Virusi vya Corona: Marufuku ya kutoka nje yaongezwa kwa siku 21 Uganda

Museveni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametangaza kuongeza muda wa marufuku ya watu kutoka nje kwa siku 21.

Hatua hiyo inachukuliwa kama njia ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Mpaka sasa watu 54 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na kati yao wanne wapemona. Hakuna kifo kilichoripotiwa kufikia sasa.

Machi 31, Museveni alitangaza marufuku ya watu kutokutoka nje kwa siku 14, ambazo zilikuwa zinaisha leo Aprili 14.

Hii leo, Museveni amesema bado wanahitaji muda zaidi wa kupambana na virusi hivyo na watu waendelee kusalia majumbani mwao.

Coronavirus
Banner

Akizungumza nna wanahabari kutoka ikilu ya rais na wanahabari katika mkutano unaorushwa mubashara, Museveni amesema serikali ingali inawasaka watu wengine ambao wamepata maambukizi.

"Hawa 54 wamegundulika kwa kuwa tuliweka hatua za kuwazpiwa na kuwazuia karantini wasafiri waliokuwa wanaingia nchini," ameeleza Museveni na kuongeza: "Kuna uwezekano baadhi ya wasafiri hawakuonesha dalili lakini wameambukizwa sasa hawa wataendelea kuambukiza watu kwa siku 34 mbele."

Museveni ameeleza kuwa kwa watu kuendelea kusalia ndani kama kuna mtu ambaye hakugundulika awali ataonesha dalili ama ataambukiza mtu wake wa karibu ambaye ataonesha dalili.

"Hata kama baba hakuonesha dalili, ataambukiza familia yake na haiwezekani familia nzima kutokuonesha dalili. Hivyo tutawapata kirahisi na hawataambukiza wengine.

"Tumepiga hatua, tuna mafanikio tuliofikia na changamoto pia. Tuchukue tahadhari zaidi."

Hatua gani zimechukuliwa Uganda

Wanajeshi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amri ya kutokutoka nje nchini Uganda inasimamiwa na vyombo vya ulinzi

Rais Museveni amesema kuwa hatua zote zilizotangazwa ilipotangazwa marufuku ya awali zitaendelea kama kawaida.

Hatua hizo ni pamoja na kuzuia kabisa mikusanyiko ya watu. Nyumba za ibada na taasisi zote za elimu zitaendelea kufungwa.

Watu pekee watakaoruhusiwa kutoka na kuendelea na shughuli zao ni wafanyakazi katika sekta muhimu kama afya, ulinzi na usalama, wafanyakazi wa benki na wanahabari.

Usafiri wa umma na wa ndege za abiria pia umepigwa marufuku.

Magari ya mizigo pamoja na ndege za mizigo zinaruhusiwa kuendelea na shughuli zake. Hata hivyo marubani na wasidizi wao katika ndege za mizigo watawekwa katika maeneo maalumu chini ya uangalizi wa serikali.