Virusi vya Corona: Changamoto anazokumbana nazo asiye na uwezo wa kuona wakati wa janga la Corona

Iliyochapishwa

Janga la coronavirus limesababisha matatizo kwa kila mmoja.

Lakini je umewahi kujiuliza hali ikoje kwa wasio na uwezo na kuona? Mwanahabari wa BBC mwenye ulemavu huu, Kate Pounds amekutana na waathirika na hapa anaelelezea.

Wakati treni ilipokuwa inakaribia London Waterloo katika safari yangu ya mwisho kutoka kazini kabla ya shughuli zote kusitishwa na serikali, abiria mwenzake aliyekuwa naye alikataa kubofya kitufe cha kufungua milango alipotaka kuingia kwasababu ya kuogopa virusi vya corona.

''Nikaanza kufikiria, kama miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo nilazima nishike vitu na mahali mara nyingi kwa , tofauti na mtu asiyekuwa na mapungufu yoyote, amesema Kate.

Nikiwa tu kwenye stesheni, ni lazima nishikeshike machine ya kukata tiketi, lazima nishike eneo la mwisho la lifti ili nitambue kama itanipeleka juu ama chini, nishike eneo la kando ya mlango kuhakikisha pengo lililopo wakati nataka kupanda treni.

Aidha ni vigumu sana kujua sabani na maji yalipo au kujua kemikali ya kuosha mikono iko wapi wakati unataka kuosha mikono, kulingana na kate.

Je wengine wenye matatizo ya kuona wanakabiliana vipi na virusi vya corona?

Sajid Ali, 40, amesomea utafiti wa biashara kutoka West Yorkshire, anasema kwenda katika duka la kufanyia manunuzi imekuwa changamoto kubwa - hasa wakati ambapo anahitajika kubeba kile atakachotumia kwa wiki nzima kwa mkono mmoja na kijiti chake kinachomuongoza kwenye mkono wa pili.

Anasema hilo linamfanya kuanza kuyumbayumba na kuwa vigumu kwake kutembea akiwa wima.

Anasema mara nyingi huomba usaidizi wa kutafuta vitu anavyohitaji lakini siku za hivi karibuni imekuwa vigumu yeye kupata usaidizi anaotaka kwasababu kila mmoja anaogopa kuambukizwa virusi vya corona.

"Walisema kwamba hawawezi kutoa msaada wao kwasababu ya kile kinachoendelea kwasasa, " anasema. "Huu itakuwa ni ugonjwa wa kuambukiza kwasababu kutafuta mtu wa kunishika mkono aniongoze.

Nilisubiri kwa zaidi ya dakika 5, ingawa hatimaye nilipata wakunisaidia."

Kwenda dukani tu ni changamoto kwa Reanna Parkinson, 22, kutoka Lancashire.

"Kuna barabara nyingi kuu hapa na kufanya iwe vigumu kuvuka na hivyobasi siwezi kufika madukani mwenye, "anasema.

Reanna, aliyehitimu katika elimu ya jinai na sosholojia, ambaye anapenda sana kuwa huru lakini kwasasa anaona hana budi zaidi ya kurejea kuishi na wazazi wake.

"Kawaida huwa kuna wanaoniletea bidhaa zangu lakini kwasasa foleni ya kusubiri hadi ufikiwe ni ndefu," anasema.

"Baadhi ya huduma za kwenye mtandao zasema kwamba wanaopewa kipaumbele ni wale wenye ulemavu.

Nimeona ujumbe tofauti tofauti kutoka kwa wasio na uwezo wa kuona wakiuliza ni vipi wanaweza kupewa kipaumbele lakini hakuna anayejibu ujumbe wao."

Lakini hata ukapata fursa ya kufanya manunuzi mtandaoni kwa watu wasiona uwezo wa kuona, mchakato huu una hatua nyingi na uko polepole, na inakuwa changamoto zaidi wakati kila mmoja anaagiza bidhaa.