Sankale Ole Kantai: Jaji aliyedaiwa kushirikiana na mshukiwa wa mauaji Kenya kushtakiwa

Chanzo cha picha, KBC/TWITTER
Jaji mmoja nchini Kenya atafunguliwa mashtaka mahakamani kufuatia madai kwamba alishirikiana na mshukiwa wa mauaji.
Jaji wa mahakama ya rufaa Sankale Ole Kantai alikamatwa na maafisa wa jinai siku ya Ijumaa na kuhojiwa kuhusu uhusiano wake wa karibu na Sara Waimu , mshukiwa mkuu wa mauaji ya raia wa Uholanzi Tob Cohen.
Jaji huyo aliachiliwa siku ya Jumamosi mchana kwa dhamana baada ya kulala katika kituo cha polisi cha Muthaiga ambapo alikuwa anazuiliwa.
Atawasilishwa mahakamani siku ya Jumanne.
Idara ya Jinai imethibitisha kwamba jaji huyo atafunguliwa mashtaka ya kuwa na njama ya kuilaghai haki na kuingilia mashahidi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwili wa raia huyo tajiri kutoka Uholanzi ulipatikana katika shimo la maji taka nyumbani kwake jijini Nairobi 2019.
Maafisa wa polisi wanasema kwamba wana sababu za kuamini kwamba jaji Sankale alikuwa na uhusiano wa karibu na mshukiwa huyo ambaye amedaiwa kumpa ushauri ili kukabiliana na kesi yake mahakamani.








