Virusi vya corona: Je kupiga marufuku uuzaji pombe ni suluhisho la kuzuia maambukizi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Marufuku ya kuuza na kusafirisha pombe wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona nchini Afrika Kusini, umesababisha vitanda hospitalini kuwa wazi, biashara imeathirika kwa kiasi kikubwa, imechochea vurugu na migongano ya kisiasa na watu kuanza kuvutiwa na mananasi.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding kutoka mjini Johannesburg anasema wazo ni rahisi.
Je hatua ya Afrika Kusini kupiga marufuku pombe inafanya kazi?
Kukomeshwa kwa unywaji wa pombe hadharani kumechangia kupungua kwa ugomvi unaotokana na ulevi, unyanyasaji, kuzuia ajali za barabarani zinazosababishwa na walevi kuendesha magari wakiwa wamelewa na pia kumepunguza shangwe za mwishoni mwa wiki katika maeneo yote Afrika Kusini.
Maafisa wa polisi, afya na wachambuzi wamesema kuwa pombe huwa inachangia uwepo wa ajali nyingi zipatazo 40% ya dharura zote hospitalini.
Wakati wa kawaida kesi za dharura huwa ni 34,000 kila wiki nchini Afrika Kusini.
Lakini tangu taifa liweke marufuku mwezi uliopita ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, takwimu hiyo imeshuka na kufikia idadi ya wagonjwa wanaopokelewa kuwa 12,000.
"Ni matokeo chanya sana," alisema Profesa Charles Parry.

Chanzo cha picha, Getty Images
'Udahlimu' wa Mkuu wa polisi
Mkuu wa Polisi Bheki Cele, amejulikana kwa kauli mbaya na vitisho kwa ajili ya katazo la matumizi ya pombe, hivi karibuni alisema jeshi lake litaharibu maeneo ya majengo wanayouza pombe.
Amekuwa akifuatilia namna marufuku ya pombe ilivyosababisha idadi ya wagonjwa kushuka kulingana na utafiti uliofanywa na baraza la madawa la Afrika Kusini.
"Kama tutasitisha marufuku ya mauzo ya pombe, tutaenda kupokea wagonjwa 5,000 kila wiki waliopata mikasa kutokana na pombe.
Ukweli wa kwamba vitanda vya ziada 5,000 ambavyo havitumiki, vitahitajika kama mlipuko wa ugonjwa wa corona utarudi tena katika wiki kadhaa kama vile maafisa wa serikali wanavyoshauri.
"Ugonjwa wa Covid-19 unaenda kuwa na athari kubwa kwa wanyaji wa pombe kupita kiasi na Afrika Kusini watu wengi wanaishi katika makazi ya mkusanyiko wa watu wengi.
"Hivyo mauzo ya pombe yanaweza kuongeza kasi ya maambukizi katika jumuiya kwa sababu watu huwa wanakunywa pombe wakiwa wengi na tunagemea kuona ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kijinsia na watoto pia kufanyiwa unyanyasaji, alionya Profesa Parry.
World Health Organization's advice
Avoid alcohol altogether
Ifyou drink keep it to a minimum
Immunesystem weakened by alcohol, especially if you drink heavily
Reducesability to cope with infectious diseases
Can cause acute respiratory distress syndrome
Drinkingalso increases risk of domestic violence

Lakini changamoto hizo zilizojitokeza kwa muda wa wiki tano au zaidi endapo Afrika Kusini itaongeza muda wa marufuku kuisha Aprili 30.
Mtu ambaye anawajibika kutunga sera za makatazo mapya ameonekana kutumia nguvu kubwa ili kuhakikisha kuwa sheria hizo zinafuatwa na atakayeenda kinyume mamlaka ya usalama kumchukulia hatua.
Kumekuwa na hofu kubwa tayari mfano madai kuwa kuna mwanaume mmoja alipigwa na askari mpaka kufa baada ya kukutwa akinywa pombe barazani kwake.

Pia unaweza kusoma:

Mkuu wa Polisi Bheki Cele, amejulikana kwa kauli mbaya na vitisho kwa ajili ya katazo la matumizi ya pombe, hivi karibuni alisema jeshi lake litaharibu maeneo ya majengo wanayouza pombe.
"Inatiliwa shaka pale kiongozi mkuu wakisiasa akiwahamasisha polisi kutumia nguvu au vurugu au kwenda kinyume na sheria.
Inaonekana kama vile waziri wa polisi anaenda ndivyo sivyo," alisema Gareth Newham, mtaalamu wa masuala ya uhalifu katika taasisi ya utafiti wa usalama nchini Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Viwanda vya pombe nchini Afrika Kusini vimeonyesha kutokubaliana na utaratibu huo kutokana na changamoto wanazokumbana nazo hivyo kutuma malalamiko yao kuwa katazo hilo la kuzuia pombe lipo kinyume na katiba na hatua hiyo imeanzishwa bila ya wao ambao ni wadau wakuu kuhusishwa kwa namna yeyote
Hatua hiyo tangu ianze imeungwa mkono
Lakini pamoja na kwamba sekta hiyo inatambua umuhimu wa jitihada za serikali dhidi ya mapambano ya kuzuia maambukizo ya ugonjwa wa corona.
Lakini changamoto kubwa ni wafanyabiashara wengi kuathirikana na hatua hiyo.
'Inawezekana kuwa utaratibu huo unaisha'
"Mambo hayako vizuri kabisa," alisema Apiwe Nxusani-Mawela, mkurugenzi wa kwanza mwanamke mweusi katika kiwanda cha bia na kiongozi wa jumuiya ya bia ya Afrika Kusini, yeye anahofia kuwa biashara ndogo zitaathirika kama katazo hili litadumu kwa muda mrefu.
"Malalamiko dhidi ya kuondoa kwa katazo linaeleweka.Watu wengi wanakosa ajira na wengine wanaokosa pombe wanatafuta mbadala wa dawa za kulevya.
"na labda kungewekwa kwa kiwango cha mauzo basi kungezuia sekta hiyo kuanguka.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Ni kama mchezo umeisha kwa upande wetu,"alisema Nick Smith, raia wa Marekani ambaye anamiliki kiwanda cha bia cha craft kilichopo nje kidogo ya Cape Town.
"Hatua hii itakuwa na matokeo mabaya sana kwa wafanyabiashara wetu wadogo," aliongeza kusema bwana Smith.
Kuongezeka kwa pombe inayotengenezwa nyumbani
Afisa wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini wa chama cha Democratic Alliance (DA), anaona ni bora marufuku hii ingewaruhusu watu kununua pombe kwa muda fulani au saa fulani kila siku.
Lakini chama kingine kinacholenga uhuru wa kiuchumi zaidi 'Economic Freedom Fighters (EFF)', amedai kuwa madai ya mapendekezo ya chama cha DA ni uuaji na ubaguzi kwa sababu tangu katazo hilo lianze kumekuwa na matokeo chanya katika upande wa sekta ya afya haswa kwa jamii ya watu weusi ambao wametoka katika jamii maskini.

Pia unaweza kutazama:

Watu wengi wamekuwa wakifananisha makatazo yaliyowekwa Afrika Kusini kuwa sawa na marufuku ambayo ilipata umaarufu mkubwa iliyowekwa Many people have compared South Africa's prohibition Marekani miongo mingi iliyopita, marufuku hiyo ilianza mwaka 1920 ikiwa ni jitihada za kuhamasisha dini na watu kufuata maadili na iliwekwa katika filamu za Hollywood kama 'Some Like It Hot na The Untouchables'.
Makundi ya kihuni ya Chicago yalikuwa na hofu juu ya marufuku ya kutouzwa pombe kunaweza kufanya watu wawe wahalifu, au kuingia katiam uvutaji wa sigara. Na ndio hali unahofiwa na wengi kutokea Afrika Kusini.
"Kadri muda wa marufuku ya kutotoka nje unavyozidi basi uhalifu na makundi ya kihalifu yataongezeka hata ,katika upande wa kuuza na kusambaza pombe," pia bwana Gareth Newham alithibitisha kwa kutoa angalizo kwa serikali kuwa tayari wanapoteza kiasi kikubwa cha kodi kutokana na marufuku hiyo.

Marufuku ya uuzaji pombe Afrika Kusini, eneo ambalo lina historia ya ubaguzi na sasa watu weusi wanazuiwa kunywa pombe hadharani na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wanapata kipato kutokana na pombe hawapati kipato hicho, jamii imekuwa katika changamoto kubwa sana.
"Sisi waafrika Kusini , hatuna uhusiano mzuri na pombe.Kwa miaka kadhaa ni kitu ambacho tunashindwa kujizuia nacho," alisema bi Nxusani-Mawela.
Lakini katazo hili halionekani kuwa linajumuisha watu katika maisha tofautitofauti. Bali ni kama linataka watu waanze kutengeneza pombe nyumbani, jambo ambalo lipo siku zote katika maeneo ya vijijini.
Video za jinsi ya kutengeneza bia ya nanasi na pombe nyingine za asili ambazo zinajulikana kama "umqombothi", ndio zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, zikiwa na tahadhari kuwa kama pombe hizo zikiandaliwa vibaya basi ni hatari kwa binadamu.

















