Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Je upo ushahidi wa virusi kutengenezwa katika maabara?
Vyombo vya habari nchini Marekani vinaonyesha kwamba maafisa wa ubalozi walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa kibaiolojia katika maabara moja ya virusi mjini Wuhan China.
Maabara hiyo ipo katika mji ambao ndio chanzo cha virusi hivyo.
Na rais Donald Trump amesema kwamba serikali ya Marekani inachunguza ripoti ambazo hazitahibitishwa kwamba virusi hivyo vilitoroka kutoka maabara.
Hivyobasi tunauliza , je suala hili linachangia vipi mlipuko uliopo?
Je vyombo vya habari vinasemaje?
Gazeti la Washington Post limeripoti kuhusu habari zilizopatikana kutoka vyombo vya kidiplomasia.
Zinaonyesha kwamba 2018 , wanadiplomasia wa kisayansi walitumwa katika ziara za mara kwa mara katika kituo kimoja cha utafiti nchini China.
Maafisa hao walituma onyo mjini Washington wakisema kwamba hakuna usalama wa kutosha katika maabara hiyo.
Taarifa hiyo ilisema kwamba maafisa hao walikuwa na wasiwasi kuhusu usalama na usimamizi katika taaisi ya utafiti wa virusi na hivyo basi wakaomba usaidizi zaidi.
Pia walisema kwamba utafiti wa virusi vya corona katika popo katika maabara hiyo huenda ukasababisha mlipuko mwengine kama ule wa Vurusi vya Sars.
Gazeti hilo linasema kwamba vyanzo hivyo vya kidiplomasia pia vilichochea mazungumzo kwamba huenda taaisi ya utafiti ya WIV ama maabara nyengine mjini Wuhan huenda ndio chanzo cha virusi hivi vilivyosababisha mlipuko.
Wakati huohuo Chombo cha habari cha Fox News pia kimekuza nadharia kwamba virusi hivyo vilitoka katika maabara.
Mlipuko huo iligundulika mwisho wa mwaka jana baada ya visa vya mapema kuhusishwa na soko moja la chakula mjini Wuhan.
Lakini licha ya uvumi wa mara kwa mara uliokuwa ukiendelea hakuna ushahidi wowote kwamba virusi hivyo vya corona vilitolewa kwa bahati mbaya katika maabara.
Je ni hatua gani za kiusalama zinazotumika katika maabara?
Maabara zinazofanyia tafiti virusi na bakteria zinafuata mfumo wa viwango unaojulikana kama BSL, ambapo BSL inamaanisha viwango vya usalama wa kibaiolojia.
Kuna viwango vinne , ambavyo hutegemea aina ya ajenti za kibaiolojia zinazofanyiwa utafiti na tahadhari inayohitajika kuchukuliwa ili kuzitenga.
Kiwango cha awamu ya kwanza cha usalama wa kibaiolojia ndio cha chini na hutumika na maabara kwa kufanyia utafiti ajenti za kibaiolojia ambazo si hatari kwa mwanadamu.
Tahadhari hizo za kuzuia virusi hivyo kutoka katika maabara huongezeka kwa awamu hadi unapofikia awamu ya nne ambayo ndio kiwango cha juu zaidi ,na hutengewa maabara ambazo hufanyia utafiti viini hatari zaidi ambavyo vina chanjo ama tiba chache kama vile ebola, virusi vya Maburg na katika taasisi mbili zilizopo Marekani na Urusi- uugonjwa wa ndui.
Viwango vya BSL hutumika kimataifa lakini tofauti.
Kwa mfano Warusi huzipatia tahadhari zake za juu kuwa nambari moja na zile za chini kuwa nambari 4 , ikiwa ni tofauti kabisa na viwango, lakini hakuna tofauti katika utekelezaji wake, kulingana na Dkt. Fillipa Lentzos, mtaalam wa maswala ya usalama katika taasisi ya King College mjini London.
Lakini huku shirika la Afya duniani WHO likichapisha viwango tofauti, havitekelezwi na makubaliano yaliowekwa.
Vimewekwa ili watu waweze kufanya kazi kwa usalama na kwa wafanyakazi wa maabara hizo ambao hawataki kujiambukiza ama kuambukiza jamii zao, mbali nakuzuia ajali za kimazingira, alisema Dkt. Lentzos.
Lakini anaongezea: Iwapo unataka kufanya miradi na washirika wa kimataifa , wanahitaji maabara ambazo utendakazi wake ni wa kiwango fulani.
Na iwapo una bidhaa za kuuza katika soko, ama kutoa huduma fulani kama vile vipimo, pia unahitajika kuwa na utendakazi wa kiwango cha kimataifa.
Ni kweli maabara ya Wiv ilipokea ufadhili kutoka Marekani , pamoja na usaidizi kutoka taasisi ya utafiti ya Marekani. Vyanzo hivyo vya habari vilipendekeza vipatiwe usaidi zaidi.
Je! Ni ukosefu gani wa usalama ambao vyanzo hivyo vinaelezea?
Jibu fupi ni kwamba hatujui kutokana na habari iliotolewa katika gazei la Washington post.
Lakini kwa ujumla , kuna njia tofauti kwamba masharti ya kiusalama yanaweza kukiukwa katika maabara zinazofanyia kazi ajenti za kibaiolojia.
Kulingana na Lentzos ,hizo ni pamoja na nani anayeweza kutumia maabara hizo, mafunzo yanayoendelea katika maabara, masharti ya kuweka rekodi, idadi ya viini hatari vilivyopo , na ajali zinazotokea mara kwa mara, mbali na tahadhari zinazofuatwa.
Kwa nini si kawaida kwa habari kama hizo kutoka katika vyanzo vya kidiplomasia?
Ajali hutokea. Mwaka 2014 , viini vilivyosahaulika vilipatikana katika kadibodi katika kituo kimoja cha utafiti karibu na mji mkuu wa Washington.
Mwaka 2015 , jeshi la Marekani kwa bahati mbaya lilisafirisha sampuli zilizohai za bakteria badala ya spores zilizokufa kwa maabara tisa nchini humo pamoja na kambi moja ya kijeshi nchini Korea Kusini.
Je kumekuwepo na madai ya virusi kutoka katika maabara?
Kweli, mara tu virusi vya corona vilipobainika kulikuwa na uvumi umwingi ambao hakuwa umethibitishwa kuhusu chanjo chake.
Nadharia moja ya mtandaoni , ambayo ilisambaa mwezi Januari ni kwamba huenda virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara kama silaha ya kibaiolojia.
Madai hayo yamepengwa na wanasayansi , ambao wanasema kwamba utafiti huo unaonesha kwamba virusi hivyo vilitoka kwa wanayama- hususan popo.
Virusi pia vinaweza kutengenezwa ili kufanyia utafiti fulani wa kisayansi.
Lakini utafiti wa jeni ya coronavirus uliochapishwa mwezi Machi haukupata dalili zozote kwamba virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara.
''Kwa kulinganisha data za jeni zilizokuwepo. tunaweza kuthibitisha kwamba virusi vya SARS-C0v=2 vinatokana na uasilia'' , kulingana na mtafiti mwenza Kristian Andersen kutoka kwa taasisi ya utafiti kwa jina Scripps mjini Californa.
Halafu kuna yale madai ya kuwachilia virusi asilia kwa bahati mbaya kutoka kwa maabara.
Ukaribu wa soko la chakula la Wuhan , ambapo mlipuko huo ulianzia hadi katika taasisi mbili zinazofanya utafiti wa magonjwa ya maambukizi ulizua uvumi kuhusu ushirikiano huo.
Kwamba taasisi ya utafiti ya WIV ilifanyia utafiti virusi vya popo ni suala ambalo linahitaji kuangaziwa.
Kazi hiyo ilifanyika kwa kufuata sheria na baadaye kuchapishwa katika jarida la kisayansi la kimataifa.
Kutokana na jinsi taifa hilo lilivyokabiliana na janga la virusi vya SARS 2000, haikuwa jambo geni kwa madai kama hayo kutolewa.
Bwana Lentzos anasema kwamba suala la chanzo cha virusi hivyo ,lilikuwa swali gumu, na kuongezea, kumekuwa na mjadala wa nyuma ya pazia ...miongoni mwa wataalam wa usalama wa kibaiolojia, wakihoji soka hilo la chakula cha baharini nchini China.
Lakini kufikia sasa hakuna ushahidi kwamba taasisi yoyote ya utafiti mjini Wuhan ilikuwa chanzo cha virusi cya corona.
Pia unaweza kusoma:
Siku ya Alhamisi iliopita waziri wa maswala ya kigeni nchini China Zhao Lijian alizungumzia suala hilo katika mkutano na vyombo vya habari akiwaambia waandishi kwamba shirika la Afya duniani limesema mara kadhaa kwamba hakuna ushahidi kwamba virusi hivyo vipya vilitebgenezwa katika maabara.
Rais Donald Trump, ambaye amekuwa akishtumiwa kuhusu jinsi alivyolichukulia suala hilo la mlipuko , alisema kwamba serikali ya Marekani inachunguza nadharia hiyo ya virusi hivyo kutengenezwa kutoka katika maabara.
China mara kwa mara imeshutumiwa kwa kukosa uwazi katika awamu za mapema za mlipuko , na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema kwamba Beijing, inapaswa kujisafisha kuhusu kile inachojua.
Na kutokana na vita hivyo vya maneno kati ya mataifa hayo mawili, utafiti kuhusu chanzo cha virusi hivyo utaendelea.