Maruri, Jaime Morla, ameliambia shirika la AFP. "Nilikuwa umbali wa mita moja unusu. Alikuwa na nywele zilezile na ngozi yake vilevile."

Mwili wake ulichukuliwa na kuchomwa na familia ikapewa majivu.

Kiuhalisia, Bwana Maruri alikuwa amepoteza fahamu na kuamka wiki tatu badae na kuanza kumuulizia dada yake.

"Hii ni miujiza. Kwa karibia mwezi mzima tulidhania amekufa," amesema dada yake, Aura. "Na sasa hivi tumehifadhi majivu ya mtu mwengine kwetu nyumbani."

Coronavirus

'Sina wa Kumlilia'

Guayaquil
Maelezo ya picha, Katika mji wa Guayaquil, vitu binafsi vya waliokufa kama magodoro vinachomwa

Hospitali imeomba msamaha kwa mchanganyiko huo.

Familia hiyo inasema inataka mamlaka kuwafidia na kuwarejeshea pesa walizotumia kugharamia mwili wao kuchomwa.

Bi. Maruri pia amenunuliwa godoro jipya kwasababu familia yake ilikuwa imetupa lile godoro lake la kitambo.

Lakini wakati familia ya Maruri ikiwa imepata faraja hasa baada ya kumpata jamaa wao akiwa hai, kuna familia nyengine nyingi zinazoendelea kutafuta miili ya wapendwa wao.

Entrance of the IESS Hospital Los Ceibos in Guayaquil, Ecuador, on April 13, 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Hospitali zimebadilika na kuwa vurugu tupu na kushindwa kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19

Kwasababu ya ghasia zinazotokea na hofu ya kupata maambukizi, familia haziwezi kuaga miili ya wapendwa wao.

Mercedes, dada yake mdogo Salinas, anasema familia yake ilishirikiana kupata mahala pa kuzika wazazi wake.

"Lakini je tutafanyaje ikiwa hawatatup miili ya wapendwa wetu?," anasema.

"Ni jambo la kuhuzunisha sana kutofahamu pale walipo mama yangu na baba yangu. Ni jambo baya sana kutokuwa na mahala pa kukimbilia."