'Mji uliojengwa na wanawake': Makazi kwa waliotoroka vita Colombia

Barabara kuu katika Mji wa Wanawake inaitwa "Avenue of the Woman Warrior"

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Barabara kuu katika Mji wa Wanawake inaitwa "Avenue of the Woman Warrior"
Iliyochapishwa

Colombia imeshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya nusu karne kati ya wanamgambo waliokuwa msituni dhidi ya wanajeshi na kulazimu zaidi ya watu milioni 8 kutoroka makazi yao.

Wanawake na raia wa nchi hiyo, hususani, wenye asili ya Afrika walipitia madhila mengi zaidi katika mapigano hayo na mara nyingi walikuwa wakijipata wamesafiri hadi miji ya mbali wakiwa hawana chochote walichobeba.

Katika mji wa pwani wa Cartagena ambao mazingira yake yisiyo ya kuridhisha, wenye joto jingi, kundi la wanawake waliokimbia vita hivyo waliamua kuchukua hatua kubadilisha maisha yao.

Mwaka 2003 waliunda chama chao na wakaanza kujenga mji wao, tofali kwa tofali: Mji wa wanawake.

Mji huo, katika eneo jirani la manispaa la Turbaco, lina nyumba 100 ambazo wanawake hao walizijenga kwa mikono yao wenyewe. Colombia imeshuhdia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya nusu karne kati ya wanamgambo waliokuwa msituni dhidi ya wanajeshi na kulazimu zaidi ya watu milioni 8 kutoroka makazi yao.

Wanawake na raia wa nchi hiyo, hususani, wenye asili ya Afrika walipitia madhila mengi zaidi katika mapigano hayo na mara nyingi walikuwa wakijipata wamesafiri hadi miji ya mbali wakiwa hawana chochote walichobeba.

Katika mji wa pwani wa Cartagena ambao mazingira yake yisiyo ya kurudhisha, wenye joto jingi, kundi la wanawake waliokimbia vita hivyo waliamua kuchukua hatua kubadilisha maisha yao.

Mwaka 2003 waliunda chama chao na wakaanza kujenga mji wao, tofali kwa tofali: Mji wa wanawake.

Mji huo, katika eneo jirani la manispaa la Turbaco, lina nyumba 100 ambazo wanawake hao walizijenga kwa mikono yao wenyewe.

Alama inayosema "kuwa makini, mfumo dume unaua" ipo katikati ya mji, karibu na nyumba 100 zilizojengwa na wanawake wenyewe na familia zao.

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Alama inayosema "kuwa makini, mfumo dume unaua" ipo katikati ya mji, karibu na nyumba 100 zilizojengwa na wanawake wenyewe na familia zao.

Wakati wa vita hivyo, unyanyasaji wa kingono na kulengwa kwa wanawake ni baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yakiwatia hofu. Wanawake wengi ni manusura wa vita hivyo.

Mji huo ni makazi kwa wanawake na familia zao ambazo zilikumbwa na mauaji, ubakaji, vitisho na dhuluma nyingine nyumbani walikotokea na hata kule walikokuwa wamekimbilia. Uhalifu wote huo dhidi yao unasalia kuwa uvunjaji wa sheria bila hofu ya kuadhibiwa.

Na ili kupiga vita madhila waliokuwa wanayapitia, waliamua kuungana na kuwa kitu kimoja na hilo likawapa msukumo na nguvu ya kupigana na mfumo dume, desturi na mila zisizokuwa na msingi na unyanyapaa dhidi ya watu waliotoroka makazi yao ambao huwa ndio waathirika wakubwa.

Leaders of the City of Women gather in their community centre on 20 January, 2020 near Turbaco, Colombia.

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Wanawake hao wanasema wamekuwa kama dada wa tumbo moja. "Tunalindana, na tunajali," amesema mkuu wao Lubis Cardenas (katikati).

"Vita vimetufanya tukatoroka makazi yetu, vinakuzimia ndoto yako, tamaduni uliozoea, na hata kuacha ardhi uliyoienzi."

Consuelo Villega Mendoza, 44, anatoka mji wa kaskazini wa Sucre, na alilazimika kuhama makazi yake baada ya wanajeshi kuanza kutekeleza mauaji ya halaiki katika maeneo yaliyokuwa karibu na nyumbani kwake.

"Ni jambo ambalo tulitarajia huenda likatoea muda wowote," anasema. "Niliondoka kwa hofu."

Akiwa na binti yake, wanaendesha mgahawa nje ya mji ambao wameujenga. Wanatengeneza mondongo, supu maarufu Colombia.

Cousuelo Villega Mendoza, 44, na binti yake wakipika kwa ajili ya wateja wao mgahawani

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Cousuelo Villega Mendoza, 44, na binti yake wakipika kwa ajili ya wateja wao mgahawani

"Kuwa sehemu ya wanawake hawa kumenisaidia sana kwasababu wamenifunza namna ya kusonga mbele na maisha. "

Bango la kumbukumbu lililoandikwa "La Ciudad de Mujeres" yaani limebadilisha maisha ya wanawake na kutimiza ndoto zao.

Wanawake katika mji huo wamekuwa wakipigania kupata haki kwa uhalifu waliotendewa lakini kesi zote 159 za unyanyasaji wa kijinsia na kuachwa bila makazi bado hazijatatuliwa.

Bango lililo katikati mwa mji linasomeka ''Mji wa wanawake''

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Bango lililo katikati mwa mji linasomeka ''Mji wa wanawake''

Alneris Orozco Caupo, 47, amesimama akijiangalia kwenye kioo katika mji wa wanawake. Mji wake halisi upo kaskazini mashariki mwa eneo la Cesar, alilazimika kutoroka makazi yake akiwa na watoto wake wawili wadogo zaidi ya miaka 20 iliyopita kwasababu ya mapigano kati ya wanajeshi na waasi wa FARC

Anaonesha picha za watoto wake akikumbuka wakati walipokuwa wanamaliza shule ya upili na kuhitimu chuo kikuu, kitu ambacho hangeweza kukifikia kwasababu ya vita.

Erika Maria Gamarra Caro, 42, kutoka El Carmen de Bolívar alikimbia vita baada ya watu wa familia yake kuuawa wakati wa mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na mrengo wa kulia wa wanajeshi wakati wanapigana na waasi wa mrengo wa kushoto wa FARC.

Anasema kwamba alinyanyaswa mara kadhaa kingono wakati ametoroka makazi yao lakini jamii yake mpya imemsaidia kukabiliana na yale aliyoyapitia.

Erika Maria Gamarra Caro, 42, (centre) laughs during a meeting with other members of the League of Displaced Women.

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Erika Maria Gamarra Caro, 42, (katikati) anacheka wakati wa mkutano na wanawake wengine wa 'Mji wa Wanawake'

"Niligundua kwamba mimi ni mwanamke na nina haki zangu na kuanza kuzidai," ameongeza. "Sasa, mimi si mwanamke mwenye haya tena, siyo yule mwanamke ambaye siwezi kuzungumza kwasababu ya hofu au kuhisi kwamba kwa kuwa ni mwanamke basi sina thamani yoyote."

A sign reading "peace" sits in the window of a home in the City of Women on 20 January, 2020.

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Alama iliyoandikwa "amani" katika dirisha la nyumba moja ya Mji wa Wanawake.

Wakati wanajenga nyumba, watu wa jamii zao waliuawa, kubakwa na kutishiwa maisha lakini wakasema mji wa waliojenga ni nembo ya Amani.

Carmen Beluas, 45, alitoroka mji wa Copey mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya mume wake kuuawa na wanajeshi waliomshutumu kwa kuwa na uhusiano na waasi wa vita vya msituni.

Carmen Beluas, 45, fled from her home of Copey, Colombia in the late 1990s after her husband was murdered by paramilitary forces who accused them of being affiliated with guerrillas.

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Aliondoka na watoto wake watatu na kuwasili Cartagena bila ya mtu yeyote na hakuna aliyemfahamu. Anasema daima atakumbuka vile mume wake alivyochukuliwa akiwa naye.

"Ni jambo ambalo haliwezi kurejea kuwa la kawaida. Najua nina watoto, lakini kuna vitu ambavyo siwezi kusahau."

Licha ya jina lake, Mji wa Wanawake huo pia una wanaume. Wanawake ambao mara nyingi wanashikilia katika kazi za majumbani, walijenga jamii ya watoto na wanze wao kuishi, na Mji huo sasa umeanza kukua na familia kuongezeka.

Kiongozi wa jumuia ya wanawake Eidavis Montes, mumewe na mtoto wao wakiwa nyumbani kwao

Chanzo cha picha, Megan Janetsky

Maelezo ya picha, Mume wa kiongozi wa jumuia ya wanawake Eidavis Montes, na mtoto wao wakiwa nyumbani kwao