Virusi vya corona: Je Trump ana 'mamlaka 'ya kuondoa marufuku ya kutotoka nje?

A quiet Wall Street with a view of a statue of George Washington and the New York Stock Exchange in New York, 13 April 2020

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Barabara ya Wall Street ilivyosalia mahame karibu na sanamu ya George Washington
Iliyochapishwa

Rais Donald Trump amedai kuwa anatumia nguvu zote ili kuhakikisha kuwa taifa kwa ujumla linajiondoa katika marufuku ya kutotoka nje kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, jambo ambalo linatofautiana na kile ambacho magavana na wataalamu wa sheria wamesema.

Rais wa Marekani anataka chanjo ianze kujaribiwa.

Lakini katiba ya Marekani inataka watu wawe salama na katika utaratibu wake.

Majimbo 10 ya Mashariki na kaskazini mwa pwani ya Marekani yana mpango wa kuachana na marufuku ya kutotoka nje.

Marekani imethibitishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kwa kuwa na wagonjwa 682,619 na vifo 23,608 vilivyotokana na corona.

Mwanamke aliyevalia barakoa akitembea na mbwa wake katika bara bara ya Park Avenue ambayo haina shughuli nyingi kutokana na corona

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke aliyevalia barakoa akitembea na mbwa wake katika bara bara ya Park Avenue ambayo haina shughuli nyingi kutokana na corona

Rais Trump alisema nini?

Bwana Trump, alisema kuwa anamalizia mipango ya kurejesha uchumi wa Marekani ambao ulikuwa umesimama kwa muda ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mamlaka ya Trump imesema kuwa anatazamia kusitishwa kwa marufuku ya kutotoka nje kufikia Mei mosi.

Kwa sasa mamlaka hiyo ya Marekani imewashauri wananchi wake kuacha kula katika migahawa, kuacha safari zisizo za klazima na kujizuia kukaa katika mikusanyiko ya watu waliozidi 10, mpaka Aprili 30.

Lakini waandishi wa habari wanahoji ikiwa bwana Trump ana mamlaka ya kutoa amri ya kutaka watu wabaki nyumbani au la katika kila jimbo, na rais akasema kama mtu ni rais wa Marekani basi ana mamlaka yote katika nchi.

"Mamlaka ni yote. Magavana wanatambua hilo."

Aliongeza: "Tunaenda kufanya kazi katika majimbo yote."

Rais alisisitiza kuwa ugawaji wa mahitaji muhimu katika taifa hilo huwa haugawi ni wapi anahusika zaidi kuliko kwingine.

Lakini wataalamu wa sheria wanasema kuwa rais hana mamlaka ya kuondoa marufuku iliyowekwa kulinda afya za watu katika eneo lolote.

Aliulizwa na mwandishi wa BBC, Jon Sopel kuhusu wasiwasi wa kuhitajika kufunga uchumi tena kama mlipuko wa virusi vya corona utarejea tena kwa kasi, rais Trump alisema: "Hajafikiria suala hilo kwanza."

New york City residents

Chanzo cha picha, Getty Images

Aliwaambia waandishi kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya corona nchini Marekani vinaanza kupungua na hii inaashiria kuwa jitihada za watu kukaa kwa mbali zinafanikiwa.

Wakati anawahutubia waandishi katika Ikulu ya White House alicheza video inayomuonyesha rais akiwahutubia namna ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu huku magavana wakiwa wanasifu utawala wa Trump.

Vyombo vya habari vingi ambavyo vilikuwa vinarusha matangazo mubashara vilikata matangazo hayo ghafla.

Coronavirus
Banner

Magavana wanasema nini?

Magavana wa majimbo mbalimbali wana haki ya kuwalinda wananchi wao na virusi vya corona wakati ambao marufuku ya kutotoka nje itakuwa imeondolewa.

Akijibu ujumbe alioandika Trump katika mtandao wake wa Tweeter mapema leo, unaodai kuwa mamlaka ya pamoja ndio yanazingatiwa Govana Tom Wolf wa jimbo la Pennsylvania alisema: "Sawa, tumeona namna tulivyokuwa na majukumu ya kufunga majimbo yetu hivyo nadhani tuna haki ya kuamua ni lini tunaweza kufungua tena majimbo hayo."

Magavana wa majimbo mbalimbali walijadili mipango ya kurejesha shughuli za kiuchumi bila kuhusisha utawala wa Trump.

Maafisa wa New York, New Jersey, kisiwa cha Rhode, Connecticut, Delaware, Massachusetts na Pennsylvania wamehaidi kuwa watachukua hatua sahihi kurejesha uchumi lakini hawakusema ni lini haswa, hatua hizo zitaanza kufanya kazi.

Mji wa New York una maambukizi ya virusi vya corona yapata 190,000 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni zaidi ya 10,000 - idadi ikiwa kubwa zaidi duniani.

Lakini kwa upande wake Gavana Andrew Cuomo alisema kuwa anaamini kuwa kipindi kibaya kimeshapita katika jimbo lake.

"Hakuna mtu ambaye alikuwa katika hali hii kabla, hakuna mtu anayefahamu jibu ya maswali," alisema bwana Cuomo. "Akiwahutubia umma kuhhusu afya na uchumi; alihoji kwani afya na uchumi kipi ni cha kwanza? Vyote ni muhimu.

Majimbo ya kaskazini mwa California, Washington na Oregon yalitangaza pia mipango ya kufungua uchumi tena.

Wataalamu wa Massachusetts, na majimbo 10 yote yanayoongozwa na magavana wa chama cha Democratic.

Zaidi ya majimbo 40 yameweka amri ya watu kubaki majumbani mwao.

Mikakati gani mataifa mengine yamechukua?

Kuna njia tofauti ambazo mataifa mbalimbali duniani yamechukua ili kuhakikisha kuwa amri ya kutotoka nje inazingatiwa.

Jimbo la Wuhan,nchini China ilikuwa sehemu ya kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya kwanza ya ugonjwa wa corona mwaka jana mwezi Desemba, na mji huo ulifunguliwa baada ya zaidi ya miezi miwili ya kujitenga.

Uhispania imeruhusu watu wapatao 300,000 ambao wanafanya kazi ambazo ni za mahitaji muhimu kurejea kazini.

Italia ni taifa lingine ambalo lilipigwa vibaya na ugonjwa huo barani Ulaya -linatarajia kuruhusu biashara kidogo kuanza kufanyika wiki hii.

Ufaransa, rais Emmanuel Macron ametangaza kuwa taifa lake litakuwa limefungwa mpaka Mei ,11.

Serikali ya Uingereza ilisema kuwa watu wasitegemee mabadiliko yoyote ya amri ya kutotoka nje kwa wiki hii.

Mambo gani mengine ambayo Trump aligusia?

Trump alisema siku ya Jumatatu kuwa hajadhamiria kumfukuza mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi nchini Marekani, Anthony Fauci - ikiwa ni siku moja baada ya rais kuandika kwenye kurusa ya tweet akiweka 'hashtag' "#firefauci".

Dr Fauci aliwataka wasaidizi wa rais kufunga nchi mapema wakati maambukizi ya corona yalivyoibuka,na kudai kuwa maisha ya wengi yangekuwa yameokolewa.

Bwana Trump alimualika Dkt Fauci - katika ikulu ya White House kutoa muktasari kuhusu ugonjwa huo na kazi ya kuzuia inabidi iende vipi.

"Nadhani ni mtu mzuri," bwana Trump alisema, aliongeza kuwa kila mtu anaridhika na utaalamu wake wa afya.

Dkt Fauci alisahihishwa au alikinzana na bwana Trump katika masuala ya kisayansi wakati huu wa janga la corona.

Lakini siku ya Jumatatu alikubali kuwa hakuwa na matamshi mazuri wakati alipohojiwa na CNN.

Wakati bwana Trump alipokuwa anachukua hatua kidogo dhidi ya maambukizi ya Corona, alikuwa peke yake akiangazia suala hilo.

Tarehe 17, Februari Dkt. Fauci alisema hatari ambazo zinaweza kuletwa na maambukizi ya ugonjwa wa corona akitofautisha na hatari ya mafua ya kawaida.