Virusi vya corona: Trump 'anajiuliza ni kwanini ' watu wanapiga simu sana kuulizia ufanisi wa kemikali za kuua vimelea

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Rais Trump amesema kuwa "sielewi ni kwanini" Simu zinazopigwa katika kitengo cha dharura kuhusu matumizi ya kemikali za kuua vimelea wa magonjwa zimeongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya rais huyo kupendekeza watu wadungwe sindano za kemikali hizo ambazo hutumiwa katika usafi wa kuua vijidudu vya magonjwa ili kuwatibu wagonjwa wa virusi vya corona.
Magavana wa majimbo ya Michigan na Maryland Jumapili walimlaumu Bwana Trump kwa ongezeko la simu za dharura latika vituo vya dharura.
Kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa wataalamu wa tiba, Bwana Trump alisema kuwa, kauli zake zilikua ni za mzaha.
Kemikali za kuua vimelea na wadudu ni hatari na zinaweza kuwa sumu iwapo zitaingizwa ndani ya mwili wa mtu.
Katika kikao na waandishi wa habari kuhusu Covid-19 siku ya Jumatatu, mwandishi wa habari alisema kuwa namna ya simu ya kituo cha dharura cha Maryland ilipokea mamia ya simu katika siku za hivi karibuni ambapo watu walitaka kupata muongozo juu ya kauli alizozitoa Bwana Trump juu ya matumizi ya kemikali kama tiba ya virusi vya corona.
"Sielewi ni kwanini ," rais alisema, aliharakisha . "Siamini hilo."

Alipoulizwa ikiwa anakiri kuwajibika na ongezeko la simu zinazopigwa kwenye vituo vya dharura, Bwana Trump alijibu: "Hapana. siwajibiki."
Wiki iliyopita, ofisi ya Gavana wa Maryland gilisema kuwa imetoa onyo katika jimbo zima ikiwaonya watu dhidi ya kudungwa au kuingizwa mwilini kwa kemikali hizo kufuatia kauli za rais.
Bwana Trump alitoa kauli siku ya Alhamisi,baada ya afisa kuwasilisha matokeo ya utafiti wa serikali ambayo yalionyesha kuwa Covid-19 inaweza kuuawa kwa dakika na kemikali ya blichi.
"Ninaona kemikali ya kuua vijidudu ikigopnga kirusi kwa dakika. Dakika moja," Bwana Trump alisema. "Na kuna njia yoyote tunaweza kufanya kitu kama hicho, kwa kuingiza ndani au kusafisha kabisa.?"
Ijumaa mchana, Bwana Trump aliwambia waandidhi wa habari: "INiliuliza swali kimzaha kwa mwandishi tu kama wewe kuona tu kile ambacho kingetokea ."
katika mkuytano na waandishi wa habari Jumatatu katika bustani ya Rose Garden, Bwana Trump aliulizwa ikiwa atachelewesha uchaguzi wa urais wa mwezi wa .
"Sijafikiria hata mara moja kubadili tarehe ya uchaguzi," alisema. "Ni kwanini nifanye hilo?"
Makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, mtu anayedhaniwa kuwa mpinzani mkuu wa Trump katika uchaguzi huo kutoka chama cha Democratic, alisema wiki iliyopita kwamba anadhani Bwana Trump " atajaribu kwa namna fulani kuahirisha uchaguzi ".
Lakini Bwana Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa wazo hilo "ni propaganda- zilizobuniwa".
"Niko tayari kwa uchaguzi huo ," alisema Bwana Trump.

Wasomi wa masuala ya katiba tayari wamese,a kwamba kama rais angetaka kubadili muda wa uchaguzi wa White House asingeweza kufanya hivyo-hata katika kipindi cha dharura-kwasababu tarehe hupangwa na Congress.
Bwana Trump pia aliulizwa na mwandishi ikiwa yeye kama rais ambaye amewapoteza Wamarekani katika kipindi cha wiki sita kuliko idadi ya watu waliokufa katika kipindi cha miongo miwili ya vita vya Vietnam anastahili kuchaguliwa tena.
Alisema utawala wake umefanya kazi "nzuri sana ambayo haikutarajiwa "
Jumla ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani ni takriban milioni moja. Kumekua na vifo zaidi ya 55,000

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:















