Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Mgogoro kuhusu amri ya kutotoka nje Malawi na mipango ya kuwalipa raia fedha
Malawi lilikuwa taifa la mwisho duniani kutangaza , mgonjwa wa kwanza wa Covid-19. Lakini tangu wakati huo , kumekuwa na kutoeleweka kwa katiba kuhusu uamuzi wa serikali kutaka kuweka marufuku ya watu kutotoka nje ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mahakama kuu ilichukua hatua ambayo haikutarajiwa kwa kuzuia mipango ya serikali kuchukua hatua hiyo ya marufuku mpaka jitihada muhimu zifanyike kusaidia wale ambao wameathirika zaidi.
Kwa sasa rais Peter Mutharika ametangaza hali ya dharura kwa kuwapa fedha watu ambao hawajiwezi kujikimu , katika taifa hilo ambalo ni miongoni mwa mataifa maskini zaidi duniani.
Serikali imelenga kufikia kaya 172,000 ambazo zitapokea malipo ya mwezi yanayokaribia kiasi cha dola hamsini kupitia simu zao za mkononi.
Kwa nini marufuku ya kutoka nje iliwekewa zuio?
Aprili,15 serikali ilitangaza marufuku ya watu kutoka nje ya muda wa siku 21, na ilitarajiwa kuanza siku tatu zilizopita lakini wafanya kampeni walilalamikia kuwa serikali ilikuwa imeamua kuweka uamuzi huo bila kuweka usaidizi wowote kwa wahitaji.
Asasi ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Defenders Coalition (HRDC) ilienda mahakamani kuhoji maamuzi hayo na mahakama kuamua kuweka katazo la marufuku hiyo isianze.
"Wakati tukiheshimu utaratibu ambao sekta ya afya umeweka kuhusu marufuku ya kutoka nje, tunataka marufuku ya kutoka nje kufuata utaratibu wote huo... sheria zifuatwe na haki za watu ambao wana mapato ya chini zifuatwe ili wasipate tabu wakati huu," alisema mwanaharakati wa kujitegemea wa haki za binadamu Victor Mhango kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Pamoja na HRDC, wafanyabiashara wa Blantyre na Mzuzu walifanya maandamano baada ya mpango wa watu kutozungukazunguka kutangazwa.
Wafanyabiashara waliwasha moto na polisi waliwasambaratisha. Wafanyabiashara wadogo walisema kuwa hawataweza kuhudumia familia zao kama watafungiwa wasitoke nje.
Makundi ya dini nayo yalisema kuwa kufungiwa ni kukiukwa kwa uhuru wa kuabudu.
Je mahakama zilisemaje?
Ijumaa, April,17 ilikuwa ni siku ambayo marufuku ya kutoka nje ilitarajiwa kuanza, nayo amri ya mahakama ikatolewa kuchelewesha uamuzi huyo kwa muda wa siku saba wakati mahakama ikiskiliza madai dhidi ya uamuzi huo.
Kufuatia uhakiki wa mahakama, jaji wa mahakama kuu aliongeza muda mwingine wa siku tano kuzuia marufuku hiyo isianze.
Siku ya Jumanne , Jaji aliamua kuwa kesi hiyo ipelekwe kwa mahakama ya katiba kwa sababu inahitaji ufafanuzi zaidi wa kikatiba.
Nini ambacho kilipendekezwa katika amri ya kutotoka nje?
Isipokuwa kwa maafisa wa utekelezaji wa sheria na watoaji wa bidhaa na huduma muhimu, ila watu wengine wote wangehitaji kupata ruhusa ya kutoka katika nyumba zao.
Watoa huduma muhimu na bidhaa watahitaji kuwa na kibali maalumu.
Soko kuu litafungwa na masoko mengine yatakuwa yanaruhusiwa kufunguliwa saa kumi na moja mpaka 12 jioni katika saa za nchi hiyo.
Je, kutolewa kwa fedha kuna maanisha kuwa amri ya marufuku nje itapitishwa?
Hapana.
Mahakama ya katiba bado inapaswa kusikiliza kesi hiyo na tarehe ya kuisikiliza kesi hiyo haijapangwa bado.
Kwa muda , watu bado wanaenda kwenye biashara zao kama kawaida - masoko yamefunguliwa na miji au mjini bado kuna watu wengi.
Lakini mwandishi wa habari Peter Jegwa kutoka mji mkuu wa Lilongwe, alisema kuwa kuna mabadiliko katika tabia za watu , ambapo kila nje ya duka au soko utakuta ndoo ya maji na sabuni au 'sanitisers'.
Ingawa , kampeni za uchaguzi zilizokuwa zitarajiwa kuanza kwa ajili ya uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika Julai 2, zimekatazwa.
Mkusanyiko wa watu zaidi ya 100, umekatazwa hata kabla ya marufuku ya kutoka nje haijatangazwa.
Je, serikali ina uwezo wa kulipa watu fedha?
Haiko wazi.
Ufadhili wa dola milioni 37 ambao umetolewa na World Bank kuisaidia Malawi kukabiliana na virusi vya corona. lakini fedha hizo huenda zikasimamia gharama hiyo. Iwapo kaya 172,000 zitapatiwa $50 kila moja jumla iyakuwa $8.6m kwa mwezi.
Rais hajasema bado kiasi hicho cha fedha kitaendelea kutolewa kwa muda gani?
Watu wamebaki njia panda kuamini mahakama au serikali.
Mapema mwaka huu, mahakama za Malawi zilichukua hatua ambazo zilikuwa hazitegemewi kwa kuweka amri ya kurudia uchaguzi uliofanyika mwaka jana baada ya upande wa upinzani kuleta malalamiko yao.
Uchaguzi huo ulikuwa unatarajiwa kurudiwa Julai 2.
Sasa kama mahakama itaenda kinyume na serikali kwa mara nyingine , washirika wa rais Mutharika watakishutumu chombo hicho kuwa na ushawishi wa kisiasa.
Mashirika ambayo yalipeleka kesi hiyo yanahusishwa na maandamano ambayo yalifanyika mwaka jana ya kutaka kiongozi wa tume ya uchaguzi kufukuzwa kazi na matokeo kufutwa.
Kumekuwa na sintofahamu ya kutoaminika kwa pande zote mbili.
Upande wa upinzani umeeleza kuwa serikali inakuza ukubwa wa tatizo la mlipuko wa corona na hata kudanganya kuhusu wale ambao walioambukizwa na virusi vya corona.
Hali ya virusi vya corona ni mbaya kiasi gani nchini Malawi?
Mgonjwa wa kwanza alitangazwa Aprili, 2, baadae zaidi ya mataifa mengine.
Tangu wakati huo, kuna wagonjwa 36 wenye virusi vya corona ambao wamethibitishwa na wengine watatu wamerikodiwa kuwa wamefariki kutokana na maambukizi ya corona.
Nitajizuia vipi kupata maambukizi ya virusi vya corona?
Jambo la muhimu kufanya ni kuosha mikono kila wakati kwa maji ya kutiririka na sabuni.
Maambukizi ya virusi vya corona yanasambaa kutokana na chembechembe za mtu anapokohoa, kupiga chafya na kufanya virusi vidogo kusambaa hewani, vinaweza kuvutwa na kusababisha maambukizi na hata pale unaposhika kitu ambacho kilipata vijidudu na ukashika pua, acho au mdomo, unaweza kuambukizwa.
Hivyo kikohozi na kupiga chafya kunaweza kukusababishia maambukizi kama ukishika uso wako bila kuosha mikono yako na kuhusiana na mtu ambaye ana maambukizi.
Watu wanaweza kuonyesha dalili ya ugonjwa kabla lakini wengine wasionyesha hata kabla hawajaumwa.
Barakoa hazitoi ulinzi kamili wa maambukizi kwa mujibu wa wataalamu wa afya , ingawa shirika la afya itaangalia mara nyingine kama watu wanapata kinga kupitia barakoa.