Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nikita Pearl Waligwa: Nyota wa Queen of Katwe wamuomboleza muigizaji mwenzao
Nyota wa filamu ya Queen of Katwe wametoa risala za rambi rambi kwa muigizaji nyota Nikita Pearl Waligwa ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 15.
Waligwa alikuwa ampetikana na uvimbe katika ubongo na akafariki katka hospitali moja mjini Kampala siku ya Jumamosi.
Alishiriki katika filamu hiyo ya 2016 inayotokana na hadithi ya kweli ya Phiona Mutesi , nyota wa mchezo wa chess kutoka mtandao mmoja wa mabanda nchini Uganda.
Nyota mwenza David Oyelowo aliandika katika mtandao wa instagram: Alikuwa mwangaza katika Queen of Katwe na maishani. Aliigiza kama mwalimu wa mchezo wa chess wa Phiona Mutesi huku Lupita Nyong'o akiigiza kama mamake.
Waligwa aliigiza kama Gloria , rafiki wa Phiona alimwelezea kanuni za Chess.
Bi Nyongo aliandika katika mtandao wa instagram akisema: Aliigiza kama Gloria na uwezo mkubwa . Katika maisha yake alikuwa anakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na saratani ya ubongo.
Gloria Nansubuga, kijana wa miaka 19 kutoka Uganda ambaye ni nyota wa mchezo wa chess ambaye aliigizwa na Waligwa aliambia BBC: Siwezi kuhimili habari kwamba mtu aliyeniigiza katika filamu amefariki.
''Nampenda kutoka moyoni mwangu. Aliniambia kwamba alitaka kujifunza kucheza chess . Nilitaka kuwa na mafunzo naye lakini alikuwa hospitali kila mara . Alikuwa mkarimu licha ya kuwa na umri mdogo''.
Waligwa kwa mara ya kwanza alipatikana na uvimbe wa ubongo mwaka 2016 na mkurugenzi wa filamu ya Queen of Katwe Mira Nair aliripotiwa kutuma watu ili kusaidia kufadhili matibabu yake nchini India, huku madaktari wa Uganda wakiripotiwa wakisema kwamba hawakuwa na vifaa vinavyohitajika kumtibu.
Nchini Uganda ni kiwango kidogo cha wagonjwa walio na hali mbaya kama hiyo ambao hupata usaidizi huo wa kimatibabu kutokana na gharama za juu. Alionekana hana tatizo lolote mwaka 2017 na kurudi shule ya upili.
Hatahivyo mwaka jana alipatikana na uvimbe mwingine katika ubongo.
Kifo chake kilitangazwa na shule kupitia mtandao wa twitter.
''Ulikuwa kipenzi cha wengi na sasa tumekupoteza kupitia saratani ya ubongo katika umri mdogo'', ilisema shule ya upili ya Gayaza.
Ibada ya mazishi ya Waligwa ilifanyika siku ya Jumapili na atazikwa baadaye siku ya Jumatatu.