Muasisi wa kundi la muziki Ladysmith Black Mambazo Joseph Shabalala amefariki dunia

Joseph Shabalala with members of Ladysmith Black Mambazo in 1998

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joseph Shabalala akiwa pamoja na wajumbe wa kikundi cha Ladysmith Black Mambazo mwaka 1998
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Joseph Shabalala, ambaye alisaidia kuifahamisha sauti ya muziki wa kitamaduni wa Zulu kwa dunia , amefariki akiwa na umri wa miaka 78.

Mwanamuzuiki huyo alifahamika zaidi kama muasisi na muongozaji wa kikundi cha kwaya cha Ladysmith Black Mambazo, kilichoshinda tuzo tano Grammy na kushiriki katika albamu ya Graceland ya Paul Simon.

Pia walifika nafasi ya 15 katika chati za Uingereza chini ya Swing Low Sweet Chariot, iliyoandaliwa kwa ajili ya Kombe la Dunia la Ruga mwaka 1995.

Shabalala amefariki dunia hospitalini mjini Pretoria, Afrika Kusini,amesema meneja wa bendi.

"Ndio ni kweli. Bwana Shabalala amefariki asubuhi ya leo," Xolani Majozi ameliambia gazeti la Afrika Kusini t South Africa Times.

" Kikundi hicho kiko katika safari ya onyesho nchini Marekani, lakini wamefahamishwa na wanamesikitishwa sana kwasababu kikundi ni familia."

katika kauli, bendi ilisema: "Tunasherehekea na kuheshimu moyo wake wa ukarimu na maisha yake ya kipekee. Kupitia muziki wako na mamilioni waliowahi kukutana na wewe, utaishi daima ."

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Transparent line (white space)

Serikali ya Afrika Kusini imetuma salamu zake za rambirambi kwa mwanamuziki huyo katika ujumbe wake wa Twitter ikisema: "Tungependa kutuma rambi rambi zetu kufuatia kifo cha Joseph Shabalala ambaye alikua muasisi wa kikundi cha Ladysmith Black Mambazo.

Iliongeza katika lugha ya Xhosa, "Ulale ngoxolo Tata ugqatso lwakho ulufezile." (Pumzika kwa amani, baba, mbio zao zimekamilika.)

Maelezo ya video, Ladysmith Black Mambazo remember singing and dancing with Nelson Mandela.

Shabalala alizaliwa mwaka 1941, akiwa ndiye mtoto wa kwanza kati ya watoto wanane katika kijiji cha Tugela karibu na mji wa Ladysmith nchini Afrika Kusini.

"Nilipokua mvulana mdogo niliota kuwa nitakua msomi , labda kama mwalimu, daktari au kitu kama hicho,"aliliambia gazeti la The Citizen mwaka 2014.

Hata hivyo , alilazimishwa kuacha shule akiwa na umri wa miaka 12 wakati baba yake alipofariki akafanya kazi katika shamba, na baadae katika kiwanda.

Katika muda wake wa ziada, alikua akiimba na rafiki zakekatika kikundi cha watu weusi.

"Wavulana wadogo walipokutana pamoja, walianza kuimba nyimb, hadi akina mama na majirani wakasema , 'Hee, fanyeni tena,'"aliiambia BBC.

Ndio hivyo tu .Walivyoitwa , 'Fanya tena,fanya tena ."

Shindano la redio mnamo mwaka 1970 liliwezesha kundi hilo kupata mkataba wa kurekodi, na mwaka 1973 walitoa albamu yao iliyouzwa sana, Amabutho.
Maelezo ya picha, Shindano la redio mnamo mwaka 1970 liliwezesha kundi hilo kupata mkataba wa kurekodi, na mwaka 1973 walitoa albamu yao iliyouzwa sana, Amabutho.

Hatimae alikua kiongozi wa na mtunzi mkuu wa kwaya, akijikita zaidi katika nyimbo za Zulu waliocheza densi ya isicathamiya kikundi cha Afrika Kusini cha muziki wa kitamaduni ambao mara nyingi ulikua na muziki laini na densi ya kuvutia.

Walibatizwa Ladysmith Black Mambazo, jina ambalo limekuwa na umuhimu katika viwango kadhaa: Ladysmith waliwakilisha mji wao, Black ikimaanisha dume la ng'ombe lililokua lenye nguvu kijijini kwao, na Mambazo, kutoka neno la kizulu linalomaanisha shoka, ikiwa ni ishara ya uwezo wa kikundi hicho wa ushinda katika mashindano

Shindano la redio mnamo mwaka 1970 liliwezesha kundi hilo kupata mkataba wa kurekodi, na mwaka 1973 walitoa albamu yao iliyouzwa sana, Amabutho.

Walifanikiwa kutambulika duniani baada ya kupewa kazi ya kuimba katika albamu iliyouzwa mamilioni ya pesa ya Paul Simon iliyojulikana kama Graceland , hususan kwa wimbo wao Homeless,wimbo ulioandikwa na Shabalala akishirikiana na Simon, iliyotokana na wimbo wa harusi ya kitamaduni ya Wazulu.

Ruka YouTube ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa YouTube ujumbe

Bendi hiyo ilijiunga na Simon katika matamasha yake aliyoyafanyua katika sehemu mbali mbali duniani. Nae akazalisha albamu zao tatu- huku wimbo wa Shaka Zulu ukishinda tuzo ya Grammy ya wimbo bora wa kitamaduni uliorekodiwa

Shabalala alistaafu kucheza katika matamasha mwaka 2014 muda mfupi baada ya kucheza katioka tamasha lililoandaliwa kwa ajili ya Nelson Mandela.

Aliendelea kufundisha kwaya za muziki wa kitamaduni, huku watoto wake wanee wa kiume (na mjukuu wake mmoja) wakiendeleza kipaji chake ndani ya kundi la Ladysmith Black Mambazo.

Mwanamuziki huyo alikuwa pamoja na mke wake Thokozile Shabalala, katika nyakati za mwisho za maisha yake. alisema Xolani Majozi.

Taarifa ya kifo chake ilisambaa, na rambirambi zikatumwa kutoka maeno mbali mbali ya dunia.

"Radiki yangu, mkarimu mkubwa, Joseph Shabalala, amefariki asubuhi ya leo," aliandika mwanamuziki wa Afrika Kusini Sipho''Hotstix''Mabuse kwenye Titter. "Salamu zangu za rambirambiziifikie familia na rafiki zake ."

"Nimesikitika sana ,"aliandika Herman Mashaba, meya wa zamani wa mji wa Johannesburg. "Utakumbukwa kama mwanamuzki mkubwa wa Afika Kusini na muasisi katika sekta ya muziki ."

Short presentational grey line